Kamati za bunge mnatuchefua

mgeni wenu

JF-Expert Member
Jan 2, 2012
3,664
1,730
Wana JF kila siku tuanaskia madudu,ubadhilifua,Uzembe,Rushwa na Ufujaji wa Mali za Uma na kupotea uadilifu kwa Viongozi ambao unai buliwa na KAMATI za Kudumu Za Bunge,

Sasa ni Kipi kinachokataza watu hawa kuchuuliwa Hatua? Kwa Niaba ya Wagosi wenzangu Hapa Tanga sasa tumechoshwa na kuskia UOZO usiochukuliwa hatua kwa kuirekibisha au Kuwachukulia Hatua wahusika(MNATUCHEFUA).

Jamani sasa Basi tumechoka na vikao vyenu visivyo na Hatua za utendaji zaidi ya kutupasha tu Habari,kazi hiyo iacheni Magazeti..
Hata Maamuzi yenu Bungeni sasa hayana Mashiko na ndo Maana Uchaguzi uliopita watu wengi hawakujitokeza kupiga Kura...
 
Sio kamati tuu nimeanza ku question maamuzi ya bunge ..... Richmond kiwira na maremeta yamezikwa kimya kimya... jairo ndo kimyaaa.... ah inachosha.
 
Kwa kweli ni hoja! Naomba niwaulize Wabunge wote wa Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Ikiwa kazi yenu kubwa ni kuisimamia Serikali kama mnavyofanya kupitia kamati zenu za Bunge na Kamati maalumu za Bunge, Lakini mnapotoa maelekezo kwa Serikali, haitekeleze, Je wajibu wenu ni nini?

1. Je mtakuwa kama mbwa anayebweka tu na kumwacha mwizi anaiba na kuifilisi Nyumba? Je mtaendelea kupiga makelele tu kupitia hizo kamati zenu?

2. Ikiwa kama Serikali itakomaa na kila siku inakuja na kuwajibu mambo yenu yanashughurikiwa, mtaendelea kupiga kelele tu?

3. Wananchi tukitoa hoja ya kuwa, Bunge mmeshindwa kazi yenu hivyo hamna budi kujiuzuru mtasemaje?

Ukweli kama mtoa mada alivyosema, mnachefua. Kwanini msipige kura ya kutokuwa na imani na Serikali mkianza na Waziri Mkuu?? Hiyo ndiyo hatua inayotakiwa mfikie, lakini mnaendelea kubweka tu kama Mbwa ambaye anamwacha mwizi anachukua vitu yeye anabweka tu. Shame on you. Tupeni jibu hapa Jamvini.
 
Umenena mkuu lakini wanaweza kupiga kura ya kutokuwa na imani na serekali hawa?
 
Wabunge wapo kimasilahi zaidi, Wanaanzisha Hoja, inajadiliwa hadi wananchi wadanganyika tunasema hili ndilo Buge. Utashangaa itakapofia na kaburi lake halijulikani.

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Wana JF kila siku tuanaskia madudu,ubadhilifua,Uzembe,Rushwa na Ufujaji wa Mali za Uma na kupotea uadilifu kwa Viongozi ambao unai buliwa na KAMATI za Kudumu Za Bunge,
Sasa ni Kipi kinachokataza watu hawa kuchuuliwa Hatua? Kwa Niaba ya Wagosi wenzangu Hapa Tanga sasa tumechoshwa na kuskia UOZO usiochukuliwa hatua kwa kuirekibisha au Kuwachukulia Hatua wahusika(MNATUCHEFUA)
Jamani sasa Basi tumechoka na vikao vyenu visivyo na Hatua za utendaji zaidi ya kutupasha tu Habari,kazi hiyo iacheni Magazeti..
Hata Maamuzi yenu Bungeni sasa hayana Mashiko na ndo Maana Uchaguzi uliopita watu wengi hawakujitokeza kupiga Kura...

one third ya wabunge wote ingekuwa ni upinzani serikali ingeliogopa bunge. bunge la sasa wapinzani hata one third hawajafika thats wy serikali haitekelezi maamuzi ya bunge yaloelekezwa kwao na bunge. in short magamba ni mengi bungeni ndo maana serikali inadharau maamuzi ya bunge.
 
Kwa unafiki na ubinafsi wa waTZ hakuna wanachokuwa serious zaidi ya kutetea maslahi yao binafsi
 
mimi huyu manufacturing of teachers aka Baba Mwanaasha ndo ananikera zaidi......

images

Viongozi wengi wanaotuhumiwa wapo chini ya jurisdiction ya presidency, sasa unategemea Kamati ikishaona madudu, report ikaenda ofisi ya speaker na wizara husika, nani wa ku-act?
 
Bunge letu liko kwa masilahi ya chama tawala zaidi na si kwa ajili ya watanzania!!!, Kumbuka spika ni mjumbe wa CC ya chama tawala!!!!
 
Kwa kweli ni hoja! Naomba niwaulize Wabunge wote wa Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Ikiwa kazi yenu kubwa ni kuisimamia Serikali kama mnavyofanya kupitia kamati zenu za Bunge na Kamati maalumu za Bunge, Lakini mnapotoa maelekezo kwa Serikali, haitekeleze, Je wajibu wenu ni nini?

1. Je mtakuwa kama mbwa anayebweka tu na kumwacha mwizi anaiba na kuifilisi Nyumba? Je mtaendelea kupiga makelele tu kupitia hizo kamati zenu?

2. Ikiwa kama Serikali itakomaa na kila siku inakuja na kuwajibu mambo yenu yanashughurikiwa, mtaendelea kupiga kelele tu?

3. Wananchi tukitoa hoja ya kuwa, Bunge mmeshindwa kazi yenu hivyo hamna budi kujiuzuru mtasemaje?

Ukweli kama mtoa mada alivyosema, mnachefua. Kwanini msipige kura ya kutokuwa na imani na Serikali mkianza na Waziri Mkuu?? Hiyo ndiyo hatua inayotakiwa mfikie, lakini mnaendelea kubweka tu kama Mbwa ambaye anamwacha mwizi anachukua vitu yeye anabweka tu. Shame on you. Tupeni jibu hapa Jamvini.

Well said,
Bunge sasa limekua kama ZE KOMEDY,wabunge wanatemeana mate tu bungeni then nothing is implemented
 
one third ya wabunge wote ingekuwa ni upinzani serikali ingeliogopa bunge. bunge la sasa wapinzani hata one third hawajafika thats wy serikali haitekelezi maamuzi ya bunge yaloelekezwa kwao na bunge. in short magamba ni mengi bungeni ndo maana serikali inadharau maamuzi ya bunge.
Bunge makini lenye wabunge makini huwa linaangalia hoja badala ya ushabiki wa kichama. Hili letu limekaa kivyama zaidi badala ya hoja za msingi za kitaifa . Kwangu mimi hili si bunge makini. Bunge gani makini mwishoni mwa mwaka jana limepitisha muswada kwa mbwembwe na kejeli lakini baada ya miezi miwili sheria inarudi kwa mabadiliko na Bunge hilohilo linapitisha tena. Huwa hawaoni hoja bali ushabiki ambao ni maumivu kwa commonmwananchi.
 
Tulisikia TCRA watu walijisomesha kwa mabilioni ya pesa, tukasikia TBS, tukasikia kwa waziri mkuu, tukasikia nishati na madini na tunaendelea kusikia kamati za bunge zikipiga kelele za wizi lakini sijasikia watu wanaofikishwa kwenye vyombo vya sheria. je tumekuwa taifa la kupiga kelele tu bila kufanya kitu? kama ndio hivyo basi hakuna sababu ya kuwa na kamati za bunge wala bunge lenyewe kama sheria kwa wakosaji hazichukui mkondo wake
 
Back
Top Bottom