Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 117,561
- 217,865
Labda kwa kuwafichulia siri , mimi ni miongoni mwa wazaliwa wa Kanda hii Kabambe , natokea kijiji cha Kajunjumele Wilaya ya Kyela , ni miongoni mwa wadau kadhaa waliochangia kuifuta ccm Kyela, wengine ni Japhet Mwakasumi sasa Marehemu, japo baadaye aliunga juhudi, ila demage aliyoisababishia CCM Kyela haikuweza kufutika , Mzee Kasyupa Alipipi aliyewahi kuwa mbunge wa ccm na Waziri mdogo wa kilimo, mwingine ni Mwanyamaki aliyemshinda Mwakyembe na kuporwa ushindi na polisi kwenye uchaguzi wa 2015, Alinanuswe Mwalwange na King Spoiller Mwaipopo au Gogodo, huyu ni kijana wa mjini aliyesaidia sana vijana wengi wa Kyela kuidharau ccm, idadi ya walioua ccm kyela ni ndefu sana siwezi kuimaliza kuandika hapa
Kwahiyo basi kanda hii inanihusu hasa na ndio maana huwa naguswa na kila jambo la chadema linalofanyika kwenye kanda hii
Leo Mwenyekiti Msigwa ameongoza kikao cha Kamati ya utendaji ili kupanga mikakati kadhaa katika eneo ambalo sitalitaja.
Mungu ibariki Chadema