Kamati za ulinzi na usalama zisaidie kukamata mafisadi, kwani nao wanahatarisha usalama wa nchi

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
0
Kwa kuwa sasa hivi kamati za ulinzi na usalama zinaonekana kujiingiza katika masuala ya kipolisi, yaani kuwaelekeza polisi nani akamatwe – wale wanaohatarisha ulinzi na usalama, basi ingefaa kamati hizo sasa ziwe zinaelekeza kukamatwa kwa mafisadi, kwani ufisadi ni jinai inayoweza kuhatarisha usalama na amani na utulivu wa nchi.

Haya ninayosema siyatungi kichwani mwangu kwani yameandikwa katika Sheria ya Kupambana na Rushwa (PCCB Act No. 11 of 2007). Ninanukuu hapa sentensi ya kwanza ya Utangulizi (preamble) ya Sheria hiyo iliyopitishwa na Bunge letu:


"WHEREAS corruption is an obstacle to principles of democracy, good governance and human rights and poses a threat to peace, tranquillity and security in the society;…..

Hivyo basi ufisadi unahatarisha usalama wan chi, hivyo hizi kamati za ulinzi na usalama zisaidie kutoa amri kwa polisi kuwasaka na kuwakama mafisadi wote katika maeneo yao.

Wasijikite tu katika kukamata watu, hasa viongozi wa upinzani wanaotoa hoja mbadala majukwaani kwa kuwaita eti wanatishia usalama, ufisadi (na hivyo mafisadi) wameandikwa kabisa in black and white katika sheriua kwamba ni wavunjifu wakubwa wa amani na usalama wan chi.

Wanabodi nawasilisha…
 

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
0
Hakuna ishu ambayo magamba wanaiogopa kama ukoma kama ishu ya kupambana na ufisadi seriously. Lakini by the way, hizo kamati za ulinzi na usalama wajumbe wake ni kina nani hasa. nani anawachagua, zipo kikatiba na jee pia wamo wapinzani?

Mie naona ni mavitu ya CCM wanayoanza sasa kuyatumia sana kujinasua kutoka ndoano iliyowanasa! Na imewanasa barabara!
 

marejesho

JF-Expert Member
Jan 6, 2011
6,640
2,000
Haitakaa iwezekane kwa mfumo uliopo sasa!!! Hii inamaanisha kwamba,waanze kujikamata wenyewe!!!!!!
 

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
0

Unazungumza nini? nani amekuambia eti CCM wapambane na ufisadi? From top (and I mean top) to bottom wanasurvike na ufisadi na inashangaza kuona hadi sasa amani hoyo unayosema bado ipo!

CCM watambue apangayo Mungu hata katika wiki mbili zijazo hakuna anayejua, ni siri yake, na Watanzania wasiamini kauli za CCM kwamba vurugu za mikutanoni hapa na pale ndizo zitavinja amani.

Amani zitavunjwa pale tu nguzo zinayojenga haki zitaanguka, na nikitazama sana naona nguzo hizo zimepasuka sana!
 

KXY

JF-Expert Member
Dec 31, 2011
877
250
hebu nikumbushe na ile kamati ya usalama ya bunge inajukumu gani tafadhali
 

ungonella wa ukweli

JF-Expert Member
Mar 27, 2012
4,211
0
Kazi ya hizi kamati mkuu,ni kushughulia wanasiasa wa upinzani mkuu,wanaopatikana katika maeneo husika na si mafisadi. Ukitaka kamati hizi zifanye kazi ni suala la kutoa amri kwa mapolis kukamata na kudhalilisha wabunge na madiwani wa upinzani. Basiii.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom