Kamati ya Ulinzi na Usalama Mbona haifuatili Mikataba Mibovu? Lakini Sukari na Bei Juu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kamati ya Ulinzi na Usalama Mbona haifuatili Mikataba Mibovu? Lakini Sukari na Bei Juu?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by August, Mar 12, 2011.

 1. A

  August JF-Expert Member

  #1
  Mar 12, 2011
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,509
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  Ni nashanga kuona kamati ya ulinzi iwe ya kitaifa au kimikoa zinafuatilia "wanaopandisha bei ya Sukari" na kuacha kufuatilia mambo mengi yanayo tokea katika jamii ambayo yana madhara makubwa kwa Taifa kiuchumi na kiusalama mfano mikataba mibovu ya madini, umeme, kwenye sekta ya mawasiliano ambayo yanakwamisha TTCL kusonga mbele nk.
  Kamati ya ulinzi kusaka wauza sukari bei ya juu
  Kutoka kwenye Gazeti la Mwananchi.
  Julieth Ngarabali, Pwani
  KAMATI ya Ulinzi na Usalama mkoani Pwani, imewataka wananchi kutoa taarifa wanapobaini kuwapo kwa mfanyabishara anayeuza sukari zaidi ya Sh1,700 kwa kilo moja.

  Akizungumza baada ya kikao chao cha dharura juzi, Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Pwani, Amina Mrisho, alisema wamebaini kuwapo kwa ukiukaji wa agizo la serikali kuuza bidhaa hiyo sio zaidi ya Sh1,700.

  Mrisho alisema wajumbe wa kikao hicho waliazimia kufanya upekuzi wa kushtukiza kwa baadhi ya maduka yaliyopo ndani ya mji na vitongoji, lengo likiwa ni kuhakikisha wafanyabiashara wanatekeleza agizo la serikali.

  "Tumelazimika kukaa pamoja na mambo mengine tujipange kukabiliana na hawa wafanyabiashara wakaidi, katika hili napenda wajue hatutafanya utani, kwani hakuna sababu inayowafanya wapandishe bei," alisema Mrisho.

  Kamati hiyo iliwataka wafanyabiashara kushusha bei ya sukari kabla ya kuanza kupita madukani. Hivi sasa kilo moja ya sukari inauzwa kwa Sh2,000.

  Alisema atakayekiuka agizo atachukuliwa hatua kali za kisheria, kwani kuna sukari ya kutosha na hakuna sababu ya msingi inayowasukuma wafanyabishara hao kupandisha bei.

  Katika kuhakikisha tamko hilo linatekelezwa mara moja, Mrisho aliawaagiza wakuu wa wilaya mkoani hapa kuitisha kamati za ulinzi na usalama kuweka mikakati ya kutekeleza suala hilo.

  Kwa upande wao wafanyabishara, walisema hawajagoma kutekeleza agizo la serikali, bali wanalazimika kuuza Sh2,000 kutokana na maduka ya jumla kuwauzi mfuko mmoja wa kilo 50 kati ya Sh85,000, bei ambayo ni sawa na Sh1,680 kwa kilo.

  Wafanyabiashara hao waliomba serikali kutoa agizo kama hilo kwa wafanyabishara wa jumla, ambao bei zao bado zipo juu ili kuwawezesha kutekeleza agizo la serikali.
   
Loading...