Kambayuwayu ka Kikwete kalikotaka kuwa tetere!

Mkwere kama na yeye ni mfanyakazi (ndege) basi ndege mjinga anayenasa katika tundu lake kwani kathibitisha na kuonyesha true colours lakini mimi kinachoniuma ni kuwa pamoja na hay yote lakini utasikia eti ameshinda kwa kishindo au ndo matetere wanamsaidia ushindi? Mibundi ndo rafiki zake huyu mkwere
 
Halafu kama hamjashtukia Mkwere (mwenye shamba) ni bonge la msanii yaani zile emotions alizoonyesha katika speech zote feki tu katika kuwapata UMBA sintoshangaa aliporudi palace akawa anafurahia na mamsup na kupokelewa na makundi ya kina tetere wakisema "You have done it....You nailed right there, those little mbayuwayus must bow for us" lol!!
 
asante mwana kijiji,
kwa hadithi ya kuhoji,
vijiji na kwenye miji,
tunakolalia uji.

hata tangu zile zama,
mkwere zake ngoma,
haukumbuki mtama,
awapo kwenye magoma.

tulimwangalia sura,
kisha tukampa kura,
amejifanya kinara,
sura ameivisha pira.

mende kwake msalani,
hata kule jalalani,
ukimfuga kabatini,
umemuweka shakani.

yatupasa kujifunza,
kofia sije tuponza,
mbeleni kujiuguza,
kesho na iwe ya kwanza.
 
...wakati Nyerere anazungumzia uchaguzi wa mwaka 1995, aliulizwa ni nani waliye mgroom kuwa next president... akajibu, "wenye macho wanaona!" Hivi ni nani anayefaa kuwa Rais Tanzania, tukiangalia pande zote? Huyu mbayuwayu nilipokuwa mdogo hata mie nilijaribu kumtungua kwa Vesi (manati), lakini mara nyingi nilimkosa, aliruka huyo pruuu na kwenda zake, na wanapokuwa kwende kundi ndo wazidi kukudanganya, kumbe ni wadogo mno, huwezi kupiga hata mbawa zao! Muheshimiwa anajaribu kupiga manati mbayuwayu... hapa nadhani atakuwa anatokota.
 
He was right.

Kikwete is right.
Mnaomuona Kikwete kama tatizo mjuwe nyinyi ndiyo tatizo. Nimeona wengi wetu humu tunafata mkumbo tu na muelekeo wa mkimbiza bendera, akitokea mtu akisema "Kikwete kakosea...", "...Kikwete hachaguliki...", "...Kikwete ana hivi ana vile...", wengi wanaungana naye blindly tu na wengine wanafika mbali zadi kwa kuonyesha wazi kuwa wanampinga Kikwete kama Kikwete na yanayomhusu Kikwete binafsi kando na uongozi wake.
Narejea tena kuwa kwa yote yanayotokea nchi hii Kikwete si tatizo kabisa na hajawahi kuwa tatizo...vuta matatizo yote ya nchi hii uweke mezani, Kikwete atabakia si tatizo.
Tatizo ni CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM).
Msitake tuamini kuwa shida za wananchi wa Tanzania zimekuja baada ya Kikwete kuwa rais, wala msitake ionekane kuwa Tanzania ilikuwa nchi ya 'asali' na 'maziwa' kabla ya Kikwete kuwa rais.
Ufisadi unaopigiwa kelele, umasikini,ujinga, maradhi na matatizo haya ya wafanyakazi yamekuwa ni sehemu ya maisha ya watanzania kwa kipindi chote cha utawala mbovu wa sera zilizoshindwa za CCM.
Leo tunasema "Kikwete hachaguliki", sawa, tuseme Kikwete mwenyewe anakubaliana na mawazo hayo na kuamua kukaa pembeni, hebu tuambiane kweli mtu atakaye kuja badala yake ndiyo ataweza kuleta hayo mabadiliko 'tunayoyaota' kila siku?
Tokea CCM iasisiwe mpaka leo mtu anambie ni mwaka upi walau tunaukumbuka kuwa maisha yalikuwa afadhali chini ya CCM?
Viongozi wote waliomtangulia Kikwete walitawala kwa kufuata ilani ya chama cha Mapinduzi kama walivyoinadi kwa wananchi, kadhalika na Kikwete. Ni sawa tu nikisema anavyofanya Kikwete ni sawa na yale waliyofanya watangulizi wake...kupitia sera na ilani ya chama hicho hicho.
Hata Kikwete akiondoka leo madarakani, mrithi wake hatoweza katu kuwaongeza mshahara wanaoutaka wafanyakazi seuze kupambana na ufisadi wala kubadilisha hali za maisha ya wananchi masikini. CCM itabaki kuwa ni ile ile iliyoshindwa kuondoa ujinga, maradhi na umasikini wakati wa Nyerere, ikafisidi nchi wakati wa Mwinyi, ikazaa matajiri wezi na wanya'nganyi wa nchi hii wakati wa Mkapa na ndiyo hiyo hiyo ya Kikwete inayoyaendeleza yote hayo ya awali.
Hapa tatizo la Kikwete lipo wapi kama Kikwete?
Watanzania msipoteze mda, CCM haifawi tena, imekuwa ni " Mbwa mkongwe asiyeweza mbinu mpya", hata ashuke Malaika kuiongoza katika hali kama hii, hakuna kitakachobadilika. Msiichaguwe CCM wala wabunge wake, miaka zaidi ya 40 ya CCM, kama haitoshi wananchi kujifunza basi 40 mingine haitatosha kusubiri "maisha bora kwa kila Mtanzania".
 
ukali huo angekuwa ameuonyesha kwa mafisadi wa EPA, Richmond, Rada, Meremeta et al., kwenye madini, uvuvi nk rasilimali zetu zingepona.

Yaani we acha tu. Kama ukali ni kuzima madai ya walio wengi wenye kutaabika na maisha ilihali wachache wanaoiba na kudhulumu wanaendelea kutumia mazuria mekundu basi kila la kheri kwenu wenye nchi!!!
 
tatizo ni watendaji kutokusanya kodi ipasavyo mpaka wanamfanya rais wao aseme nchi haina pesa
rais nakushauri ukawabane wenye migodi ili watoe kodi tuweze kuwalipa wafanyakazi wetu
si unajua ugomvi na wafanyakazi hauna tija, pili tupunguze semina za wazee wapate milioni chache
kwani sioni ufanisi wao
 
Kikwete is right.
Mnaomuona Kikwete kama tatizo mjuwe nyinyi ndiyo tatizo. Nimeona wengi wetu humu tunafata mkumbo tu na muelekeo wa mkimbiza bendera, akitokea mtu akisema "Kikwete kakosea...", "...Kikwete hachaguliki...", "...Kikwete ana hivi ana vile...", wengi wanaungana naye blindly tu na wengine wanafika mbali zadi kwa kuonyesha wazi kuwa wanampinga Kikwete kama Kikwete na yanayomhusu Kikwete binafsi kando na uongozi wake.
Narejea tena kuwa kwa yote yanayotokea nchi hii Kikwete si tatizo kabisa na hajawahi kuwa tatizo...vuta matatizo yote ya nchi hii uweke mezani, Kikwete atabakia si tatizo.
Tatizo ni CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM).
Msitake tuamini kuwa shida za wananchi wa Tanzania zimekuja baada ya Kikwete kuwa rais, wala msitake ionekane kuwa Tanzania ilikuwa nchi ya 'asali' na 'maziwa' kabla ya Kikwete kuwa rais.
Ufisadi unaopigiwa kelele, umasikini,ujinga, maradhi na matatizo haya ya wafanyakazi yamekuwa ni sehemu ya maisha ya watanzania kwa kipindi chote cha utawala mbovu wa sera zilizoshindwa za CCM.
Leo tunasema "Kikwete hachaguliki", sawa, tuseme Kikwete mwenyewe anakubaliana na mawazo hayo na kuamua kukaa pembeni, hebu tuambiane kweli mtu atakaye kuja badala yake ndiyo ataweza kuleta hayo mabadiliko 'tunayoyaota' kila siku?
Tokea CCM iasisiwe mpaka leo mtu anambie ni mwaka upi walau tunaukumbuka kuwa maisha yalikuwa afadhali chini ya CCM?
Viongozi wote waliomtangulia Kikwete walitawala kwa kufuata ilani ya chama cha Mapinduzi kama walivyoinadi kwa wananchi, kadhalika na Kikwete. Ni sawa tu nikisema anavyofanya Kikwete ni sawa na yale waliyofanya watangulizi wake...kupitia sera na ilani ya chama hicho hicho.
Hata Kikwete akiondoka leo madarakani, mrithi wake hatoweza katu kuwaongeza mshahara wanaoutaka wafanyakazi seuze kupambana na ufisadi wala kubadilisha hali za maisha ya wananchi masikini. CCM itabaki kuwa ni ile ile iliyoshindwa kuondoa ujinga, maradhi na umasikini wakati wa Nyerere, ikafisidi nchi wakati wa Mwinyi, ikazaa matajiri wezi na wanya'nganyi wa nchi hii wakati wa Mkapa na ndiyo hiyo hiyo ya Kikwete inayoyaendeleza yote hayo ya awali.
Hapa tatizo la Kikwete lipo wapi kama Kikwete?
Watanzania msipoteze mda, CCM haifawi tena, imekuwa ni " Mbwa mkongwe asiyeweza mbinu mpya", hata ashuke Malaika kuiongoza katika hali kama hii, hakuna kitakachobadilika. Msiichaguwe CCM wala wabunge wake, miaka zaidi ya 40 ya CCM, kama haitoshi wananchi kujifunza basi 40 mingine haitatosha kusubiri "maisha bora kwa kila Mtanzania".

tunaweza kuwalipa wafanyakazi wetu kama tukisimamia rasilimali zetu vizuri, kwani unajua makampuni ya simu
pamoja na mikodi wanapata msamaa wa kodi kiasi gani, ni kitu cha ajabu kusema nchi yetu haiwezi kulipa
mishahara mizuri cha msingi tuongeze mapato kutokana na rasilimali zetu kwani mbona boswana wao
wameweza kulipa wafanyakazi wao vizuri kwani wana nini cha kutuzidi kwenye rasilimali?
 
yaani, ile jazba aliyoinoesha jana sijawahi kumuona akiwa nayo kwenye suala lolote nyeti la kitaifa..!!

Si wajua ukiwa mpenda sifa kwa wageni. Si umemuona mwanausalama Kova akipewa 'special coverage' hapo ITV kupiga mkwara atakayebeba mabango akisisitiza 'Tanzania Kisiwa cha Amani'
 
umasikini wa akili ndio tatizo letu!!!!! ..............nchi ni yake? au .....acha ukali baba utakosa kura kwa mjini mwaka 2010.....tumekasirika sana ulivyolopoka.....utaona
 
Jamani tutatunga mashairi,tutabeza ,tutaandika makala za kila aina lakini mgomo haukufanyika!!!Tena katika siku ambazo wafanyakazi wamewahi kufika kazini ni leo ya tarehe 5 ,wameulizwa kulikoni leo mnawahi kuliko za siku kawaida ?Wamejibu we achaaa!!!Tufukuzwe ?Hao ndiyo wafanyakazi Watanzania!!
 
Ameonyesha ni jinsi gani anaweza kuwa mkali ukijaribu kugusa maslahi yake na jamaa zake. Ashaelezwa kuwa akitoa mshahara huo kwa mbaywayu, hatapata hela ya kuagizia Ma VX na tripu kibao za ugaibuni. Ndio maana aliwaambia kuwa kwa mshahara huo hazina itakwisha!! kitu ambacho sicho.

Mbona inapokuja suala la marupurupu ya wakubwa, wabunge, mawaziri na safari zake hafanyi hiyo cost analysis????
 
yaani, ile jazba aliyoinoesha jana sijawahi kumuona akiwa nayo kwenye suala lolote nyeti la kitaifa..!!

Jazba ile ilikuwa ni lazima kwa sababu mgomo ulihatarisha ulaji wake, na ulaji wa CCM, hebu fikiria kama ungeungwa mkono na waajiriwa wote including Polisi & Jeshi kwani hata na wao wanawaeleza wenzao kuwa "mkatuwakilishe vyema sie haturuhusiwi kugoma lakini cha moto nasi twakiona" ukweli huo JK anaujua vyema na hataki kuwe na ndoa ya namna hiyo asilani, Mzee MKJJ angalia bajeti ijayo itakavyouma na kupuliza hasa kwa wanaotegemewa kusukuma jahazi Octoba na wengine watakavyoachwa solemba
 
Safi sana - upeo mkubwa mkuu - nimesoma inaonyesha uchungu sana njisi mbayuwayu anavyohaha shambani kwa mkulima pamoja na kufanya kazi zote hizo lakini hapati haki kama ndege wengine. Tetere ndiyo wanatesa tu shambani wanaonekana wafalme na mwenye shamba hana la kusema juu ya ndege hawa.

Nimejifunza yafuatayo

Mkulima pamoja na juhudi zake za kuwa na shamba zuri lakini uongozi wa shamba lake ni weak, ana upendeleo kwa baadhi ya ndege.

Uamuzi wa Mbayuwayu kuahirisha mgomo wao ni mzuri sababu hata kama wangeamua kugoma yale mapaka ya mwenye shamba yangewamaliza wote maana yalikuwa yamepewa kibali cha kuwamaliza.

Ndege wote shambani kwa mkulima huyu hawana umoja sababu masilahi yao ni tofauti - kwa mantiki hiyo hata mgomo unakuwa na walakini. Laiti umoja huo ungekuwapo ndege wote wangeungana na Mbayuwayu na kumdhibiti mwenye shamba kwa urahisi zaidi.

Mbayuwayu arudi aendelee kuishi shambani kwa mkulima huyu kwa kudra za mwenyezi mungu huku akijipanga ni njisi gani ataweza kumdhibiti mwenye shamba siku za usoni - ni kazi sana sababu mwenye shamba akigundua anaweza kuwateketeza mbayuwayu wote na kuanza upya kwa hiyo umakini unahitajika kwa mbayuwayu wote.
 
<object width="640" height="385"><param name="movie" value="http://www.youtube.com/v/y2V9hQZ5lg...&feature=player_embedded&fs=1"></param><param name="allowFullScreen" value="true"></param><param name="allowScriptAccess" value="always"></param><embed src="http://www.youtube.com/v/y2V9hQZ5lg...x4e9e00&hl=en_US&feature=player_embedded&fs=1" type="application/x-shockwave-flash" allowfullscreen="true" allowScriptAccess="always" width="640" height="385"></embed></object>

Milio mizuri tu ya mbayuwayu
 
Haya mambo ni mazito. Mimi nasubiri kikao cha Tarehe 8/5/2010 kama walivyokubaliana.

KWA KWELI HII NGOMA!!!!! MHHHHHHHHHHHHHHHHHHH.
 
Haya mambo ni mazito. Mimi nasubiri kikao cha Tarehe 8/5/2010 kama walivyokubaliana.

KWA KWELI HII NGOMA!!!!! MHHHHHHHHHHHHHHHHHHH.

Tusitegemee lolote jipya.Ameshaapa kuwa hata kama ni miaka 8 ijayo kamwe TUCTA wasitegemee kupata wanachotaka.Sasa kama ana maamuzi tayari kuna suluhu hapo?
 
Tusitegemee lolote jipya.Ameshaapa kuwa hata kama ni miaka 8 ijayo kamwe TUCTA wasitegemee kupata wanachotaka.Sasa kama ana maamuzi tayari kuna suluhu hapo?

Inaelekea hapa alijihesabia kipindi chake cha pili (ambacho ana uhakika nacho) na miaka mingine 3 kwa atakayemrithi ndiyo mbayuwayu wairudishe hoja mezani....
 
Back
Top Bottom