Kambi ya Balozi Kagasheki yaendelea kuwatesa wananchi, hivi tutafika?

Nov 26, 2013
9
0
MANISPAA YA BUKOBA YAENDELEA KUWAKA MOTO
Hii inafuatia hatua ya baadhi ya madiwani wanaoongozwa na waziri wa maliasili na utalii, Balozi Khamis Kagasheki wanaotaka kumg'oa madarakani mstahiki Meya wa manispaa ya Bukoba, Anatory Amani kwa manufaa yao binafsi ya kuandika barua ya kutokuwa na imani ya ofisi ya mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali ambayo iliwasilishwa kwa mkurugenzi mtendaji wa manispaa hiyo.

Kwa mujibu taarifa madiwani hao wanadai kuwa mkaguzi huyo wa hesabu za serikali anachelesha kusoma taarifa ya tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka zinazomkabili kwa lengo la kumlinda, madiwani hao chini ya mwavuli wa Balozi Kagasheki wameishaunda mikakati ya mikali ya kumg'oa Meya huyo hata kama mapungufu ya tuhuma zinazoelekezwa kwake hazitabainika.

Kweli mikakati hiyo ni ya kuiendeleza manispaa au kuididimiza, kwa kuwa mgogoro kati ya kambi ya kagasheki na Mstahiki meya umechangia umaskini wa kukithiri katika manispaa ya bukoba, kwa sasa mzunguko wa fedha ni dogo sana, kama soko lingejengwa, standi ikajengwa na mradi wa world bank utaendelea manispaa ingekuwa juu sana na umaskini wananchi wangeusikia kwa majirani, je, Kagasheki anawatakia mema wananchi?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom