Kamati ya Siasa ya Wilaya ya Ngara Yatembelea Bunge la Tanzania

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,891
939

MHE. NDAISABA RUHORO ATEMBELEWA BUNGENI NA KAMATI YA SIASA WILAYA YA NGARA

Mbunge wa Jimbo la Ngara Mhe. Ndaisaba George Ruhoro wiki hii aliialika Kamati ya Siasa ya Wilaya ya Ngara chini ya Mwenyekiti wake Mhe. Mwl. Vitalis Ndailagije na Mkuu wa Wilaya ya Ngara Kanali Mathias Julius Kahabi kuhudhuria Mkutano wa 11 wa Bunge la 12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kikao cha 14

Baada ya ziara ya Bungeni Mhe. Ndaisaba aliipeleka Kamati hiyo kwenda kuuona Mji wa Kiserikali Mtumba (Magufuli City) na kupokelewa na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Utumishi na Utawala Bora Ndugu Xavier Daudi

Kamati ilipata nafasi ya kuzungukia Miradi ya Ujenzi wa Miundombinu mbalimbali kuona namna Serikali ya awamu ya sita ya chini ya Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan inavyotekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi

Kamati ilipata wasaa wa kukutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Raisi TAMISEMI Mhe. Angellah Kairuki huku ujumbe wa Kamati ukiwa ni kutoa salamu za Shukrani kwa Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuelekeza fedha zinazoendelea kukamilisha miradi mbali mbali ya Maendeleo Jimboni

Mhe. Waziri alifurahi sana na kuwakaribisha tena wajumbe wa Kamati, na kuwaahidi kuwa Serikali itaendelea kutenga fedha kwaajili ya kukamilisha Miradi ya Maendeleo, ili Wananchi wake waendelee kupata nafuu ya maisha.
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2023-04-29 at 20.38.00.jpeg
    WhatsApp Image 2023-04-29 at 20.38.00.jpeg
    54.5 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2023-04-29 at 20.37.58(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-04-29 at 20.37.58(1).jpeg
    48.1 KB · Views: 4
  • WhatsApp Image 2023-04-29 at 20.37.59(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-04-29 at 20.37.59(1).jpeg
    46.7 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2023-04-29 at 20.37.57.jpeg
    WhatsApp Image 2023-04-29 at 20.37.57.jpeg
    59.9 KB · Views: 4
  • WhatsApp Image 2023-04-29 at 20.38.00(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-04-29 at 20.38.00(1).jpeg
    59.4 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2023-04-29 at 20.38.01.jpeg
    WhatsApp Image 2023-04-29 at 20.38.01.jpeg
    36.7 KB · Views: 4
Back
Top Bottom