Kamati ya Ulinzi na Usalama Morogoro, simamieni viwango vya makanisa yanayojengwa kwa nguzo za miti na mbao bila kuta za matofali

Faana

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
31,829
33,224
Napenda kuishauri Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Morogoro, kuchukua tahadhari na kusimamia viwango vya makanisa yanayojengwa kwa nguzo za miti na mbao bila kuta za matofari.

Jana 16.01.2022 majira ya asubuhi karibia na ibada kuanza Kanisa la Nabii Joshua Lililopo Kihonda Yespa liliporomoka kutokana na either nguzo na mbao za paa lake kuoza au viwango vya ujenzi kuwa hafifu, endapo kungekuwa na waumini ndani ya kanisa hilo basi yaliyotokea Mwanza hivi majuzi (watu 14 kufariki kwa ajali) yangejirudia Morogoro kwa mamia ya waumini kufukiwa na paa la kanisa hilo.

Wito kwa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa ni kupitia upya viwango vya ujenzi wa makanisa yote yaliyojengwa kama mabanda na kuwataka wenye makanisa kuyaimarisha kwa vyuma badala ya miti na mbao kwakuwa ni hatari sana kwa maisha ya watu, hali iliyovyo kwenye kanisa hilo inatisha hivi sana, nakushauri Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na usalama ya Mkoa ufike kwenye eneo la tukio ili ujionee hali ilivyo hatarishi.
 
Naunga mkono hoja asilimia 101% sio ifanyike mikoa yote

Kanisa linajengwa ndani ya wiki hahaaaa sie huku nilipo ujenzi umeaanza tangu 2014 hadi leo 2022 ndo wanakaribia weka paaa hahaaaaa kanisa litajengwa na wenye nia na moyooo

Rome was never built in a day
 
Naunga mkono hoja asilimia 101% sio ifanyike mikoa yote

Kanisa linajengwa ndani ya wiki hahaaaa sie huku nilipo ujenzi umeaanza tangu 2014 hadi leo 2022 ndo wanakaribia weka paaa hahaaaaa kanisa litajengwa na wenye nia na moyooo

Rome was never built in a day
Asante Mkuu
 
Back
Top Bottom