Kamati ya Uongozi wa Bunge yakutana Kwa Dharura

Sasa hapo wanakutana vipi kwa dharura wakati kila kinachoenda kujadiliwa kishajulikana.
na wana mpa zawadi ya nini wakati yeye anafanya mambo hayo kw auzalendo wake mwenyewe..?
chamsingi tumuunge mkono mh JPM kwa haya aliyoyafanya kwani anaanza kuvivaa viatu vya babu Nyerere
na sokoine.
watz bana et leo magufuli ndo mzalendo wap kina zito kabwe,, james mbatia,,tundu lisu,, walio kuwa wanapigania hi mikataba feki isi sainiwe wakati huo magufuli alikuwa ni miongoni mwa wanao shangalia na kupiga meza za bunge na kupaza sauti ndio ipite!!!!! Leo tuwe wazalendo!!!!!
 
Muda utaongea!

Kama JPM angekuwa kweli MZALENDO
1.Angekubali kukosolewa.
2.Angeacha bunge liwe huru kutekeleza wajibu wake bila kuingiliwa naye.
3.Angewaacha wapinzani wafanye siasa kama wanavyofanya CCM
4.Angefanya kazi kwa ukaribu na wapinzani ili kuifanya hata nia yake kuwa kweli ya kitaifa.
5.Aache uhuru wa mawazo.

Lakini kwa vile anaongoza bunge kwa remote control na yuko hapo kwa ajili ya kukomoa wapinzani,hakika sijui kama adhma yake itafanikiwa kwa asilimia 100
 
Kamati ya Uongozi ya Bunge inakutana kujadili namna ya kumpongeza Rais Magufuli kwa hatua anazochukua kulinda rasilimali za nchi.
Mnampongeza kitu gani ambacho siyo majukumu yake, hawa wabunge wa ccm wamekuwa hawaisimamii serikali bali wanasimamiwa na serikali, hata siku moja sijawahi kusikia sheria ikitungwa na Bunge bali kutungwa na serikali, ambapo hoja inatoka serikalini na wabunge wa ccm kupitisha kura za kidikteta za NDIYOOOOOOO kuipitisha kuwa sheria
 
Kamati ya Uongozi ya Bunge inakutana kujadili namna ya kumpongeza Rais Magufuli kwa hatua anazochukua kulinda rasilimali za nchi.
Ha ha ha ha ha ha haaaaaaaa saa nyingine natamanigi nisingezaliwa Mtanzania, na ni kwa sababu ya CCM! hii nchi bila maCCM ingekua nchi nzuri sana
 
Mimi ninadhani ni ku disclaim responsibility. Labda wanataka kusema hizo sheria na mikataba ni fake havikupitishwa na bunge la jmt
 
Nanyie members wa humu itabidi kesho mkae kikao cha dharula kunipongeza kwa kazi yangu ya kulima shamba langu maana naona tumefika huko
 
Kamati ya Uongozi ya Bunge inakutana kujadili namna ya kumpongeza Rais Magufuli kwa hatua anazochukua kulinda rasilimali za nchi.





Kuna haja ya kuifanyia uchunguzi wa kiafya hiyo kamati pamoja na wabunge wote wa ccm,haiwezekani bunge lililopitisha vifungu vya sheria vinavyoruhusu uporwaji wa Rasilimali zetu,leo ligeuke kupongeza uchafu lililoufinyanga lenyewe.Huu ni uzezeta wa kiwango cha lami!
 
Ni vizuri kupongezana ila chondechonde wasije kulipana posho kwenye hicho kikao
 
wanaenda kujadili namna ya kuwatimua wabunge wa upinzani ili Magu awanyooshe nje ya bunge kama alivyoahidi.
 
Back
Top Bottom