Kambi Ndogo yataka 'Kambi Rasmi' ya Upinzani Bungeni Iondolewe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kambi Ndogo yataka 'Kambi Rasmi' ya Upinzani Bungeni Iondolewe

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kishongo, Feb 3, 2011.

 1. Kishongo

  Kishongo JF-Expert Member

  #1
  Feb 3, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  [FONT=&quot]Kambi isiyo rasmi ya upinzani, imekusudia kuwasilisha hoja binafsi kuomba kutengua kanuni namba 131 ili kuondoa neno ‘kambi rasmi’ bungeni kwa nia ya kupewa nafasi ya uwenyekiti kwenye kamati za kudumu.[/FONT][FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]Mwenyekiti wa kambi hiyo, Hamad Rashid Mohamed, alisema jana kuwa lengo lao sio kupata marupurupu, bali ni kushirikishwa kwenye kamati.[/FONT][FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]Hamad, ambaye pia ni Mbunge wa Wawi (CUF), alisema tayari wameshajipanga kuwasilisha hoja hiyo ili vyama vingine vya upinzani viruhusiwe kuongoza baadhi ya kamati za bunge.[/FONT][FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]Hamad alimlaumu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, kwa kuishutumu CUF kwamba, inawasiliana na chama hicho kupitia vyombo vya habari wakati na wao (Chadema) hufanya hivyo akitolea mfano taarifa ya Kamati Kuu ya Chadema. [/FONT][FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]Hata hivyo, alisema walipokea barua kutoka Chadema inayosema kuwa chama hicho kitaunda serikali kivuli ndani ya Bunge bila kushirikisha vyama vingine.[/FONT][FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]“[/FONT][FONT=&quot]Sisi tulifahamu mapema. Tangu siku ya mdahalo, nilimwambia Mbowe, baada ya kusema kwamba, sisi tuna ushirikiano Zanzibar. Tulidhani Chadema wangeheshimu maamuzi ya wananchi kuhusu kuundwa kwa Serikali ya Umoja Kitaifa kwa sababu haya hayakuwa maamuzi ya CUF,” alisema. Alisema wamesikitika kwa hatua ya Chadema kuwatenga Wazanzibari kwa madai kuwa CUF sio chama cha upinzani tena.[/FONT][FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]“[/FONT][FONT=&quot]Tunataka kuwahakikishia Watanzania kwamba, CUF ni chama cha upinzani na tutaendelea kutetea maslahi yao kwa kuzingatia misingi ya haki na usawa, tofauti yetu na wao itakuwa moja tu tutaangalia zaidi maslahi ya taifa,” alisema.[/FONT][FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]Hamad alisema wataheshimu sheria na katiba ya nchi na kuchambua hoja zenye maslahi ya taifa.[/FONT][FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]Kuhusu Katiba mpya, Hamad alisema chama hicho kinataka rasilimali za nchi, ikiwamo ardhi, zisimamiwe na wananchi sio serikali.[/FONT][FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]Pia Katiba itamke wazi juu ya udhibiti wa malighafi za viwandani, yakiwamo madini ya uranium, mipaka ya raia, tume huru ya uchaguzi, mahakama ya kikatiba na kupunguza madaraka ya Rais.[/FONT][FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]Kuhusu tume huru, alisema rasimu, ambayo wameshaiwasilisha, inaeleza bayana kuhusu muundo wa tume hiyo kwa kupendekeza makamishna wawe wanaomba nafasi hizo na kuthibitishwa na Bunge[/FONT][FONT=&quot][/FONT]

  Source: IPP MEDIA.

  Comment:
  Hii ni safi sana.
  Ulimbukeni na ulevi wa wadhifa wa ‘Kambi Rasmi ya Upinzani’ utaisha very soon.
  Wabunge wa CCM watawaunga mkono mahasimu wa CHADEMA katika hiyo hoja na hivyo kuwalazimisha kuacha tabia hii mbaya ya ubinafsi.
  Kwa hakika viongozi wa Chadema wamezidi kuonesha uchanga wao kisiasa. Na kwa mwenendo huu wanaweza kusababisha chama hicho kuondolewa kabisa kwenye kuongoza kambi ya upinzani na nafasi hiyo wakapewa wenzao.

  Suala hili linawezekana kwa sababu mahasimu wao wana uungwaji mkono wa CCM iwapo itabidi kupigia kura suala hilo.
  Sijui CHADEMA watakua lini…
  Endeleeni na kiburi chenu na matokeo mtayaona.
   
 2. Ernesto Che

  Ernesto Che JF-Expert Member

  #2
  Feb 3, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,117
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Unachonifurahisha unatoa mada mwenyewe, unachambua mwenyewe, unatoa mwelekeo mwenyewe, hatimaye unahitimisha mwenyewe. This shows how "ignorant one sided man'you are. Kuna haja ya kuchangia?? sidhani!
   
 3. coscated

  coscated JF-Expert Member

  #3
  Feb 3, 2011
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 254
  Trophy Points: 180
  :car:
   
 4. Horseshoe Arch

  Horseshoe Arch JF-Expert Member

  #4
  Feb 3, 2011
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 11,230
  Likes Received: 4,951
  Trophy Points: 280
  ''Unachonifurahisha unatoa mada mwenyewe, unachambua mwenyewe, unatoa mwelekeo mwenyewe, hatimaye unahitimisha mwenyewe...Kuna haja ya kuchangia??''

  Inatosha mkuu...ndizo dalili za mfa maji!
   
 5. Nono

  Nono JF-Expert Member

  #5
  Feb 3, 2011
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,305
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Ni rahisi kufikiri hivyo, ila utekelezaji unaweza kuwa mgumu kidogo kwani kunakuwa na pande mbili ambazo ni vigumu kushiriki kwa upande mmoja. Ikiwa chama kilichopata ushindi ndicho kinachounda serikali, basi chama kinachofuata kwa kura nyingi ndicho kitakachokuwa kiongozi kwa upande wa upinzani. Na kwa hili sidhani kama chama kitakachokuwa kimeunda serikali itakuwa sahihi kwao kuwa na kura katika kuchagua kiongozi wa kundi hili. Hivyo kwa vyovyote CDM hata kama kifungu cha kambi rasmi kitatenguliwa itaendelea kuwa na uongozi wa kambi ya upinzani bungeni.
   
 6. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #6
  Feb 3, 2011
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  wafa maji ni chadema
   
 7. Mabel

  Mabel JF-Expert Member

  #7
  Feb 3, 2011
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 1,018
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Mkuu, Spika kasha sema hakuna kitu kinaitwa 'KAMBI ISIYO RASMI' na neno RASIMI halikuwepo katika kanuni za Bunge ila HAMAD RASHID alishinikiza iwe hivyo baada ya bwana Mapesa kumbwaga katika kinyang'anyiro cha unyekekiti wa kamati fulani inayoundwa na kambi ya upinzani. Hamad alifanya hivyo akijua kuwa CUF siku zote itaendelea kuongoza kambi ya upinzani bungeni akitegemea mtajia wa wabunge kutoka Zenji. CUF wanayao madudu pia, walikuwa nayo wanajaribu kuyaficha kwa wakati huu!
   
 8. Mdau

  Mdau JF-Expert Member

  #8
  Feb 3, 2011
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,771
  Likes Received: 252
  Trophy Points: 180
  Muungano huu unazidi kuelekea kwenye matatizo......YAANI MBUNGE WA WAWI, ambayo ni kama kijitongoji tu huku bara anataka anyime haki wananchi wa Tanzania Bara wa majimbo karibu 30, tena ambao ni mara kumi hata ya Zanzibar yote?????? Hamad Rashid unafiki na uroho unampeleka pabaya jamani!!!!
   
 9. Mimibaba

  Mimibaba JF-Expert Member

  #9
  Feb 3, 2011
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 4,566
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Ebu MODs wahurumieni hawa na njaa zao wafungieni maisha. Boring. Is JF political confrotation or just constructive forum for exchanging of great ideas?
   
 10. Ernesto Che

  Ernesto Che JF-Expert Member

  #10
  Feb 3, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,117
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Unajua wanajaribu ku - twist mind za watu wenye fikra sahihi. Ila wanachosahu ni kwamba hatuwezi kudanganywa na "cheap arguments" kama hizo tuna busara za kutosha. Wajaribu mbinu nyingine! This is too much
   
 11. eliesikia

  eliesikia JF-Expert Member

  #11
  Feb 3, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 423
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 45
  Kishongo hivi unajua neno Kambi rasmi ililetwa na nani bungeni??? Kama sio Hamad Rashid ili awakomoe akina Marando mwaka 1995??

  Wameshafulia hao kila kitu wao.. Mbona CHADEMA walinyamaza kimya wakati CCM na CUF kule zanzibar wanakubaliana mambo kwa usiri na kuwatenga wengine kwenye serikali ya Zanzibar??
  Waamue moja tuu hawa wapemba
   
 12. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #12
  Feb 3, 2011
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,641
  Likes Received: 1,429
  Trophy Points: 280
  sichangii hii kabisa naogopa:ban:
   
 13. T

  Tata JF-Expert Member

  #13
  Feb 3, 2011
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,734
  Likes Received: 655
  Trophy Points: 280
  Naomba nikumbushwe kidogo. Hivi CUF imeshirikisha wapinzani wengine kwenye serikali ya Umoja wa Kitaifa kule Zanzibar? Mbona wanalia sana kutengwa huku bara wakati wenyewe hawashirikishi vyama vingine kwenye uongozi wao wa pamoja na CCM?
   
 14. nsimba

  nsimba JF-Expert Member

  #14
  Feb 3, 2011
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 785
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  :clap2:
   
 15. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #15
  Feb 3, 2011
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,635
  Likes Received: 4,743
  Trophy Points: 280
  Ni kawaida ya watu wa visiwani, ni wabinafsi mno chao chao na chetu chao, safari hii wamekwama hakuna mteremko, yaani wabunge wao wanaochaguliwa na watu elf moja wanataka wawe na hadhi sawa na mbunge aliyechaguliwa na watu laki moja , HAPANA. CUF ridhikeni na milichopata, nyie ni chama tawala bana.
   
 16. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #16
  Feb 3, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Kumbe ishu ni vyeo..omg...cuf kweli ni walevi wa vyeo.

  Kumbe mahasimu wa cdm ambao ni ccm wanatawaunga mkono cuf..nimeipenda hii. Inaonesha jinsi gani mlivyo kinyonga!
   
 17. mgen

  mgen JF-Expert Member

  #17
  Feb 3, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 15,180
  Likes Received: 1,904
  Trophy Points: 280
  Tumewachoka wajameni na yenu ya kuleta kila kukicha wekeni hata ratiba ya katiba hayo mnayo bwabwaja hatuja watuma aslan.
  AR kwani usirudi pemba kufaidi popo nundu balahau!
   
 18. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #18
  Feb 3, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Mkuu kumbe unasoma katikati ya mistari........hawa wamechoka sana....hamad rashid ni mroho wa madaraka na anatumika kuvuruga upinzani bara kwasababu wao wameshapata ulaji Zanzibar.
   
 19. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #19
  Feb 3, 2011
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,598
  Likes Received: 3,888
  Trophy Points: 280
  Jamani mswali mengine, hao wengine wamepata kura ngapi , ebu andika chadema walipata kura ngapi zanzibar?? kwenye kura za urais?? inaonekana furaha ya ccm inataimizwa na tabia hizi
   
 20. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #20
  Feb 3, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Cheap prostitute!
   
Loading...