Kamati za bunge zaishauri Serikali kutekeleza miradi ya maendeleo kwa ubia na sekta binafsi

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,500
9,279
WAJUMBE wa Kamati za Kudumu za Bunge za Miundombinu, Bajeti na Kamati ya Uwekezaji na Mitaji, wameishauri Serikali kutekeleza kwa vitendo miradi mikubwa na yenye tija kwa Umma kwa kutumia njia ya Ubia kati ya Umma na Sekta binafsi ili kuchochea haraka maendeleo ya nchi.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti Mhe. Mashimba Ndaki amesema kuwa wabunge wameridhishwa na na hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kuhakikisha kuwa mpango wa ubia kati ya Serikali na sekta binafsi unafanikiwa na unachochea maendeleo ya wananchi.

“Kama wabunge tungependa kuona mpango unaingizwa katika mipango ya Serikali ili kuharakisha miradi ya maendeleo na pia tunapongeza hatua zilizochukuliwa na Serikali ikiwemo kumteua Kamishna anayeshughulikia miradi ya ubia kati ya sekta binafsi na ile ya umma, “ Alisisitiza Mboya

Alibainisha kuwa jukumu la Serikali ni kuhakikisha kuwa inaweka mazingira wezeshi kwa wawekezaji wote watakaojitokeza kushirikiana na Serikali katika kutekeleza miradi ya maendeleo hapa nchini.

Mwenyekiti wa Bunge ambaye pia ni Mbunge wa Bariadi Mhe. Endrew Chenge amesema kuwa nchi nyingi Duniani zimefanikiwa kuwaletea wananchi wake maendeleo kupitia utaratibu huo ambapo jambo la muhimu ni kufanywa kwa maandalizi ya kina na kuwepo kwa utashi kutasaidia kufanikiwa kwa miradi husika .

Aliongeza kuwa mwaka huu Serikali imeleta Bungeni Mswada wa Marekebisho ya Sheria ya PPP utakaojadiliwa na wabunge katika Bunge linaloanza Septemba 4 mwaka huu, pamoja na mambno mengine Muswada huo unapendekeza kuanzishwa kwa Kituo cha PPP chini ya Wizara ya Fedha na Mipango, ambacho kitakuwa na jukumu la kuishauri Serikali kuhusu masuala yanayo husu miradi mbalimbali itakayowasilishwa kwa mfumo wa Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi

Akizungumza katika Semina hiyo, Kamishna wa Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi, Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. John Mboya amesema kuwa Dhamira ya Serikali ni kuhakikisha kuwa inaweka mazingira wezeshi katika kutekeleza miradi ya ubia na Sekta binafsi ili kuleta mageuzi katika maisha ya wananchi.

“Lengo la kuwa na miradi ya ubia kati ya Serikali na sekta binafsi ni kutekelezaIilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM), kutekeleza mpango wa maendeleo na hatimaye kutoa huduma bora kwa wananchi,” Alisisitiza Mboya

Akifafanua Mboya amesema kuwa moja ya hatua za maboresho zilizochukuliwa na Serikali ni kuhamisha Kituo cha kusimamia miradi ya ubia katika ya Umma na Sekta binafsi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu kuja Wizara ya Fedha.

Akizungumzia majukumu ya chombo cha kusimamia utekelezaji wa miradi hiyo Dkt. Mboya amesema kuwa chombo hicho kimepewa jukumu la kufanya uchambuzi wa kina kuhusu miradi yenye sifa na kusimamia mchakato wa uteklezaji wa mpango huo kwa kufuata ngazi zote zilizopo hadi utekelezaji wa mradi husika.

Aliongeza kuwa ili kufanikisha mpango huo Serikali inasisistiza uwazi, uwajibikaji na utayari hali itakayo sababisha kufikiwa kwa malengo ya miradi ya ubia kati ya sekta hizo mbili ambapo alitaja baadhi ya miradi itakayotekelezwa ambayo upembuzi yakinifu umekamilika kuwa ni ile ya ujenzi wa Viwanda vya dawa, usambazaji wa gesi majumbani katika Jiji la Dar es Salaam, Mtwara , Lindi na ule wa uendeshaji wa mabasi ya mwendo kasi Jijini Dar es Salaam ambao umeanza na uko katika hatua mbalimbali za uendelezwaji.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Bohari Kuu ya Dawa (MSD) Bw. Laurean Bwanakunu amesema kuwa tayari Bohari hiyo imekamilisha upembuzi yakinifu wa mradi wa ujenzi wa viwanda vya dawa na vifaa tiba vinavyotokana na malighafi zinazozalishwa hapa nchini ikiwemo pamba na kufikia machi mwakani zabuni ya mradi huo itatangazwa ili kuwapata wabia.

Katika kutekeleza mradi huo kiwanda cha kuzalisha maji ya dripu yanayotumika kwa wagonjwa mahosipitalini pia kitajengwa ambapo kwa sasa maji hayo yanaagizwa kutoka nchini Uganda na kwamba hatua hiyo itapunguza gharama za Serikali za kuagiza dawa na vifaa hivyo kutoka nje ya nchi ambapo zaidi ya shilingi trilioni 1.8 hutumika kuagiza bidhaa hizo kila mwaka.

Kwa upande wake. Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC) Mhandisi Kapuulya Musomba amesema kuwa mradi wa kusambaza gesi majumbani katika Jiji la Dar es Salaam, Mtwara na Lindi unaotarajiwa kuhgaribu zaidi ya shilingi bilioni 300, utaleta mageuzi kwa wananchi wa mikoa hiyo ambapo wananchi zaidi ya 120,000 katika Jiji la Dar es Salaam watafikiwa.

Aliongeza kuwa katika mikoa ya Lindi na Mtwara wananchi zaidi ya 5,000 wataunganishiwa gesi majumbani mwao huku viwanda zaidi 30 katika maeneo ya mradi vitaunganishiwa huduma hiyo pamoja na vituo vya kujaza gesi kwenye magari yanayotumia nishati hiyo.

Semina kwa wabunge wa Kamati za Bajeti, Miundombinu na ile ya Uwekezaji Mitaji imefanyika Jijini Dodoma ikiwashirikisha wajumbe wa Kamati hizo ili kuwajengea uwezo wa namna dhana hiyo inavyoweza kuleta maendeleo hapa nchini.

Na Benny Mwaipaja,
WFM, Dodoma
 
Hii miradi hii ya kukurupuka kwa mpigo hii,
Hebu waulizeni wafanyakazi wanaotaraji kustaafu kuna nn kinajiri kwenye pesa zao zilizopo kwenye mifuko ya jamii,
Nawaza tu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
PPP ni jambo zuri kwa.mustakabari wa maendeleo lakini changamoto kwa sasa hatuna wataalamu wenye ujuzi wa kubuni, kufanya upembuzi yakinifu na kufanya analysis ya kina kwa miradi inayokuja kutoka kwa private party.
 
Back
Top Bottom