Kambi Ndogo yataka 'Kambi Rasmi' ya Upinzani Bungeni Iondolewe

Mkuu kumbe unasoma katikati ya mistari........hawa wamechoka sana....hamad rashid ni mroho wa madaraka na anatumika kuvuruga upinzani bara kwasababu wao wameshapata ulaji Zanzibar.

:clap2::clap2::clap2::clap2::clap2::clap2:
 
Kambi isiyo rasmi ya upinzani, imekusudia kuwasilisha hoja binafsi kuomba kutengua kanuni namba 131 ili kuondoa neno ‘kambi rasmi’ bungeni kwa nia ya kupewa nafasi ya uwenyekiti kwenye kamati za kudumu.
Mwenyekiti wa kambi hiyo, Hamad Rashid Mohamed, alisema jana kuwa lengo lao sio kupata marupurupu, bali ni kushirikishwa kwenye kamati.
Hamad, ambaye pia ni Mbunge wa Wawi (CUF), alisema tayari wameshajipanga kuwasilisha hoja hiyo ili vyama vingine vya upinzani viruhusiwe kuongoza baadhi ya kamati za bunge.
Hamad alimlaumu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, kwa kuishutumu CUF kwamba, inawasiliana na chama hicho kupitia vyombo vya habari wakati na wao (Chadema) hufanya hivyo akitolea mfano taarifa ya Kamati Kuu ya Chadema.
Hata hivyo, alisema walipokea barua kutoka Chadema inayosema kuwa chama hicho kitaunda serikali kivuli ndani ya Bunge bila kushirikisha vyama vingine.
“Sisi tulifahamu mapema. Tangu siku ya mdahalo, nilimwambia Mbowe, baada ya kusema kwamba, sisi tuna ushirikiano Zanzibar. Tulidhani Chadema wangeheshimu maamuzi ya wananchi kuhusu kuundwa kwa Serikali ya Umoja Kitaifa kwa sababu haya hayakuwa maamuzi ya CUF,” alisema. Alisema wamesikitika kwa hatua ya Chadema kuwatenga Wazanzibari kwa madai kuwa CUF sio chama cha upinzani tena.
“Tunataka kuwahakikishia Watanzania kwamba, CUF ni chama cha upinzani na tutaendelea kutetea maslahi yao kwa kuzingatia misingi ya haki na usawa, tofauti yetu na wao itakuwa moja tu tutaangalia zaidi maslahi ya taifa,” alisema.
Hamad alisema wataheshimu sheria na katiba ya nchi na kuchambua hoja zenye maslahi ya taifa.
Kuhusu Katiba mpya, Hamad alisema chama hicho kinataka rasilimali za nchi, ikiwamo ardhi, zisimamiwe na wananchi sio serikali.
Pia Katiba itamke wazi juu ya udhibiti wa malighafi za viwandani, yakiwamo madini ya uranium, mipaka ya raia, tume huru ya uchaguzi, mahakama ya kikatiba na kupunguza madaraka ya Rais.
Kuhusu tume huru, alisema rasimu, ambayo wameshaiwasilisha, inaeleza bayana kuhusu muundo wa tume hiyo kwa kupendekeza makamishna wawe wanaomba nafasi hizo na kuthibitishwa na Bunge

Source: IPP MEDIA.

Comment:
Hii ni safi sana.
Ulimbukeni na ulevi wa wadhifa wa ‘Kambi Rasmi ya Upinzani’ utaisha very soon.
Wabunge wa CCM watawaunga mkono mahasimu wa CHADEMA katika hiyo hoja na hivyo kuwalazimisha kuacha tabia hii mbaya ya ubinafsi.
Kwa hakika viongozi wa Chadema wamezidi kuonesha uchanga wao kisiasa. Na kwa mwenendo huu wanaweza kusababisha chama hicho kuondolewa kabisa kwenye kuongoza kambi ya upinzani na nafasi hiyo wakapewa wenzao.

Suala hili linawezekana kwa sababu mahasimu wao wana uungwaji mkono wa CCM iwapo itabidi kupigia kura suala hilo.
Sijui CHADEMA watakua lini…
Endeleeni na kiburi chenu na matokeo mtayaona.


kelele zanini? badilisheni kwanza kanuni za Bunge?Hamad nilijua utaumia sana kukosa malupulupu ya Uongozi wa kambi ya upinzani ndiyo maana inakuuma sana,siku hizi sikuoni tena ukibeba create za bia na soda pole sana ndiyo hivyo rafiki yangu ulijisahau ulitakiwa ujenge Chama badala ya kutanua na leo ungebaki na wadhifa wako labda,lakini kila kukicha mambo magumu pole.

Acha kelele fanya kazi katika nafasi uliyonayo usiwadanganye watanzania bwana 2005 tunajua wazi CUF hamkuwa na uwezo wa kutengeneza kambi peke yenu waache wenzenu wafanye kazi kanuni zinawaruhusu.Hatutaki udaku uliouanza mapema sana.Bahati mbaya uwajui wenzetu wa Ile rangi ya majani kwani wanakutumia na kukutupia hapo.
 
Lipumba mwenyekiti wa CUF kwa zaidi ya miaka 15; Cheyo ni mwenyekiti wa UDP kwa zaidi ya miaka 15, mrema ni mwenyekiti kwa zaidi ya miaka 15 [kupitia vyama mbalimbali] na Mbatia [sina kumbukumbu zake].; kwa mantiki hiyo rahisi utaona ni jinsi gani nyuma ya pazia la hiyo kambi isiyo rasmi ya upinzani kulivyochafuka kwa kujaza ma-sultani. Kwa hiyo hao jamaa hawapo pale kwa ajili ya kujenga taifa lijalo bali wapo kwa ajili ya kumaliza njaa zao na ndugu zao wa karibu. CUF, UDP, TLP huenda na NCCR-Mageuzi zimeshakuwa kampuni binafsi na si vyama vya siasa!! KIBAYA ZAIDI WAMEAMUA KUFANYA BIASHARA NA CHAMA TAWALA KWA KUINGIA MAKUBALIANO YA KIBIASHARA NA SI MAKUBALIANO YA KISIASA!!!
 
Back
Top Bottom