Kamati ya Zitto yaishukia PPF Juu ya Malipo ya Mamilioni ; Yaagiza kusitishwa malipo mapya!

Status
Not open for further replies.
Tutakuelewesha.

Gratuity ni mafao ya mwisho wa mkataba kwa wafanyakazi walio katika ajira za mkataba wa muda maalumu. Wakurugenzi wa PPF wana mikataba ya miaka mitatu mitatu. Hii ni haki yao

Group Endowment: Ni mafao ya mwisho wa ajira kwa wafanyakazi wa kudumu wanapofikia umri wa kustaafu. Kwa PPF ipo wazi kuwa ni miaka 55 kama utastaafu kwa hiari au 60 kwa lazima. Kwa PPF hutolewa pia kwa wategemezi kama mfanyakazi amestaafu kwa njia ya kifo.

PPF wamekosea wapi nitashirikiana nanyi pamoja na Kaka yetu mtetezi wa Taifa la Tanzania Mzee Mwanakijiji.

Issue ni kuwa serikali kupitia Bodi ya Wadhamini iliamua mwaka 2002 kuwa menejimenti ya PPF wawe kwenye mikataba. Wakati uamuzi huu unafanywa, menejimenti ya PPF walikuwa wafanyakazi wa kudumu na wako kwenye Group Endowment Scheme (GES). Hivyo walivyoingia kwenye ajira ya mikataba wakaendelea kupata GES na gratuity kila mkataba ukiisha.

Sidhani kama kuna sheria yoyote iliyo wazi inayosema kuwa GES lazima awe ni mwajiriwa wa kudumu na wale wa mikataba hawaruhusiwi. Pia hakuna usimamizi/waraka/sera wa hizi GES unaofanywa na Hazina hivyo kutokea huu utata.

gratuity na group endowment
sijavielewa hivi vitu nin nini?
 
Issue ni kuwa serikali kupitia Bodi ya Wadhamini iliamua mwaka 2002 kuwa menejimenti ya PPF wawe kwenye mikataba. Wakati uamuzi huu unafanywa, menejimenti ya PPF walikuwa wafanyakazi wa kudumu na wako kwenye Group Endowment Scheme (GES). Hivyo walivyoingia kwenye ajira ya mikataba wakaendelea kupata GES na gratuity kila mkataba ukiisha.

Sidhani kama kuna sheria yoyote iliyo wazi inayosema kuwa GES lazima awe ni mwajiriwa wa kudumu na wale wa mikataba hawaruhusiwi.

Kwa PPF iko wazi ila ni matumizi ya nguvu za madaraka. Nyaraka zinazokataza walio katika mikataba wasipewe group endowment zipo. PPF imekuwa na wafanyakazi wa mikataba wengi. Kwa nini wakurugenzi peke yao? wengine wanaambiwa mikataba yenu haisemi mpewe GES. Mikataba ya wakurugenzi iliandaliwa na wakurugenzi hawa hawa. Draft contracts walizokuwa wanapitishiana kuulizana kama ipo powa ninay

Pia hakuna usimamizi/waraka/sera wa hizi GES unaofanywa na Hazina hivyo kutokea huu utata.

Habari ya kuisifia PPF imetoka Jamboleo. Ni uongo. Its a spin.

Kamati imewakaripia PPF na tumemwagiza CAG achunguze malipo yakiyokwisha fanywa, tumesimamisha malipo ya sasa na tumepiga marufuku double payments ie gratuity na endowment scheme. The citizen wameandika sawa na hata Dailynews wameandika sawa. Maslahi ya JamboLeo ni nini kupotosha habari ya kamati?

Mfumo wa ajira za mikataba kwa mashirika ya umma ni mwanya wa senior staff kujilipa mabilioni ya fedha za Mashirika. CAG ameelekezwa na kamati kukagua mfumo huu kwa mashirika yote ya umma kwa kuanzia na mifuko ya pensheni kisha mashirika makubwa kama TANAPA, TCRA, EWURA nk. Mwaka jana kamati iliagiza TPA kuachana na mfumo huu na vile vile Katibu Mkuu utumishi alitoa waraka kuzuia mfumo wa aina hii.

Endowment scheme ni kwa wafanyakazi wote wa shirika na inakubalika. Gratuity ni ufujaji wa mali na ni marufuku kwa mtu mmoja kufaidika na gratuity na wakati huo huo endowment scheme.

Nitamletea mod hansard ya kikao cha kamati ili wasomaji wa JF waone ukweli wa mjadala na habari ya jambo leo ambayo ni spin ipuuzwe!

Zitto,

Nilipoteza imani nawe kabisa juu ya utetezi wetu kupitia kwako. Sidhani kama baada ya kupoteza imani niewahi sema zuri juu yako hata pale uliposema zuri, sikusifia, nilinyamaza.

Namshukuru Mungu kuwa sasa umerudi Kundini na kuwa Zitto tuliyemfahamu.

Hili suala la GES pale PPF anayelifahamu vizuri ni yule Mhasibu Mkuu aliye wakatalia kuwalipa 2008.

1. Kwa kuwa Kamati yako imekubali kuwa kuna tatizo, je huyu Mhasibu aliyeathitirika kwa kupigania ukweli Kamati inamsaidiaje?
2. Chief Internal Auditor ambaye alitoa waraka mwaka 2002 kuwa walio katika mikataba hawastahili GES (waraka upo MH.) hakumsaidia Mhasibu mkuu kukataza uizi huu kwa kuwa naye alikuwa anapata. Baada ya kupokea tu, akatoa waraka mwingine kwenda kwa mkurugenzi wa utawala luwa atengeneze policy ya kuruhusu GES, akasema malipo haya ya 200M @ hayana supporting documents (copy ipo) ni PM email address yako nikuletee.
3. Katika uchunguzi huu kama wataitumia menejimenti hii, utaona majibu. Wana pesa kama mchezo, hili unalijua. Mhasibu wetu mkuu walimhamishia Mbeya ndiye pekee anayeweza kuelezea vizuri kwa CAG na hata kwenu Kamati. Ila wafanyakazi tunahofia usalama wake. Wasije mchomoa nafsi ili kuficha makosa yao
 
Issue ni kuwa serikali kupitia Bodi ya Wadhamini iliamua mwaka 2002 kuwa menejimenti ya PPF wawe kwenye mikataba. Wakati uamuzi huu unafanywa, menejimenti ya PPF walikuwa wafanyakazi wa kudumu na wako kwenye Group Endowment Scheme (GES). Hivyo walivyoingia kwenye ajira ya mikataba wakaendelea kupata GES na gratuity kila mkataba ukiisha.

Sidhani kama kuna sheria yoyote iliyo wazi inayosema kuwa GES lazima awe ni mwajiriwa wa kudumu na wale wa mikataba hawaruhusiwi. Pia hakuna usimamizi/waraka/sera wa hizi GES unaofanywa na Hazina hivyo kutokea huu utata.

Nimesema hansard nitaweka hapa. Kuhusu tuzo ya utawala bora tuliwapongeza. Kuhusu hati safi tuliwapongeza. Tumewakaripia kuhusu malipo na TUMEYAZUIA. Kupata gratuity na group endowment is against the public service act. Double payment hairuhusiwi. CAG ameagizwa kukagua malipo ya nyuma ya PPF na kama yalikwenda kinyume na sheria waliolipwa lazima warejeshe. Nimelisema wazi hilo jana.
Tuzo ya ubora ya EAC is a small matter here and we didn't even discuss it. Hati safi kila shirika sasa linapata kwa kuwa CAG anakuwa hayaoni haya ambayo wananchi wanayalalamikia.
Hii sio kwa PPF tu, tumemwambia aende mashirika yote. Tayari kamati imepiga stop kwa TPA mwaka jana na wamefuta.
You get pension, its a right. Endowment is an incentive, powa. Gratuity without endowment is ok. Gratuity plus endowment is wrong. Ni mfumo wa wizi kwa watu wachache. Tumeupiga marufuku. Kwa mashirika yote ya umma.
Pia endowment schemes za mashirika ziwe managed na fund managers na sio shirika lenyewe. Those were major decisions.

Kuhusu jamboleo nimemjulisha katibu wa Bunge awaite na kuwahoji wajieleze.

Sidhani kama kuna sheria yoyote iliyo wazi inayosema kuwa GES lazima awe ni mwajiriwa wa kudumu na wale wa mikataba hawaruhusiwi.

Zitto,

Utaratibu huu ulipoanzishwa ulilenga wafanyakazi wa kudumu tu. Uliwekwa maalumu wakati wa kustaafu kwa umri au kifo. Bwana Mattaka alipobadilishiwa ajira na kuwa ya mkataba, alilipwa GES na kufanya kazi kwa mkataba. Malipo yake ya mkataba hakulipwa GES kama wanavyofanya hawa.

Nyaraka za PPF zilzo kuwepo hadi May 2008 zinasema kuwa ni wafanyakazi wa kudumu tu ndio wanaostahili. Wafanya kazi wa mikataba ambao walikuwepo PPF na walilipwa GRATUITY pekee ni kama Bw. Kilima (Ag. Director of Investiment) Mbala na Mwageni. Je Mh. Zitto kwa nini Ibague?

Tumewakaripia kuhusu malipo na TUMEYAZUIA.

Hapa hongera.

Kupata gratuity na group endowment is against the public service act. Double payment hairuhusiwi.

It was also against PPF GES policies and its Trust DEED, PPF financial Regulations, PPF staff and Admin. PPF Budget and good governance

CAG ameagizwa kukagua malipo ya nyuma ya PPF na kama yalikwenda kinyume na sheria waliolipwa lazima warejeshe. Nimelisema wazi hilo jana.

Ili kupata majibu mazuri naomba Mh. Umshauri apitie nyaraka zifuatazo:

1. GES trust deed, original document iko NIC
2. Chief internal Auditor report ya Sept 2002
3. PPF budgets 2006 to 2009
4. PPF annual reports (kipengele cha GES) 2006 to 2009
5. Mabishano ya Mhasibu Mkuu na wakurugenzi juu ya kutokuwa halali

Pia ahoji wafanyakazi akiwemo aliyekuwa mhasibu Mkuu 2006 to 2008

You get pension, its a right. Endowment is an incentive, powa.
Gratuity without endowment is ok. Gratuity plus endowment is wrong. Ni mfumo wa wizi kwa watu wachache. Tumeupiga marufuku.

Maneno yako haya haya yalimponza Mhasibu Mkuu wetu Bw. Mbwilo. Yeye aliwaambia Gratuity plus endowment is wrong. GRATUITY for contract staffs, ENDOWMENT for permanent staff and PENSIONS for all. Erio akataka kumfukuza kazi. Kamati ya Bunge, Waziri wa fedha na Katibu Mkuu kiongozi wamsaidie apate haki zake kitaaluma.
 
Mambo mengine ni machafu kiasi kwamba huwerzi hata kuelewa kama nchi hii kuna Rais aliye timamu. Huyu Erio ni mteule wa Rais. Nakumbuka vizuri sana alipoteuliwa kuna vichwa vilileta ushabiki eti mdogo kwa umri kumbe bure! bure kabisa!

Sifa kubwa ya kupata nafasi kama hiyo ni mpwa wa Mkapa!

Huyu mtu alivyo hawezi hata siku moja kuleta mafanikio ya kazi.

Jamani Elimu yake ikoje? au naye amepewa vyeti kwa sababu tu ni ndugu wa Mkapa. Nahisi pia makuzi yake ni zero.
 
Mi nafikiri ni vizuri tukawa na independent remuneration committe ambayo itakuwa inadevelop remuneration policy kwa kila shirika ili kuweza kucontrol haya matatizo maana km yasipodhibitiwa mapema yanaweza kuleta Scandal ya Enron, 2002 ya marekani ambapo watendajili wakuu walikuwa wanajilipa malipo makubwa yasilingana nautendaji wao.
 
Mimi ningependa kujua kama hawa viongozi wa PPF ni watanzania? Na kama jibu ni ndiyo, basi ningependa kujua Tanzania imewakosea nini?
 
Nadhani bado hujaelewa kinachogombewa ni nini? Hatukusema kuwa GES ni corruption! Tulichoonesha na ambacho tutaonesha mbeleni ni kuwa wakurugenzi wa PPF walitumia ambiguity ya sheria/ taratibu zao wenyewe kujifanya wanastahili malipo ya GES wakati tayari walikuwa wanalipwa gratuity ya 25% ya mishahara yao. Walichokifanya ni kukubaliana kuwa "wao wanastahili" mwisho wa mkataba.

Tatizo ni kuwa GES ni malipo kwa mtu aliyemaliza ajira siyo mkataba. Sasa wao walipolipwa 2008 ingekuwa wameondoka PPF ingeonekana hata labda kuna kukubaliana lakini ulikuwa ni "mwisho wa mkataba" mmoja na wakaanza mkataba mwingine. Walitumia nafasi zao kujistahilisha na baadaye kuhalalisha malipo ambayo vinginevyo wasingeyastahili; huu ndio ufisadi.

Lakini vile vile, kanuni ya GES ni ipi? Kwa hiyo ukiondoa hilo kuna suala la kiwango cha malipo; ni mfanyakazi gani wa PPF ambaye ametumikia shirika hilo na siyo Mkurugenzi ambaye atapata GES ya milioni 220!?

To tell you the truth; natofautiana na Zitto kwenye hili: Watendaji hawa walistahili kulipwa Gratuity kwa mujibu wa mikataba yao na siyo GES. Kwa vile wao walikuwa ni waajiriwa wa mkataba basi walikuwa waongozwe na mikataba hiyo. GES ni kwa ajili ya watumishi wa kudumu wa PPF. HIvyo, Wakurugenzi hawa wa mikataba hawakustahili kulipwa kutoka GES.

Hongera sana Mwanakijiji,

Ukweli kuhusu hii endowment scheme kwa wafanyakazi ambao wako kimkataba zaidi wahana stahili ya kupewa endowment fund zaidi ya Gratuity kwani iwapo sheria inawaharalisha kwao kuchukua hizo pesa basi wazirejesha. Huo ndiyo ulikuwa ugomvi uliokuwepo baina ya Chief Accountant (Mbwilo) ambaye walimtoa baada ya kukataa kuwa hawajamaa hawastahili kulipwa hizo pesa kwakuwa wao wako kwenye mikataba with a simple logic na ku avoid double payments mfano gratuity na endowment. CAG alifanyie kazi kwani haya mapungufu yalekebishwe na wahusika walikiuka sheria ya malipo na penalty yake ni kuwa wawe dismissed kwenye employment.
 
RASJAH, Mbona ulipotea? Umechelewa, tayari Erio kawapa Mmari (DF) na Hossea Kashimba(CIA) mkataba mpya baada ya kulamba endowment nyingine.

Erio hana mchezo ni kuzilamba pesa za PPF

Mwanakijiji, fight Baba! Mungu atakulipa.

Back
Top Bottom