Kamati ya utendaji Simba yakubali kukutana na Mohamed Dewji

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,399
Hatimae uongozi wa klabu ya Simba umemuandikia barua mfanyabiashara (Bilionea) Mohamed Dewji “Mo”, ya kumktaka ahudhuria kwenye kikao maluum cha kamati ya utendaji ya klabu hiyo, ili kueleza dhamira yake ya kutaka kuwekeza kiasi cha shilingi billioni 20.

Katibu mkuu wa klabu ya Simba Patrick Kahemele, amemuandikia “Mo” barua hiyo, kwa kumthibitishia maazimio yaliyopitishwa na wanachama katika mkutano mkuu wa klabu ya Simba ambao ulifanyika jana katika ukumbi wa bwalo la polisi jijini Dar es salaam.

Katika barua hiyo “Mo” ameombwa kukutana na kamati ya utendaji ya klabu ya Simba Agust 15 mwaka huu.


Cowv3hdXYAAmc-h.jpg:large
 
Ina maana wakina aveva wameshindwa kabisa kuiendesha Simba!!! Na nyie wanachama hawa watu si mmewachagua wenyewe ina maana mlikiwa Hampimi walichokuwa wanaahidi? Kama mmefikia huo uamuzi basi sawa ila mnatakiwa mfanye evaluations na tafiti ya kila kuhusiana na simba na Mali zake ili thamani halisi iwekwe na sio mtu ndo apange kiasi ambacho atawekeza maana hata ukienda sokoni kariakoo muuzaji ndo anapanga bei kwa hiyo ww mnunuzi ndo unaweza kubargain na sio we ndo unapanga bei.
 
Ina maana wakina aveva wameshindwa kabisa kuiendesha Simba!!! Na nyie wanachama hawa watu si mmewachagua wenyewe ina maana mlikiwa Hampimi walichokuwa wanaahidi? Kama mmefikia huo uamuzi basi sawa ila mnatakiwa mfanye evaluations na tafiti ya kila kuhusiana na simba na Mali zake ili thamani halisi iwekwe na sio mtu ndo apange kiasi ambacho atawekeza maana hata ukienda sokoni kariakoo muuzaji ndo anapanga bei kwa hiyo ww mnunuzi ndo unaweza kubargain na sio we ndo unapanga bei.
Na hilo swala la tathmini linakuja baada ya kukubaliana ni mabadiliko ya aina gani simba ina kwenda kufanya?
Je ni private company ambayo itanunuliwa na mtu mmoja pekee na wanasimba kubaki kama washabiki tuu kama ilivyo Azam japo haikununuliwa?

Je ni public company kama lengo la Dewiji lilivyo la kununua baadhi ya hisa na wanachama na wewekezaji wengi kuruhusiwa kununua? Japo Dewiji anahitaji kuwanunulia hisa wanachama.

Cha muhimu kwa sasa kama wana hitaji mabadiliko ni kuanza na mabadiliko ya katiba ambayo yataibadili simba kuwa public company au kuwa private company halafu watapeleka mapendekezo hayo TFF.

Pili ni lazima ifanyike tathimini au evaluation ya thamani ya mali za Simba na thamani ya kila mwanachama ndani ya simba ina gharama kiasi gani hapa lazima pande zote zishirikishwe kuanzia TFF, uongozi wa simba , wanachama na wawekezaji.

Pia ni lazima iangaliwe na ipimwe kwa uhalisia wa sasa kulingana na thamani ya simba na hisa na thamani ya hisa watakazo ona hiyo billion 20 ina thamani gani kwa hisa na thamani za hisa?

Bila shaka huu mchakato una hitaji wataalam na wanasheria sio mchakato wa kukurupuka tuu.. Ni wazi lazima watu wakae chini na wapime hayo mambo.

Pia ni lazima watu wajue kuwa Mo ametoa offer ya 20bn lakini simba wanaweza wakapima baada ya utathimini wakamwambia kwa hiyo 51% hatuwezi kukubali labda uongeze kiasi fulani au kwa hiyo 20bn utapewa 48% halafu zilizo baki zitakuwa nafasi kwa wanachama na wawekezaji wengine kununua.

Na katika huu mchakato ni lazima Simba wajisajili kwenye soko la hisa la Dares.-salaam(DSE) ili watu na wengine wanunue hizo hisa..!

Hivyo ni vyema wana simba wakawa na upole maana swala hili linaweza kuchukua mwaka mzima au zaidi kufikia makubaliano mazuri na yamanufaa.

Kwa kipindi hiki Mo anaweza wasaidia kununua wachezaji kama mpenzi wa simba wakati mchakato wa mabadiliko na mazungumzo ukiendelea..

Hapa ugumu unaweza kuwa ni thamani ya hisa na kiasi mtu anacho taka apewe na fedha aliyo nayo pia thamani ya mali za simba kwa sasa.

Ni vyema wana simba wakawa wapole kwa sasa wasitake kuharakisha mambo bila taratibu kufatwa.
 
Mimi naomba nisaidiwe haya mambo ya kisasa kidogo mageni kwangu . Unaposema 20 billion hisa asilimia 5 1 inamaana kila hisa bei gani?kama ni kugawa ina maana wakitokea watu wawili wakanunua hizo asilimia 49 zilizobaki ndio habari Imeisha au inakuweje?ajuae anielimishe
 
Kinachotakiwa ni viongozi kuonesha mapenzi na klabu kama wanachama watiifu kwa kusimamia maslahi ya klabu kwa kuhakikisha mchakato unaenda vizuri,ikiwepo na kufanya tathmini ya kina hususani katika kujua thamani halisi ya SIMBA(assets and liability)
 

Bora wamuite tu. Huyu Jamaa anatakiwa achanwe LIVE kabisa.... Yaani anang'ang'ania kupewa timu utafikiri maisha yake yanategemea Simba SC.

Anajua kuwa viongozi hawampendi ila analazimisha.
 
Back
Top Bottom