Kamati yapokea na kujadili taarifa ya Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kuhusu muundo na majukumu ya Wizara hiyo

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
707
461
Kamati ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo imepokea na kujadili taarifa ya Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kuhusu muundo na majukumu ya Wizara hiyo kwa mujibu wa ratiba na vikao vya Kamati za Bunge ambavyo vimeanza Machi 10, 2023.

20230313_093912.jpg

========

Kamati ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo imepokea na kujadili taarifa ya Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kuhusu muundo na majukumu ya Wizara hiyo kwa mujibu wa ratiba na vikao vya Kamati za Bunge ambavyo vimeanza Machi 10, 2023.

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo Mhe. Prof. Kitila Mkumbo amesema kamati hiyo inatambua kuwa Utamaduni, Sanaa na Michezo ni sekta muhimu kwa maendeleo ya Taifa.

Kamati hiyo imekutana Machi 12, 2023 jijijini Dodoma kujadili majukumu na muundo wa Wizara hiyo muhimu sana kwa maendeleo ya Taifa na Watanzania kwa ujumla.

“Utamaduni ni kila kitu, sekta za wizara hii ni muhimu sana kwa maendeleo ya Taifa letu, ni wakati mwafaka sasa tunapozungumza kuporomoka kwa maadili, lazima tujiulize yameporomoka kutoka wapi, yapi ni maadili ya taifa. Ni wakati sasa kuyapambanua haya kwa kuwa utamaduni ni kila kitu, tunaamini nini kuhusu kilimo, tunaamini nini kuhusu viwanda, haya yote ni utamaduni” amesema Prof. Mkumbo.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Hamis Mwinjuma amewahakikishia Wajumbe wa Kamati hiyo ya Bunge kuwa Wizara itaendelea kushirikiana na kamati hiyo kwa kufanyakazi kwa weledi na kwa kasi ili kuwahudumia Watanzania na wadau wa sekta za wizara hiyo.

Wakichangia taarifa hiyo wajumbe wa kamati hiyo wamesema Watanzania wanapenda michezo ikiwemo mpira wa miguu, wawekezaji wanapaswa kuwekeza kwenye michezo nchini ili kukuza ligi zetu kuanzia ngazi ya chini hadi ligi kuu tofauti na hali ilivyo sasa ambapo Ligi Kuu pekee nchini ndiyo yenye wadhamini na kusisitiza kujifunza kutoka nchi nyingine wananafanyaje katika eneo hilo.

Aidha, wajumbe hao wa Kamati ya Elimu, Utamaduni na Michezo wameipongeza Wizara kwa kazi nzuri inayofanywa na kuwahimiza Viongozi wapya walioteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. SAMIA SULUH HASSAN kusimamia sekta za Wizara hiyo ili kufanyakazi kwa tija na kuwahudumia Watanzania.

Timu ya Wizara imeongozwa na Naibu Waziri Mhe. Hamis Mwinjuma, Naibu Katibu Mkuu Bw. Nicholas Mkapa, Wakurugenzi pamoja na Wakuu wa Vitengo.
 
Back
Top Bottom