Daniel Mbega
JF-Expert Member
- Mar 20, 2013
- 338
- 180
Wadau,
Nimeambiwa kwamba leo hii kamati mbalimbali za kudumu za Bunge zimeanza vikao vyake kujiandaa na mambo kadha wa kadha, ikiwemo Bajeti ijayo na ya kwanza kabisa katika Serikali ya Awamu ya Tano.
Hata hivyo, tofauti na ilivyozoeleka kwamba vikao hivyo hufanyika katika Ofisi Ndogo ya Bunge jijini Dar, badala yake vikao hivyo vinafanyika kwenye Jengo la LAPF pale Makumbusho.
Najiuliza tu, Bunge hili halihusiki na kauli mbiu ya ‘Hapa Kazi Tu’ inayoendana na kubana matumizi?
Jamani, si Rais Magufuli ameagiza kuwa vikao vya idara za umma vifanyike katika kumbi mbalimbali za umma zilizopo badala ya kwenda kukodisha? Au kwa kuwa Bunge ni mhimili mwingine nalo linaweza kupanga linavyoona inafaa?
Najua LAPF ni shirika la umma, lakini kwa kawaida kumbi zake hukodishwa kwa sababu ni miongoni mwa vitegauchumi vyake katika ‘kuzungusha’ fedha za wanachama wake.
Kulikoni vikao hivyo havikufanyikia kwenye kumbi za Bunge au hata Karimjee kama lengo la serikali ni kubana matumizi?
Labda kama wamepewa bure, lakini LAPF nao watapaswa kuwajibika ni kwa vipi watoe bure kumbi hizo? Kama wamelipia, ni shilingi ngapi na fedha zimetoka katika mfuko gani? Natambua vikao vya Bunge vimesitishwa kurushwa 'live' kwa sababu hiyo hiyo ya kubana matumizi. Vipi vikao hivi kufanyikia kwenye kumbi za kukodi?
Naweza kuwa nimepitwa na wakati, lakini ni mambo yanayonitatiza, lakini kama kuna mtu anayefahamu vizuri zaidi, naomba atujuze na siye wengine – huenda tunakosea kuwalaumu, au tunaweza kuwa sahihi kuhoji uwajibikaji.