Kamati ya Uchaguzi ya TFF yapitisha Jina la Wallace Karia kuwa Mgombea pekee wa nafasi ya Urais

Kuna haja ya Chadema kupisha mawazo mapya maana haiwezekani mtu mmoja kuwa ndio Mwenyekiti wa kudumu huku ukihimiza demokrasia na kudai katiba mpya, kwanza tuanze na katiba za vyama kufanya nafasi ya uwenyekiti kuwa na vipindi maalum.

Hii sio kwa Chadema tuu mpaka CUF,TLP,UDP na wengineo muache kuhodhi madaraka.
 
Bwashee mbna unapwaya hv????
CCM wana demokrasia pana sana linapokuja swala la uchaguzi wa ngazi zote tofauti na Chadema ambao mgombea wa nafasi ya mwenyekiti ni " yule yule " miaka nenda rudi.

Chadema inafanana sana na TFF ambayo mgombea wake wa kudumu kwa nafasi ya Rais ni Wallace Karia.

Karia ni CCM lakini anaendesha TFF kichadema Chadema.

Nawasalimu kwa jina la JMT!
 
Ndio maana ya vile vikanuni vya kipuuzi puuzi mara wadhamini sijui ujinga gani, lengo ndio hili kuwachuja wote bila sababu abaki mmoja tu
 
Wallace Karia amekuwa mgombea pekee wa nafasi ya Urais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) baada ya Kamati ya Uchaguzi ya TFF kuwaengua Evans Mgeusa na Hawa Mninga kwa kukosa sifa.

Karia anagombea nafasi hiyo kwa muhula wa pili.

======

Wallace Karia amepita kuwa Mgombea pekee kuelekea kwenye uchaguzi mkuu wa kutafuta viongozi wa Shirikisho la mpira wa Miguu Tanzania TFF.

Wagombea wengine wawili Evans Mgeusa na Hawa mniga hawajafuzu vigezo.

Kwa mujibu wa katiba ya TFF "kama ikitokea mgombea wa Urais amebaki peke yake na amekizi vigezo basi hatopigiwa kura na badala yake ataenda kuthibitishwa na wajumbe wa Mkutano mkuu"

Kwa maana hiyo Wallace Karia atasubiri kuthibitishwa na wajumbe wa mkutano mkuu baada ya kubaki peke yake.

Chanzo: Maulid Kitenge
Lugha nyepesi ni kwamba kapita bila kupingwa.

Huyu Msomali kweli katuweza Wabongo.
 
Kwa taarifa za hivi punde ni kuwa mgombea urais wa TFF Ndugu Wallace Karia amebaki mgombea pekee baada ya wenzake aliokuwa anagombea nao kukosa sifa! Na hivyo huyo jamaa anasubiri tu utaratibu wa kumtawaza aendelee kuwa rais wa TFF.

Najua kwa Tanzania yetu hili la kupita bila kupingwa si jambo jipya! Jipya ninaloliona ni kwanini na wale jamaa zangu ninaofahamu fika kuwa ni ccm kindaki ndaki nao walalamikie utaratibu wa ovyo uliompitisha Wallace Karia?? Wengine wa ajabu kwenye kadhia hii ni hawa "ndugu wahandisi wa habari"! Wanaropoka kupitiliza

Binafsi Principles zangu zinakataa kata kata huu undumilakuwili unaoneshwa. Kama walikaa kimya kipindi wabunge wa ccm wanapitishwa bila kupingwa wakae hivyo hivyo kimya kipindi hiki cha Wallace Karia. Kwa maana nyingine hawana moral audacity kuzungumzia au kulalamikia uozo wa TFF kama uozo huo huo waliubariki kipindi cha ccm na NEC.

(Ni kama tu ishu ya Diamond ilivyokuwa kule BET Awards! Hakuna sehemu aliwahi kusimama na wananchi kutetea maslahi yao dhidi ya utawala dhalimu. Zaidi ya yote hakuwa na moral audacity ya kuvaa kimaasai wakati hajawahi kuwa sauti ya wamaasai kwa lolote, popote! Unafiki ulipitiliza unafiki!)

Mfumo utakaotumika kumpata na kumsimika Wallace Karia unatokana na Katiba ya TFF. Inasemekana ni Katiba mbovu sana! Halikadhalika mfumo unaotumika kuwapata na kuwasimika viongozi waliopita bila kupingwa unatokana na Katiba yetu ambayo ni mbovu zaidi ya ubovu wenyewe!

Tuwe watu wa principles. Wenye uwezo wa ku-command moral audacity! Tunapopiga kelele yale ya Wallace Karia tupayapazie sauti na kukemea yale ya ccm na Katiba ya nchi.
 
CCM wana demokrasia pana sana linapokuja swala la uchaguzi wa ngazi zote tofauti na Chadema ambao mgombea wa nafasi ya mwenyekiti ni " yule yule " miaka nenda rudi...
Acha upotoshaji wako!

TFF wameiga kutoka ccm na NEC.

Tujifunze kuuchukulia uchaguzi kama Hatua mojawapo ya kupata ridhaa na baraka za wanaongozwa.
 
Imekwisha hiyo, tukutane tena 2025 kwenye uchaguzi mwingine wa TFF, ambao kama kawa Msomali atakuwa mgombea pekee tena kwenye nafasi ya urais katika uchaguzi huo kwa ajili ya kukamilisha awamu yake ya tatu ya uongozi kwa mujibu wa katiba ya TFF. Wasiompenda wataendelea kuinjoi show mpaka 2029.
 
Wallace Karia amepita kuwa Mgombea pekee kuelekea kwenye uchaguzi mkuu wa kutafuta viongozi wa Shirikisho la mpira wa Miguu Tanzania TFF.

Wagombea wengine wawili Evans Mgeusa na Hawa mniga hawajafuzu vigezo.

Kwa mujibu wa katiba ya TFF "kama ikitokea mgombea wa Urais amebaki peke yake na amekidhi vigezo basi hatopigiwa kura na badala yake ataenda kuthibitishwa na wajumbe wa Mkutano mkuu"

Kwa maana hiyo Wallace Karia atasubiri kuthibitishwa na wajumbe wa mkutano mkuu baada ya kubaki peke yake.

Chanzo: Maulid Kitenge
Nasikia Maulidi K wanamwita Kidoti, kachero ivi n kweli ?!
 
Hivi hii TFF na wenyewe wana utaratibu wa kuwa na mihula au wako namna gani na kama hawana basi huyu Msomali hatatoka anavyoonekana, atakuwa kama Ndolanga.
 
Wallace Karia amekuwa mgombea pekee wa nafasi ya Urais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) baada ya Kamati ya Uchaguzi ya TFF kuwaengua Evans Mgeusa na Hawa Mninga kwa kukosa sifa.

Karia anagombea nafasi hiyo kwa muhula wa pili.

======

Wallace Karia amepita kuwa Mgombea pekee kuelekea kwenye uchaguzi mkuu wa kutafuta viongozi wa Shirikisho la mpira wa Miguu Tanzania TFF.

Wagombea wengine wawili Evans Mgeusa na Hawa mniga hawajafuzu vigezo.

Kwa mujibu wa katiba ya TFF "kama ikitokea mgombea wa Urais amebaki peke yake na amekizi vigezo basi hatopigiwa kura na badala yake ataenda kuthibitishwa na wajumbe wa Mkutano mkuu"

Kwa maana hiyo Wallace Karia atasubiri kuthibitishwa na wajumbe wa mkutano mkuu baada ya kubaki peke yake.

Chanzo: Maulid Kitenge
Ni fedhea kwa Takfa na upumbavu kwa waendeshaji.
Jambo hili Alina afya na mshikamano katika nchi. Mbaya zaidi linafanywa kwa wajinga wenye tamaa za madaraka.
Hafai tena kuongoza taasisi ya kitaifa.
Naomba watanzania lisituzoe ili na tulikemee si tu kwenye taasisi, hata kwenye siasa.
Tujiamini tunapokuwa viongozi na tujipime utendaji wetu kwenye chaguzi
 
Back
Top Bottom