Kamati ya siasa ya chama cha mapinduzi mkoa wa simiyu imeomba serikali kuajiri walimu

EKILOZO

Member
Jul 16, 2021
23
34
Kamati ya siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Simiyu, imeiomba serikali kuajiri walimu wengi wa kutosha, ili kukabiliana na ongezeko la wanafunzi watakaoanza masomo yao mapema mwakani.

Ushauri huo umetolewa na Katibu wa CCM mkoa wa Simiyu Innocent Nazaba, wakati wa ziara ya kamati ya siasa ya chama hicho mkoa ilipokagua utekelezaji wa Ilani yake ya uchaguzi ya mwaka 2020 hadi 2025, ambapo pia imeeleza kuridhishwa na ujenzi wa vyumba vya madarasa vinavyojengwa kwa fedha za UVIKO-19 wilaya ya Meatu mkoani humo.
Na kusema kwamba ongezeko la wanafunzi na vyumba vya madarasa vinaasisi pia fursa nyingine ya ajira za walimu.

Chanzo: Eatv
 
Back
Top Bottom