Kamati za ulinzi na usalama na mitafaruku ya kisiasa wakati wa uchaguzi majimboni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kamati za ulinzi na usalama na mitafaruku ya kisiasa wakati wa uchaguzi majimboni

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mghaka, Sep 21, 2011.

 1. M

  Mghaka JF-Expert Member

  #1
  Sep 21, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 320
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Vyama vya siasa ebu nisaidieni kuuliza hili kwa mwenyekiti wa TUME YA UCHAGUZI. Kukosekana kwa upendo mara nyingi hutokana na mashaka ya kutuhumiana kwa pande mbili zenye ushindani hasa katika suala la kisiasa. Upande mwingine unaona kuna mazingira ambayo marefa wanashabikia au kusaidia upande mwingine kushinda.

  Upande moja unaona kuwa haupewi nafasi na pale unapopewa nafasi haulindwi ili kutekeleza majukumu yake ipasavyo. Agenda yangu ya leo ni kwamba wenyeviti wa kamati ya Ulinzi na Usalama wa wilaya ni Wakuu wa Wilaya ambao kimsingi ndio kama mabosi wa viongozi wa vyombo vya dola amabvyo vinasimamia haki na usalama wa siasa zenyewe.

  Wakuu wa wilaya na mikoa ni makada wa Chana tawala. Na sote tumeona wakati wa uchaguzi agenda ya kuwapo kwa amani ni ya muhimu na ni ya lazima sasa unapokuwa na wakuu wa wilaya ambao wanaona uhitaji wa kushinda uchaguzi kwa chama chao ni kipaumbele wanawezaji kuwa neutral na wasitumie kipengele cha amani kuwagandamiza washindani wao.

  Hivi DC aliyedaiwa kusema bila aibu CHADEMA walikusudia kumbaka anawezaji kuwa neutral wakati wa kikao cha kamati ya ulinzi na usalama? anawezaji kutoa haki? Anawezaje kuacha kutumia jukwaa la kamati ya ulinzi na usalama kufanya siasa?
   
Loading...