Kamati ya Zitto yaishukia PPF Juu ya Malipo ya Mamilioni ; Yaagiza kusitishwa malipo mapya! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kamati ya Zitto yaishukia PPF Juu ya Malipo ya Mamilioni ; Yaagiza kusitishwa malipo mapya!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by The Informer, Apr 1, 2011.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. T

  The Informer Senior Member

  #1
  Apr 1, 2011
  Joined: Jun 14, 2010
  Messages: 119
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  POAC yaipongeza PPF kwa clean audit opinion

  Kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma (POAC), chini ya uenyekiti wa Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, imetoa pongezi kwa Mfuko wa Pensheni nchini (PPF) kwa kuwa na hati safi ya ukaguzi (clean audit opinion) iliyotolewa na ofisi ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

  Zitto pia amesema kuwa kwa mujibu wa taarifa ya Mamlaka mpya ya Usimamizi wa Mifuko ya Pensheni (SSRA), PPF ni mfuko wa pensheni unaoongoza Tanzania kwa kuwa endelevu na wenye usimamizi mzuri.

  "Tunawapongeza kwa clean audit opinion ... PPF ni mfuko unaoweza kukaa muda mrefu kuliko yote. Tunawapongeza sana kwa hilo," alisema Zitto kwenye kikao cha POAC na menejimenti ya PPF kilichofanyika Dar es Salaam tarehe 31 Machi, 2011.

  Zitto pia ameipongeza PPF kwa kupewa tuzo ya kuwa mfano bora miongoni mwa mashirika ya hifadhi ya jamii katika nchi za Afrika Mashariki na Kati katika uimarishaji na uendelezaji wa misingi ya utawala bora.

  Tuzo hiyo ya utawala bora ilitolewa kwa PPF hivi karibubi na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Burundi Thérence Sinunguruza, wakati wa mkutano wa tatu wa Shirikisho la Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya Afrika Mashariki na Kati (ECASSA) uliofanyika jijini Bujumbura, Burundi.

  Kamati ya POAC pia imeipongeza PPF kwa Group Endowment Scheme yake ambayo ni mfumo wa kuwapa motisha wafanyakazi wote wa PPF kuanzia kada za chini, kati, mpaka menejimenti.

  "Endowment scheme is a system of retaining wafanyakazi kwa muda mrefu. Ni mfumo ambao uko kwenye mashirika mengi na hata tumeishauri TANAPA ianzishe scheme hiyo. PPF inaweza kuchangamkia biashara hiyo ya kuendesha Endowment Scheme ya TANAPA," alisema Zitto.

  Kutokana na malipo hayo ya Group Endowment Scheme, baadhi ya wafanyakazi wa PPF wamelipwa kati ya shilingi milioni 150 mpaka 220 milioni/- pale wanapoacha kazi.

  Baadhi ya wajumbe wa POAC walisema kuwa kumekuwa na malalamiko kuwa menejimenti ya PPF wanalipwa Endowment Scheme, Gratuity na pensheni wakati wafanyakazi wengine wa PPF wanalipwa Endowment Scheme na pensheni tu.

  Hata hivyo Mkurugenzi Mkuu wa PPF, William Eriyo, alieleza kuwa Bodi ya Wadhamini ya PPF iliamua mwaka 2002 kuwa menejimenti ya PPF wote waajiriwe kwa mikataba, hivyo kwa utaratibu wa kawaida kwenye shirika lolote lile, wafanyakazi waliokuwa kwenye mikataba hulipwa gratuity wanapomaliza mikataba yao.

  Eriyo akasema kuwa malipo ya gratuity yanaweza kuepukwa kwa kurudisha utaratibu wa awali wa kuwaajiri menejimenti ya PPF kama waajiriwa wa kudumu (permanent and pensionable employment).

  Aidha, Eriyo, alisema kuwa PPF ina wastaafu karibu ya 20,000 ambao ni wengi kuliko wastaafu wa mifuko yote ya pensheni mingine kwa ujumla wao.

  Alisema kuwa thamani ya mfuko imeongezeka mpaka kufikia zaidi ya shilingi bilioni 624 ilipofika mwaka 2009 na mfuko unaendelea kupata faida.

  "Sisi tuko 100 percent funded. Tunaweza kulipa pensheni bila ya kuuza rasilimali za PPF au kukopa. Tathmini zinaonesha kuwa kwa rasilimali zake za sasa, PPF inaweza kufika mpaka mwaka 2056," alisema Eriyo.


  Baada ya kufanya majadiliano, kamati ya POAC ilitoa maagizo yafuatayo makuu kwa PPF:


  • CAG akishirikiana na Treasury Registrar wafanye review ya malipo ya Group Endowment scheme na gratuity kwenye mifuko yote ya pensheni nchini halafu wahamie kwenye mashirika mengine makubwa kama TANAPA, TPA, nk.


  • PPF itoe restrictive tender ili mmoja wa mifuko ya pensheni iliyopo ipewe jukumu la kuendesha Group Endowment scheme. PPF nayo ikashauriwa kuchangamkia tenda ya kuendesha Group Endowment scheme ya TANAPA.


  • PPF imtoe Mbunge kuwa mjumbe wa Bodi wa Bodi yake wa Wadhamini na imtaarifu Waziri wa Fedha kuwa kuna nafasi moja wazi ya mjumbe. Sheria mpya inakataza wabunge kuwa wajumbe wa mifuko ya pensheni.
   
 2. Zitto

  Zitto MP Kigoma Urban

  #2
  Apr 1, 2011
  Joined: Mar 2, 2007
  Messages: 1,197
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  Habari ya kuisifia PPF imetoka Jamboleo. Ni uongo. Its a spin.

  Kamati imewakaripia PPF na tumemwagiza CAG achunguze malipo yakiyokwisha fanywa, tumesimamisha malipo ya sasa na tumepiga marufuku double payments ie gratuity na endowment scheme. The citizen wameandika sawa na hata Dailynews wameandika sawa. Maslahi ya JamboLeo ni nini kupotosha habari ya kamati?

  Mfumo wa ajira za mikataba kwa mashirika ya umma ni mwanya wa senior staff kujilipa mabilioni ya fedha za Mashirika. CAG ameelekezwa na kamati kukagua mfumo huu kwa mashirika yote ya umma kwa kuanzia na mifuko ya pensheni kisha mashirika makubwa kama TANAPA, TCRA, EWURA nk. Mwaka jana kamati iliagiza TPA kuachana na mfumo huu na vile vile Katibu Mkuu utumishi alitoa waraka kuzuia mfumo wa aina hii.

  Endowment scheme ni kwa wafanyakazi wote wa shirika na inakubalika. Gratuity ni ufujaji wa mali na ni marufuku kwa mtu mmoja kufaidika na gratuity na wakati huo huo endowment scheme.

  Nitamletea mod hansard ya kikao cha kamati ili wasomaji wa JF waone ukweli wa mjadala na habari ya jambo leo ambayo ni spin ipuuzwe!
   
 3. fangfangjt

  fangfangjt JF-Expert Member

  #3
  Apr 1, 2011
  Joined: Apr 25, 2008
  Messages: 571
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 33
  safi sana, hii ndio WEB 2.0, huwezi ficha kitu!

  hilo JamboLeo mtalichukulia hatua gani?
   
 4. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #4
  Apr 1, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Thank you very much Zitto kwa kuwahi ku-clarify hili... Mimi binafsi nimesikia uliyosema wewe na sielewi kwanini magazeti kama jambo leo yasifungiwe na pia inaonyesha wazi kwamba jamboleo wako corrupt!!!

  Rai yangu kwenu kamati ya bunge, msiishie kwenye recommendations, please tighten the screw at reach to completion of what you have recommended

  Tutawaheshimu na kuwaamini.... we want results and not findings and recommendations
   
 5. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #5
  Apr 1, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Swali zuri sana.... imefikia wakati magazeti yaache utani na mambo ya maslahi kwa taifa.... nadhani bunge lina nguvu sana na adhabu kwa jambo leo italeta heshima, walifungie gazeti, mwandishi, mhariri na yeyote aliehusika... kwenye professionalism, misconducts may lead to deletion or suspension ya kupractice

  waliohusika wafungiwe kabisa kufanya hiyo kazi
   
 6. L

  LAT JF-Expert Member

  #6
  Apr 1, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  indeed a vital committee .... magnificent performance .... kindly please pull up your socks
   
 7. W

  Warofo Member

  #7
  Apr 1, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 75
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mh. Zitto hebu tuwekee hiyo hansard tuone kama hukuwapongeza PPF kwa hati safi ya ukaguzi na kupata tuzo ya utawala bora ili tuwashambulie waandishi wa habari kwa kuwa spin masters.

  Kuhusu suala la menejimenti kulipwa Group Endowment Scheme, Gratuity na pensheni, nadhani ni suala la kisera. Kwa ufahamu wangu, mashirika mengi ya umma yana mfumo huu. Ukaguzi wa CAG utaibua mambo mengi sana. Hata shirika dogo kama Tanzania Standard Newspapers (TSN) menejimenti wanalipwa gratuity kila mara mkataba wao unapoisha na waki renew ukiisha wanalipwa tena gratuity and so on. Kama menejimenti wakiwa kwenye mkataba basi suala la gratuity halikwepeki.

  Kuna masuala yafuatayo hapa:

  1. Pensheni ni haki ya kila mfanyakazi, wakiwemo permanent and pensionable na wale wa mikataba
  2. Gratuity ni malipo ambayo hayakwepeki kwa senior management staff walio kwenye mikataba

  Suala ni kuwa, Je wafanyakazi walio kwenye mikataba nao wanastahili kuwekwa kwenye Group Endowment Scheme au hiyo iwe kwa wafanyakazi ambao ni permanent and pensionable peke yao?

  Ieleweke kuwa kabla ya uamuzi wa Bodi ya Wadhamini ya PPF mwaka 2002 kuwa menejimenti waajiriwe kwa mikataba, menejimenti hawa walikuwa kwenye permanent and pensionable employment na hivyo walikuwa kwenye Group endowment scheme, hivyo walivyoingia kwenye contract employment ilitakiwa ufanywe uamuzi wa kuwalipa pesa zao la Group endowment scheme ili wabaki na gratuity na pensheni zao.

  CAG, Katibu Mkuu Kuingozi, au Wizara ya Fedha wanatakiwa watoe waraka kuhusu nani anastahili kuweko kwenye Group endowment scheme au wafute contract employment kwa wafanyakazi wa menejimenti ili kuondoa gratuity.
   
 8. D

  Domo Zege JF-Expert Member

  #8
  Apr 1, 2011
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 687
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Asante Mr.Zitto kwa taarifa hii,

  Ombi langu ni hatua gani mtachukua kama kamati kuhusu gazeti hili sababu lipo sokoni tayali na madhara yake ni makubwa

  Je kama kamati kwanini msikanushe habari hii kupitia media ili kuepusha upotoshwaji huu

  Haya ndio magazeti ya kusoma kama barua kama alivyosema spika
   
 9. Zitto

  Zitto MP Kigoma Urban

  #9
  Apr 1, 2011
  Joined: Mar 2, 2007
  Messages: 1,197
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  Nimesema hansard nitaweka hapa. Kuhusu tuzo ya utawala bora tuliwapongeza. Kuhusu hati safi tuliwapongeza. Tumewakaripia kuhusu malipo na TUMEYAZUIA. Kupata gratuity na group endowment is against the public service act. Double payment hairuhusiwi. CAG ameagizwa kukagua malipo ya nyuma ya PPF na kama yalikwenda kinyume na sheria waliolipwa lazima warejeshe. Nimelisema wazi hilo jana.
  Tuzo ya ubora ya EAC is a small matter here and we didn't even discuss it. Hati safi kila shirika sasa linapata kwa kuwa CAG anakuwa hayaoni haya ambayo wananchi wanayalalamikia.
  Hii sio kwa PPF tu, tumemwambia aende mashirika yote. Tayari kamati imepiga stop kwa TPA mwaka jana na wamefuta.
  You get pension, its a right. Endowment is an incentive, powa. Gratuity without endowment is ok. Gratuity plus endowment is wrong. Ni mfumo wa wizi kwa watu wachache. Tumeupiga marufuku. Kwa mashirika yote ya umma.
  Pia endowment schemes za mashirika ziwe managed na fund managers na sio shirika lenyewe. Those were major decisions.

  Kuhusu jamboleo nimemjulisha katibu wa Bunge awaite na kuwahoji wajieleze.
   
 10. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #10
  Apr 1, 2011
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Mh. Mzitto

  Thanks kwa maelezo mazuri nimekugongea thanks

  Note: Rudisha imani yako kwa watanzania wanzako, pigania tanzania yako, usipende sifa na Kuwa mpiganaji wa ukweli
   
 11. fredmlay

  fredmlay JF-Expert Member

  #11
  Apr 1, 2011
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,855
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Safi sana, kwahilo nakupongeza wewe na kamati yako, sasa sijui hawa jamaa wa gazeti la Jambo leo wanatafuta nini kwa kupotosha ukweli...???
   
 12. W

  Warofo Member

  #12
  Apr 1, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 75
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kwenye post zake humu JF, Mzee Mwanakijiji ameweka invoice za malipo ya Group Endowment Scheme ambayo menejimenti ya PPF wamelipwa mamilioni ya pesa akasema hii ni corruption kumbe ni utaratibu unaoruhusiwa na hata kamati ya POAC imeshauri TANAPA nao wauanzishe.

  Kinachokatazwa ni double payment ya Group Endowment Scheme na gratuity kwa mtu mmoja. Lakini ieleweke kuwa malipo ya gratuity yanatokana na uamuzi wa serikali yenyewe kusema menejimenti ya PPF wawe kwenye ajira ya mikataba na si ajira ya kudumu.

  Hapa suluhisho ni dogo tu. Serikali itangaze kuwa menejimenti ya PPF na mashirika mengine yote ya umma iwe kwenye ajira ya kudumu (permanent and pensionable employment) ili kuondokana na malipo ya gratuity.

  Kuna mtazamo kuwa menejimenti inapokuwa mkataba wa muda wanakuwa hawana uzalendo sana na hawazingatii maslahi ya kudumu ya shirika kwani wanajua kuwa ajira yao ni ya mkataba wa muda mfupi.

  Menejimenti wanapokuwa kwenye mkataba wa kudumu wanakuwa motisha zaidi na kuwa na ownership zaidi na shirika wanaloliongoza.
   
 13. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #13
  Apr 1, 2011
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 719
  Trophy Points: 280
  Endowment is an incentive, powa. Gratuity without endowment is ok. Gratuity plus endowment is wrong.  piga marufuku yote...huu wote ni wizi tu......wanabadilisha maneno tu la nyuma linaenda mbele la ,bele linarudi nyuma ili hali kuhalalisha malipo hewa... maneno kama haya Gratuity without endowment is ok. Gratuity plus endowment is wrong.
   
 14. Zitto

  Zitto MP Kigoma Urban

  #14
  Apr 1, 2011
  Joined: Mar 2, 2007
  Messages: 1,197
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  Hapana kaka. Endowment fund ni kwa wafanyakazi wote wa shirika husika. Hii ni njia bora kabisa kuhakikisha kuwa wafanyakazi wa shirika wanakaa kazini muda mrefu ie low turn over.
  Gratuity inawahusu wakuu katika shirika peke yake. Hili ni tatizo kubwa na ndio maana kamati imeamua kupiga marufuku.
   
 15. Sita Sita

  Sita Sita JF-Expert Member

  #15
  Apr 1, 2011
  Joined: Aug 25, 2008
  Messages: 1,197
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  People are very smart and creative

  if you close on door

  they will search for ways to open another one

  The solution is to open the doors with a limit.

  Just give them the gratuity and endowment but the amounts should be scaled

  The amounts should be realistic with the work they have done (i.e. they should be paid according to achievements in that financial year)

  It you did not achieve to accomplish what was planned then you do not deserve that gratuity or endowment.

  There are hundreds of people who can fill in their positions if they decide to leave.
   
 16. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #16
  Apr 1, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Mh. Zitto umefanya vizuri sana kujitokeza mapema kuweka sawa ili jambo, kuepusha Controversy lakini najua tu watakuja wale wagonjwa wako wanaoumwa Zittophobiasis! najua upo tayari kuwapa dawa
   
 17. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #17
  Apr 1, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  This has to be taken seriously sababu gratuity wanayochukua hawa wakuu katika shirika peke yake sasa hivi imeishafanywa siri mtu mmoja anachukua gratuity ya karibia milioni 100.
   
 18. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #18
  Apr 1, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Zitto NA WENGINEO,

  Naomba kuuliza ili kuepekana na hizi policy za serikali hasa katika pension funds na marupurupu ya kujilimbikizia kwanini wakurugenzi (directors) na utawala wasiwe wanapewa contract za miaka 5. Na katika contract za miaka 5 malipo yao kuwepo na mshahara (lump sum), na incentive based on PERFORMANCE???

  Swali jengine ni malipo ya wakurugenzi wakuu wa hizi pension kwanini SSRA isiweke kipengele kuwa kila mwaka malipo haya yatolewe in public ijulikane?

  Nauliza tu kutaka kufahamu.
   
 19. G

  Godwine JF-Expert Member

  #19
  Apr 1, 2011
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  mimi sichangii kwani nina maslahi nayo
   
 20. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #20
  Apr 1, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Unasema!!!
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...