Ronal Reagan
JF-Expert Member
- Nov 4, 2010
- 5,299
- 3,055
Baada ya majina yao kuwa nominated kama wagombea wa nafasi ya Urais TLSL, Tundu na Masha wameanza kupiga kampeni mapema, kampeni zenye mrengo wa kisiasa.
Ni hivi karibuni tu wawili hao wamekua wakitoa kauli zenye mrengo wa kisiasa kuelekea Uchaguzi wa TLS na pia wafuasi na mashabiki wa watu hao wenye mrengo wa siasa za upinzani wakipiga kampeni kwa kuuambia uma kuwa ni zamu sasa ya ukawa kuiongoza TLS kwa kuwa kwa muda mrefu ilikua chini ya makada wa CCM.
TLS kama Bar Association ya Tanganyika ni society ya kitaaluma ambayo hushughulika na maswala muhimu ya mawakili, na sheria.
TLS haina afiliation na chama chochote cha siasa wala haijihusishi na siasa.
TLS sio ngo ya maswala ya kupigania haki za raia.
TLS ni jumuiko la kitaaluma.
Hivyo kwa wagombea hao kuanza kampeni zenye zinazoonesha mrengo flani wa kisiasa ni kukengeuka.
Ili kulinda TLS kamati ya Uchaguzi iwaondoe watajwa mara moja katika orodha ya wanaogombea nafasi ya Urais.
Tulieni hapo hapo hadi Lissu aukwae urais wa TLS ndipo uje/mje tuanze mjadala rasmi.
Mnashangaza sana na kuhuzunisha sana ninyi watu!
Hivi hizi kelele zenu mlizoanza wiki iliyopita ni kutokana tu na our Learned Brother Tundu A. M. Lissu kugombea? Hofu na kihoro chenu sababu yake nini?
Je tulipokuwa tunasema na kupiga kelele dhidi ya ukiukwaji wa waziwazi wa Sheria za Nchi, Taratibu na hata kusiginwa kwa Katiba ya nchi mlikuwa mnadhihaki sasa mlitakaje?
Ni hivi, kipele kinaelekea kumpata mkunaji hivyo tulieni. Tanzania ni yetu sote. Tunaumia tunapoona mnafanya mchezo na mambo muhimu na mustakabali wa nchi yetu.