Kamati ya uchunguzi wa Jairo hii hapa

Mathias Byabato

JF-Expert Member
Nov 24, 2010
1,020
691
Neville Meena, Dodoma
MKUTANO wa nne wa Bunge la Bajeti ulihitimishwa jana kwa Spika wa Bunge, Anne Makinda kutangaza majina ya wabunge watano, wanaounda Kamati Teule kuchunguza utaratibu uliotumiwa na Wizara ya Nishati na Madini, kukusanya fedha kutoka katika taasisi zilizopo chini ya wizara hiyo kwa ajili ya kufanikisha mchakato wa kupitisha wa bajeti.

Makinda akihitimisha Bunge baada ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kutoa hoja ya kuahirisha bunge, alisema kamati hiyo itakayofanya kazi kwa wiki zisizozidi nane pia itachunguza iwapo hatua ya Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo, kutangaza matokeo ya uchunguzi dhidi ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, David Jairo uliingilia haki na madaraka ya Bunge.

Hii ni kamati teule ya pili kuundwa wakati wa uongozi wa Rais Jakaya Kikwete, lakini kwa wizara hiyohiyo ya Nishati na Madini ambayo hivi sasa inaongozwa na Waziri William Ngeleja.

Februari 7, 2008 aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa na waliowahi kuwa mawaziri wa Nishati na Madini, Dk Ibrahim Msabaha na Nazir Karamagi walilazimika kujiuzulu baada ya kutajwa katika ripoti ya Kamati Teule ya Bunge iliyoundwa kuchunguza mkataba tata wa Kampuni ya Kufua Umeme wa Dharura ya Richmond.

Kamati hiyo iliongozwa na aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini, Dk Harrison Mwakyembe. Mwakyembe sasa ni Naibu waziri wa Ujenzi.

Wanaounda kamati ya kumchunguza Jairo ni mbunge wa Tunduru Kaskazini, Injinia Ramo Makani (CCM), Mbunge wa Karagwe, Goesbert Blandes (CCM), Mchungaji Israel Natse (Karatu-Chadema), Khalifa Suleiman Khalifa (Gando-CUF) na Mbunge wa Viti Maalum, Martha Jachi Umbulla (CCM).

"Mtakumbuka kwamba tarehe 24, Agosti, 2011, Bunge lilipitisha azimio la kuunda Kamati Teule kwa ajili ya kuchunguza uhalali wa utaratibu wa Wizara kuchangisha fedha kwa ajili ya kupitisha bajeti na kubaini kama kitendo cha Katibu Mkuu Kiongozi, kutoa taarifa kwa waandishi wa habari juu ya uchunguzi wa suala la fedha zilizokuwa zikichangishwa na Wizara ya Nishati na Madini kimeingilia na kuathiri madaraka ya Bunge," alisema Makinda na kuongeza:

"Sasa napenda kuwataarifu kwamba utaratibu huo umekamilika na kamati hiyo nimeiunda kwa mujibu wa Kanuni ya 2(2) na 117(4) ya Kanuni za Bunge toleo la 2007".

Makinda alisema kamati hiyo itafanya kazi kwa kuongozwa na hadidu tano za rejea ambazo ni kuchunguza utaratibu uliobainika wa kukusanya fedha kwa ajili ya kukamilishwa kwa uwasilishaji wa Hotuba za bajeti za wizara bungeni na kwamba, hadidu hiyo ya kwanza itakuwa na vipengele vitatu.

Vipengele hivyo ni pamoja na kuchunguza uhalali wa utaratibu huo kisheria na kwa mujibu wa kanuni, iwapo fedha hizo huwa zinakasimiwa katika bajeti husika pamoja na matumizi halisi ya fedha zilizokusanywa.

"Hadidu rejea ya pili ni kupitia taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuhusu uchunguzi alioufanya kuhusiana na agizo la Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini kuchangisha fedha taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo kwa ajili ya kufanikisha uwasilishaji wa Bajeti ya Wizara hiyo Bungeni," alisema Makinda na kuongeza:

"Hadidu rejea ya tatu ni kuchunguza mfumo wa Serikali kujibu hoja zinazotolewa bungeni na taratibu za kuarifu Bunge matokeo ya utekelezaji wa hoja hizo".

Makinda alisema hadidu rejea hiyo ya tatu ina vipengele viwili ambavyo ni kuchunguzwa kwa usahihi wa utaratibu uliotumiwa na Katibu Mkuu Kiongozi kwa suala la Jairo na kubaini iwapo utaratibu huo umeathiri dhana ya haki na madaraka ya Bunge.

Aliitaja hadidu ya rejea ya nne kuwa ni kuangalia nafasi ya Mamlaka ya Uteuzi kwa ngazi za Makatibu Wakuu katika kushughulikia masuala ya nidhamu ya anaowateua na ya mwisho inawaelekeza wajumbe wa Kamati hiyo kuangalia mambo mengine yoyote yenye uhusiano na uchunguzi huo.

"Ni imani yangu ya wabuge wote na Watanzania wote kwa ujumla kwamba ninyi niliowateua mtafanya kazi hii kwa umakini, busara na uaminifu mkubwa mkiongozwa na Katiba ya nchi, sheria na kanuni zetu na vilevile mtatoa haki kwa watu wote watakaohusika na suala hili," alisema Spika Makinda.

Rais Kikwete alimsimamisha kazi Jairo kwa mara ya pili ili kupisha uchunguzi zaidi juu ya tuhuma zinazomkabili kuhusiana na matumizi mabaya ya madaraka yake.

Hatua hiyo ilithibitishwa juzi na Waziri Mkuu, wakati akijibu maswali ya papo kwa hapo bungeni. Pinda alisema kuwa, suala la Jairo limefika kwa Rais na tayari kiongozi huyo wa nchi amekwishalitolea uamuzi.

Jumanne wiki hii wabunge walitishia kusimamisha shughuli zote za Serikali katika Bunge hilo hadi hapo uchunguzi wa Jairo ambaye alituhumiwa na Mbunge wa Kilindi kuwa anahusika na uchangishaji wa fedha zitakapopelekwa bungeni.

Kitendo cha wabunge kutoa kauli hiyo kilitokana na kauli ya Luhanjo kutangaza kuwa Jairo hakupatikana na hatia katika uchunguzi uliofanyika na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na kwamba, alitakiwa kurudi kazini kuanzia Jumatano.Uamuzi wa kuundwa kwa kamati teule ulifikiwa Jumanne baada ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, kusema kuwa Luhanjo alikuwa amelidharau Bunge na Waziri Mkuu.

Baada ya mchakato wa kikanuni, suala hilo lilihitimishwa kwa kukubaliana na hoja ya Mbunge wa Simanjiro, Christopehr Ole Sendeka (CCM), ambaye alipendekeza kuundwa kwa kamati hiyo.

Chanzo-Mwananchi.
 
Mheshimiwa Spika kwa mamlaka aliyopewa na kanuni za Bunge amewateua wafuatao
. Eng. Makani
Goseberth Blandes
Israel Natse
Khalifa S. Khalifa
Martha Umbulla
 
Jioni hii wakati spika akikamilisha shughli za bunge,ametaja kama kamati iliyoundwa,wajumbe ni Mh.Ramo mathayo makani,Mh.Gosbert blandes,Mhe.Halifa suleiman halifa,Mhe.Martha humbula..(hayo ndio majina kama nimekosea rekebisha)
 
Kamati ya teule ya Bunge itapitia Hadidu rejea zifuatazo.


Uhalali wa utaratibu huo kisheria na kikanuni.
Kupitia hesabu za Mkakuguzi mkuu wa serikali
Kuchunguza mfumo wa serikali kujibu hoja zitolewazo bungeni.

Kuangalia nafasi ya mamlaka ya nafasi ya makatibu wakuu anaowateua
Kuangalia mambo mengine yahusianayo

Wajumbe


Ramo matala makani - Mwenyekiti

Gosbert Gumisha
Israel Yohana
Halifa Suleiman hali
Lachi humbula

Muda wa uchunguzi

Kamti itahitajika Kufanya kazi kwa Kipindi cha wiki nane.
 
Ungetulitea na wasifu wa kila mjumbe ingekuwa vizuri zaidi
 
Sijawahi kuwasikia hawa wabunge hata mmoja!! sijui pia wasifu na vyama vyao.... wenye taarifa watujuze...Naona pia spika amesita kuweka vichwa vyenye majina makubwa sijui hatima yake nini?
 
Tanzania bwana! Tunalalamikia wizi wa fedha za umma halafu tunachunguza kwa kutumia pesa za umma ilihali majibu tunayo! Kisha Bunge nalo

linaishia kuunda kamati ambayo pamoja na mambo mengine inamchunguza CAG! Kama watanzania hawataridhika labda na kikwete aunde yake

kuweka mambo sawa. Matatizo yetu yanakuwa source ya ulaji kwa wengine
 
Mh!sizani kama watakuta lolote kwa jairo.kama awali alisafishwa,na sasa wanataka kumchunguza sioni kama kuna ma ntiki yoyote,alikua wa kumpeleka mahala husika kujibu tuhuma mizinguo tu wanayotulea kama alivyosema JAIRO kuwa ni ZE COMEDY.
 
Hawa si ni ma CCM wote ? Maana kama ni hilo basi hakuna kitu hata kimoja .
 
mheshimiwa spika kwa mamlaka aliyopewa na kanuni za bunge amewateua wafuatao
. Eng. Makani
goseberth blandes
israel natse
khalifa s. Khalifa
martha umbulla

najua blandes ni mwanasheria lakini hao wengine................ Tusubiri tuone.
 
Mh! Hawa wajumbe mbona simjui hata mmoja? Mh nina wasiwasi

Huwa wanalala sana, kwa vile tuu hawajanaswa! Natse nimewahi kumsikia mara moja kwenye wizara ya ardhi akichangia. Kwa staile ile sidhani kama

ananguvu ya kufanya mambo yaende. . . Labda kwa kuwa ni mchungaji atasimamia haki (Kama kweli anamtii Mungu), Vinginevyo tusitegemee

kitu. Kashfa nzito hazichunguzwi legelege. Spika atakuwa amepewa maelekezo tuu from above!
 
najua blandes ni mwanasheria lakini hao wengine................ Tusubiri tuone.

All lawyers are corrupted! Serve few with very distinction. Laiti wanasheria wangesimamia haki na ukweli! Nchi yetu ingekuwa mbali sana. But

Tanzanian lawyers have actively participated in screwing our nation. .. . Na bado wengi hatuwafahamu! Most of exceptional leaders in the world are

lawyers! If Tanzania Lawyers would stand in their positions!
 
Back
Top Bottom