Kamati ya uchunguzi wa Jairo hii hapa

Mbona hao woote kama walalaji Bungeni, kweli wanajua hata nini kinaendelea, maaana isijekua wamestushwa na wito wa spika , na kisha kusababisha wakaenda kumuuliza sasa tufanyaje
<br />
<br />
watapewa maelezo ya nn cha kufanya.
Ripot imeshaandaliwa wao ni ku-edit kwa kutumia maneno yao.
 
hili nalo limeisha tunasubiri tukio lingine maana nchi hii ni full movie........
 
Kama Bunge lingekuwa serious kwenye mambo ya nchi, serikali ingekuwa makini na mambo inayofanya. Bunge limeunda tume kuchunguza pesa zilizotolewa na hizo taasisi zilizo chini ya wizara ya nishati na madini, lakini hiyo kamati teule inaweza ikatumia zaidi ya pesa zinazochunguzwa. Na mwishowe ikawa kama kamati teule ya dokta Harison Mwakyembe, hamna hata mmoja aliyefikishwa mahakamani. Serikali iliwasafisha watumishi wake kama mkuu wa PCCB, mwanasheria mkuu aliyepita nk. Kamati ile ilisababisha uspika wa Sita kuota mbwawa, Wakina Mwakyembe kupewa Uwaziri ili kuwafunga mdomo. Mimi siono jipya katika hiyo kamati teule, biashara itakuwa kama ile ya richmond.

Kama wabunge wangekuwa serious, wangekuwa wameshaunda kamati teule kuchunguza kampuni kama KAGODA,MEREMETA, DEEP GREEN FINANCE,utoroshaji wanyama pale KIA nk, lakini hawawezi. Wanajua wakifanya hivyo ni sawa na kukata tawi ambalo wabunge wenyewe wamekalia( Wabunge wa CCM), mwishowe wanaishia kumng'ang'ania Jairo tu

Kama wangekuwa serious wangekuwa wameshawachunguza wabunge wa kamati ya hesabu za serikali za mitaa waliotuhumiwa na Kafulila kwamba walipokea rushwa,

Wangekuwa serious wasingeishia kwa Jairo, wangeangalia mfumo mzima wa serikali, wangepata majibu zaidi ya hilo. Hapo hamna hata Katibu Mkuu wa Wizara au Waziri ambaye angepona.

Kuna msomi mmoja anaitwa PROFESA ISA SHIVJI, ALISEMA UFISADI KATIKA SERIKALI UNASABABISHWA NA MFUMO ULIOPO. HATA KIONGOZI AWE MSAFI KWA KIASI GANI LAKINI KWA MFUMO ULIVYO, ATAANGUKA TU
 
Hakuna umakini woowte hapo Ni sawa sawa na kesi ya ngedegere na nyoka kumpa nyani. Uhaifu wote utaonekana ni wa nyoka.

Wabunge ni wanufaika wa hizo pesa na inawezekana walizipokea na . What if kwenye hiyo hiyo kamati mmoja au wawili wa wajumme alipokea hizo bahasha. ??????

simply kamati iliyotakiwa kuundwa ilitakiwa isiwe ya wabunge bali majaji wastaafu kama kina warioba Serikali na wabunge ni suspect hawawwezi kujichunguza. Kudhani bunge ni safi kwa hii kashafa ni changa la macho

Na kuchunguza wizara moja na yenyewe n kama ni movie basi iko kwenye mfumo wa cartooon. wametufanya watoto...... teh teh teh teh

Kwa style hii hii movie kila mtu anaweza kujua itakwishaje. Tom and Jerry
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Mi nina wasiwasi na terms of reference, inaonyesha kama hii nishati na madini ni sample lakini issue ni kuchunguza michango ya bajeti katika wizara mbalimbali, nimemsikia mama makinda na nasubiri ripoti za magezeti yakesho yaliyokopi kwenye hansard ili nizitafakari hizi terms of reference. Kuhusu wajumbe sina hoja nafikiri msingi uliotumika pia ni muhimu kwani waliotuhumu moja kwa moja wangepewa nafasi ya kuchunguza lazima wangekuwa biased. Huyu bwana ni kweli tunamtuhumu lakini kuna issue ya natural justice hapo, tunaomba hawa wajumbe wachunguze ikiwezekana hata five years back, huyu ni mgeni lakini napata hisia kuwa hiki chanzo ambacho sio rasmi kimekuwa kisima kikuu cha ufisadi kipindi cha bajeti. Waende na wizara ya fedha na wizara nyingine, inawezekana tukawa tunamuonea Jairo kumbe kuna wizara nyingine zimechangisha mabilioni ya pesa. USHAURI WANGU, HII FURSA ITUMIKE KUTUJULISHA NI KIASI GANI KIMESHAKUSANYWA HATA IKIBIDI KATIKA WIZARA NYINGINE NA MATUMIZI YAKE, SWALI? KWANINI UTARATIBU HUU UENDELEE WAKATI MATUMIZI YOTE YA SERIKALI LAZIMA YAWE BUDGETED NA YANAPITISHWA NA BUNGE? HIZO OC ZINA GAZI GANI???? TUFUNGUENI JAMANI TUNA MATARAJIO MAKUBWA.
 
kikwete nadai anazungukwa pale ikulu maana hata taarifa ya kurejea jairo aliipata asubuhi ya tarehe 25.na papo hapo akamuru asimamishea na yeye mwenyewe ataamia ni lini na wapi jairo atarudi kazini
 
Itafana kazi kwa muda wa wiki nane.

Leo ni Friday, August 26, 2011.

Kama Kamati ikianza kazi Jumatatu ijayo basi earliest deadline ni Monday, October 24, 2011.

Wekeni kwenye diary zenu!
 
Hakuna umakini woowte hapo Ni sawa sawa na kesi ya ngedegere na nyoka kumpa nyani. Uhaifu wote utaonekana ni wa nyoka.

Wabunge ni wanufaika wa hizo pesa na inawezekana walizipokea na . What if kwenye hiyo hiyo kamati mmoja au wawili wa wajumme alipokea hizo bahasha. ??????

simply kamati iliyotakiwa kuundwa ilitakiwa isiwe ya wabunge bali majaji wastaafu kama kina warioba Serikali na wabunge ni suspect hawawwezi kujichunguza. Kudhani bunge ni safi kwa hii kashafa ni changa la macho

Na kuchunguza wizara moja na yenyewe n kama ni movie basi iko kwenye mfumo wa cartooon. wametufanya watoto...... teh teh teh teh

Kwa style hii hii movie kila mtu anaweza kujua itakwishaje. Tom and Jerry




umeisoma taarifa ya ikulu leo mkuu? jk anadai taarifa juu ya jairo alikuwa hajui kama amerudi kazini ila aliambia asubuhi ya tari 25....na papo hapo akaagiza aendelee na likizo na yeye ndo ataamua ni lini jair atarudi kazini na wapi atapangiwa....so unaweza kuona jinsi tukio kubwa kama hili linafanyika yanapita masaa zaidi ya 11 mkuu wa nchi hana habari..... analalamika kuwa anazungukwa pale ikulu...halafu asivyo na maana anasema hivi'' mimi sijashinikizwa na mtu kuchukua maamuzi haya'
 

HII TAARIFA IMENISHANGAZA SANA......jk hakuwa na habari


UNITEDREPUBLIC OF TANZANIA

DIRECTORATEOF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS


Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com
press@ikulu.go.tz
[h=4]Fax: 255-22-2113425[/h]
PRESIDENT'S OFFICE,
THE STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
[h=5][/h]



TAARIFAYA UFAFANUZI
Tarehe 21 Julai,mwaka huu, 2011, Katibu Mkuu Kiongozi Bwana Phillemon Luhanjo,akitumia madaraka yake ya Mamlaka ya Nidhamu ya Watumishi wa Umma,alitangaza hatua ya kumpa likizo ya malipo Katibu Mkuu wa Wizara yaNishatai na Madini, Bwana David Kitundu Jairo, ili kupisha uchunguzialiokuwa ameuagiza ufanyike dhidi yake.
Bwana Luhanjoalichukua hatua ya kumsimamisha Bw. Jairo kufuatia tuhuma zilizokuwazimeelekezwa dhidi yake na baadhi ya wabunge wakati wa mjadala kuhusuMakadirio na Matumizi ya Wizara ya Nishati na Madini kwa mwaka2011/12 katika kikao cha Bunge kilichofanyika tarehe 18 Julai, 2011.
Katika mjadalahuo, baadhi ya wabunge walihoji uhalali wa Wizara kuomba michango yafedha kutoka kwenye Taasisi zilizoko chini ya usimamizi wake ilikusaidia Bajeti ya Wizara hiyo kupita kwa urahisi.



Kufuatia hatuahiyo ya kumsimamisha kazi Bw. Jairo, Katibu Mkuu Kiongozi alimwombaMdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Bwana LudovickUtouh kufanya ukaguzi maalum na uchunguzi wa awali juu ya tuhumahizo.
Tarehe 9 Agosti,mwaka huu, 2011, Bw. Utouh aliwasilisha Ripoti yake kwa Katibu MkuuKiongozi, na tarehe 23, Agosti, 2011, Katibu Mkuu Kiongoziakiambatana na Bw. Utouh alitangaza mbele ya waandishi wa habarimatokeo ya ukaguzi huo maalum na uchunguzi wa awali juu ya tuhumadhidi ya Bw. Jairo.
Katika Ripoti yakembele ya waandishi wa habari, Bw. Utouh alihitimisha:"Ukaguzi maalum haukuthibitisha kuwepo kwa usahihi wa tuhumazilizotolewa dhidi ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Bw.David Kitundu Jairo."
Kufuatia Ripotihiyo ya Bw. Utouh, Katibu Mkuu Kiongozi naye aliwaambia waandishi wahabari: "Matokeoya uchunguzi huo ni kwamba tuhuma zilizotolewa Bungeni tarehe 18Julai, 2011, hazikuweza kuthibitika. Kutokana na matokeo haya yauchunguzi wa awali, mimi kama Mamlaka ya Nidhamu ya Katibu Mkuu,Nishati na Madini, Bwana David Kitundu Jairo, sitaweza kuendelea nahatua ya pili ya kumpa taarifa ya tuhuma (notice) na Hati yaMashitaka kwa sababu Bwana David Kitundu Jairo, hajapatikana na kosala kinidhamu (disciplinary offence) kwa mujibu wa Taarifa ya UkaguziMaalum."
Alihitimisha:"Kufuatiamatokeo ya taarifa hii ya awali na kwa mamlaka niliyonayo kwa mujibuwa Sheria Na. 8 ya Utumishi Umma ya Mwaka 2002 na kanuni zake zaMwaka 2003, NINAAMURU BWANA DAVID KITUNDU JAIRO AREJEE KAZINI KUANZIASIKU YA JUMATANO, TAREHE 24 AGOSTI, 2011."
KURUGENZI YAMAWASILIANO YA RAIS, IKULU,inapenda kutoa ufafanuzi kuwa baada ya kupokea taarifa ya uchunguziya CAG na uamuzi wa Katibu Mkuu Kiongozi kuhusu suala hilo asubuhi yatarehe 25 Agosti, 2011, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, Rais waJamhuri ya Muungano wa Tanzania, aliamua kuwa Ndugu Jairo asirudikazini mpaka kwanza yeye Rais atapoamua namna gani ya kurudi kazini,lini na wapi.
Katibu MkuuKiongozi alifikisha uamuzi huo wa Rais kwa Ndugu David Jairo ambayemapema asubuhi ya siku hiyo alikuwa ameripoti kazini. Ndugu Jairoalitii uamuzi huo wa Rais.
Tunapendakusisitiza kuwa Mheshimiwa Rais hawaja kigeugeu kwa sababu alifanyauamuzi mmoja tu baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Katibu MkuuKiongozi. Na uamuzi huo aliufanya kabla ya Bunge kulizungumzia sualahilo na hivyo uamuzi huo wa Rais haukutokana na shinikizo la Bunge.Pamoja na kumweleza Katibu Mkuu Kiongozi, Rais pia alimfahamishaWaziri Mkuu kuhusu uamuzi wake huo asubuhi hiyo ya tarehe 25, 2011.
Aidha, tunapendakufafanua zaidi kwamba Katibu Mkuu Kiongozi ametimiza wajibu wakeipasavyo kama Mamlaka ya Nidhamu kwa Katibu Mkuu kwa mujibu waSheria, Kanuni na Taratibu za Utumishi wa Umma. Mheshimiwa Rais, kwaupande wake, ametumia madaraka yake kama Mamlaka ya Ajira ya KatibuMkuu. Hakuna suala la kujichanganya wala ukigeugeu ndani ya Serikalikuhusu suala hili.
Mwisho.
Imetolewana Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
Dares Salaam.
26Agosti, 2011
 
najua blandes ni mwanasheria lakini hao wengine................ Tusubiri tuone.
pia Gosbert ni kinara wa wizi wa kura huko Jimbo la karagwe hivyo tutegemee wizi na taarifa fake ya kupikwa tu!
 
naunga mkono wanaotaka NBAA wamfutie usajili utoah kama kachakachua,isiwe NBAA wanakua wakali kwa akina pangu pakavu tu.
 
Jairo ametuhumiwa na bunge,na yeye akawaita zecomedy. Waliotuhumu wanaunda tume,na wanataka sisi wote tuamini kile watakachokipata. Yale yale ya CAG na Luhanjo kumlinda Jairo! Tunapoteza pesa kwa jambo ambalo bunge lingetoa tamko kwamba huo utaratibu wa kuchangisha pesa ukome. Maana ktk hali halisi tunaona ni kwanini CDM walikua wanapinga hii kitu inaitwa posho. Kamati ama tume ya maana ingekua na uwakilishi mpana,ikishirikisha bunge,serikali,wasomi, na taasisi za kirai.
 
najiuliza hii kamati imeundwa kwa nini kama raisi yeye ndo ataamua ni lini na wapi na namna gani jairo arejee kazini
 
hiyo kamati imechaguliwa kwa vigezo vipi? Mi naona panakitu fulani kimefichwa kwenye hio kamati,mbona hamna wapiganaji kwenye hio kamati? Watamweza jairo anayelindwa na ikulu? Tz nchi ya malofa.
 
naunga mkono wanaotaka NBAA wamfutie usajili utoah kama kachakachua,isiwe NBAA wanakua wakali kwa akina pangu pakavu tu.

utouh hana uwezo wa kuchunguza.........yeye kazi yake ni kuangalia risiti kama zipo hata kama n feki.....sso uchunguzi ulipaswa kufanywa na majaji wastaafu ...hata hii kamati ni usitegemee kipya......
 
&lt;br /&gt;<br />
&lt;br /&gt;<br />
mbona sio majina maarufu?
<br />
<br />
kanuni hazitaji km mbunge atakayeuunda kamati km hii awe maarufu.Ila mi pia nina wasiwasi maana wengine hapo waliingia bungeni kwa nguvu za dola!Especially Gosbert Blandes!Alichakachua jimbo la karagwe.Chadema walisemekana kushinda.
 
umeisoma taarifa ya ikulu leo mkuu? jk anadai taarifa juu ya jairo alikuwa hajui kama amerudi kazini ila aliambia asubuhi ya tari 25....na papo hapo akaagiza aendelee na likizo na yeye ndo ataamua ni lini jair atarudi kazini na wapi atapangiwa....so unaweza kuona jinsi tukio kubwa kama hili linafanyika yanapita masaa zaidi ya 11 mkuu wa nchi hana habari..... analalamika kuwa anazungukwa pale ikulu...halafu asivyo na maana anasema hivi'' mimi sijashinikizwa na mtu kuchukua maamuzi haya'

Unajua nishajua moja ya mapendekezo na makosa ambayo kamati itakuja nayo.

KOSA
watasema wizara ilifanya kosa kuomba pesa za kuendesha shughuli zake kutoka kwenye idara zilizo chini yake.Kosa la pesa za "mawasiliano" halitatjwa na litakwepwa.. Kosa ya integrity ya wabunge kuwa compromised halitatajwa pia.......

MAPENDEKEZO
wizara ipange bajeti yake vizuri na iwe kamili kuondoa makosa ya kuomba omba fedha . Hiyo itasadaia movie hizi sizijulikane kwa wananchi. teh teh teh teh
Tena watasema hili tatizo linatokana na wizara kupewa bajeti ndogo. so serikali itashauriwa iongegeze bajeti wizara hata ama zitoongeza deficit

NB

Kumbuka wizara nyingi zinafanya hivi inawezekana nafuu yao ni kwamba wizara nyingine hawajachangisha bali toka mwanzo makao makuu wanafungu ya kuchota pesa za "mawasiliano". So Kosa kubwa litaloonekana na wizara ya nishhati ni kuchangisha pesa kutoka idara nyingine Movie kwishney. Tutapiga makofi

Kinyume na hapo

  • wakifichua ukweli wote na uozo wote watakuwa wamemdhalilisha CAG na katibu Mkuu kiongozi na hata wabunge - Hii tusitegemee Tanzania bado hatujafikia hapa
  • hawawezi kuifcha makosa watakuwa wamemdhalilisha PM aliyesema angemfukuza Jairo. -

So itabidi wafanye compromise kuridhisha pande zote bila kuathiri au kudhalilisha pande zote (serikali na bunge).Kazi ngumu lakini kwa wanasiasa wa kitanzania ni kama kufumba macho gizani.

Mwisho wa siku mwananachi wa kawaida ndio kabiwa

Movie kwisha Tutasubiri series nyingine hope ile ya UDA itakuwa tayari kutoka kwenye majukwaa ya habari ikiwa edited kulingana "maproducer" wanavypenda watazamaji na wasomaji tuone
 
Yani hawa wabunge na vuguvugu lote lile bungeni mi siwajui hawa bila shaka walikuwa madoja afadhari hata wasira yeye alikuwa anakuja kulala zake2 mjengoni thn anasaini mzigo unaingia!
 
Back
Top Bottom