Byendangwero
JF-Expert Member
- Oct 24, 2010
- 871
- 56
Hivi karibuni kamati ya bunge ya nishati na madini imeunda kamati ndogo ya kuchunguza kiini cha uchakachuaji wa mafuta ya petroli. Kwa maoni yangu, hatua hiyo haikustahili, kwani kuna vyombo husika ambavyo kamati hiyo ingeliviagiza kufanya utafiti huo; hii ikiwa ni pamoja na EWURA na hata wizara yenyewe. Kama vyombo hivyo vingelishindwa au vingelipuuzia kufanya utafiti huo baada ya maelekezo hayo, basi kamati ingelichukua hatua ya kuwaripoti watendaji wakuu wa vyombo hivyo kwa mamlaka zao za ajira ili wachukuliwe hatua za kinidhamu.