Kamati za bunge zinatimiza wajibu wake ipasavyo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kamati za bunge zinatimiza wajibu wake ipasavyo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by rodrick alexander, Apr 16, 2012.

 1. r

  rodrick alexander JF-Expert Member

  #1
  Apr 16, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 4,112
  Likes Received: 1,499
  Trophy Points: 280
  kamati za bunge zinatimiza wajibu wake ipasavyo
  juzi juzi katibu mkuu wa ccm ndugu wilson mukama aliitisha mkutano na kulalamika namna kamati za bunge zinavyoendesha shuguri zake alisema kazi ya kamati ni kufatilia,kuhoji na kuwasilisha taarifa zake bungeni ili zijadiliwe na kutolewa maamuzi.lakini kamati hizo zimekuwa zikifanya maamuzi kinyume na kanuni zilizotumika kuziunda kama kukata mishahara ya watumishi,kufungia viwanda au mashirika na kutoa taarifa kwenye vyombo vya habari kabla taarifa hizo hazijawasilishwa bungeni.nimekuwa nikifattilia kazi ya kamati hizo kwa muda mrefu lakini utendaji wake umekuwa ni wa kutia mashaka na kujitafutia umaarufu kwa wananchi ukiondoa kamati iliyokuwa ikiongozwa na dr slaa kama mna kumbuka kuna kipindi hamadi rashidi ambaye ni mbunge wa cuf wakati akiongoza mojawapo ya kamati hizo aliibua utata wa fedha za mauzo ya almas zilizokuwa zimehifadhiwa london nini mwisho wake?je tuhuma hizo zilijadiliwa bungeni. Kama zilijadiliwa ni hatua gani zilichukuliwa?tuhuma nzito kama hizo zinazohusu pesa za walipa kodi hazitakiwi ziachwe hivihivi mpaka sasa hivi siyo bunge wala hivyo vyombo vya habari vimeweza kutupatia hatma ya pesa hizo.kamati ya zito iliwahi kuibua tuhuma ya jinsi baadhi ya maofisa wa ndc walivyotumia dhamana za ndc ili kampuni binafsi ipate mkopo pamoja na tuhuma nzito lakini juzijuzi bodi mpya ya ndc imeteuliwa na mzindakaya ambaye alikuwa mwenyekiti wa bodi amerudishwa na wala hatujasikia hatua zozote zilizochukuliwa kwa watuhumiwa.sakata la tbs wakati bado jipya waziri wa viwanda ameteua bodi mpya ya tbs na mkurugenzi mkuu wa tbs bado anadunda kazini.bado hatujasahau mikutano iliyokuwa inaitishwa na mwenyekiti wa kamati ya nishati na madini january makamba kwa waandishi wa habari juu ya matatizo ya umeme nini kimefanyika umeme umepandfa bei na bado umeme umekuwa siyo wa uhakika na hata kamati ya mwakyembe waliokuwa watuhumiwa wa richmond walipoanza kujisafisha na kulalamika wameonewa mwakyembe aliomba sakata hilo lirudishwe bungeni ili waeleze mambo waliyoyaacha hili kulinda hadhi ya serikari .pia sakata la pesa za nssf ambazo ziliwekezwa kwenye kampuni za general tyre na kiwira zitto kabwe kwa kutumia madaraka yake kama mwenyekiti wa kamati aliizuia nssf isichukue hatua ya kupata pesa zake na kushikiria maamuzi ya nssf iondeshe kiwira wakati pesa za nssf ni za wanachama ambao ni wafanyakazi wa kawaida sio za serikali.lakini pia kuna sakata la baadhi ya wajumbe wa kamati hizi kuomba hongo ambalo pamoja na kuripotiwa kwa spika bado hatua sahihi hazijachukuliwa hali inayonifanya niamini kuna mchezo unaochezwa nyuma ya pazia kwenye hizi kamati.hii tabia ya kamati hizi kukimbilia kwa vyombo vya habari haitusaidii sisi wananchi kwani vyombo vyetu baada ya kuripoti habari hizi huwa hawafatilii mwisho wake.tunataka kama wamegundua uozo waupeleke bungeni ujadiliwe na kutolewa maamuzi ya kisheria ili wahusika wachukuliwe hatua
   
 2. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #2
  Apr 16, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu font inataka nitumie miwani ya 3D!
   
 3. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #3
  Apr 16, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  dah,pole kitoch changu kinaonesha vzuri,
  mtoa mada,NADHAN LEO UMESKIA KUWA WABUNGE WALIOINGIA MJENGON WAMEINGIA KWA HONGO,so waunda kamat ndo watoa hongo,
  hawatakua na kuhoji
   
 4. r

  rodrick alexander JF-Expert Member

  #4
  Apr 17, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 4,112
  Likes Received: 1,499
  Trophy Points: 280
  Ninachotaka wakina zitto na mrema wasiishie kuitisha mikutano na wanahabari wapeleke taarifa bungeni zijadiliwe na kutolewa maamuzi
   
 5. w

  wakijiwe Member

  #5
  Apr 17, 2012
  Joined: Apr 8, 2012
  Messages: 34
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mafanikio ya kamati zote za bunge ni kuona yale yanayoibuliwa yanachukuliwa hatua stahiki kwa uwazi na kuwawajibisha wanaohusika na tuhuma, kitendo cha kutochukua hatua wakati kamati zimefanya ufuatiliaji ni kupoteza rasilimali na nguvu kazi yaani bora wangekaa bungeni na kusinzia tu....haiingii akili kuwaamini wabunge na kuwapa mamlaka ya kufuatiliz utendaji wa serikali alafu wanapotoa maainisho hayafanyiwi kazi au nyakati zingine zinatiwa kapuni
   
Loading...