Kamati ya sera ya fedha yaridhishwa na utekelezaji wa sera ya fedha nchini na mwenendo wa ukuaji wa uchumi Tanzania

Getrude Mollel

JF-Expert Member
Apr 26, 2022
259
353
Saa chache zilizopita kupitia kurasa zake katika mitandao ya kijamii, Benki Kuu imetoa taarifa ya Kamati ya sera ya fedha ambayo kazi yake kubwa ni kufanya tathmini ya utekelezaji wa sera ya fedha na mwenendo wa uchumi.

Chini ya Rais Samia Suluhu ukuaji wa uchumi wa Tanzania imeendelea kuimarika na kukua kwa kuridhisha kadiri siku zinavyosonga mbele. Rais Samia Suluhu ana siku 505 tu madarakani, waswahili wanasema nyota njema huonekana asubuhi.

Ripoti hii iliyotoka leo inatoa tathmini ya utekelezaji wa sera ya fedha na mwenendo wa kiuchumi kati ya Mei na Juni 2022.

Huu ni muhtasari tu wa mengi ambayo yameelezwa kwenye ripoti hiyo:

1: Kamati imeridhishwa na utekelezaji wa sera ya fedha ambapo utekelezaji huo umeleta faida zifutatazo
  • Kuongezeka kwa ukwasi kwa mabenki
  • Kuchochea ongezeko la mikopo kwa sekta binafsi
2: Kamati imetamka kwamba mwenendo wa uchumi katika nusu ya kwanza ya mwaka 2022 imeimarika sambamba na matarajio ua ukuaji kwa mwaka 2022 kwa asilimia 4.7% na kwa 5.4% kwa Tanzania Bara na Zanzibar mtawalia.

Mfumuko wa bei uliongezeka kufikia 4.0% na kwa asilimia 4.4% Juni 2022 kutokana na kupanda kwa bei za bidhaa kutoka nje ya nchi.

3: Ujazi wa fedha imeimarika zaidi kulingana na matarajio ya mwaka 2021/22. Ukuaji wa mikopo kwa sekta binafsi umeimarika kwa asilimia 9.9% sanjari na lengo la mwaka 2022/22 huku vyanza vya mapato vikizidi kuongezeka.

Lakini mwisho kamati ilishauri Tanzania kupunguza kasi ya kuongeza ukwasi kwenye uchumi katika nusu ya pili ya mwaka 2022, ili kukabiliana na athari za ongezeko la mfumuko wa bei, bila kuathiri kasi ya ukuaji wa uchumu.

Pia Tanzania imeshauriwa kuongeza akiba ya kutosha ya fedha za kigeni, ili kuendelea kudumisha utulivu wa thamani ya shilingi na kulinda uchumi dhidi ya athari za kuongezeka kwa bei za bidhaa katika soko la dunia.
 
Hajui kuwa miradi mingi imedhoofu au imesimama, bima ya afya hiyo inajaribu kujiotesha manyoya.
 
Napenda mtu akisema kitu awe objective sio subjective. Ukisema miradi mingi useme ni upi na upi halafu useme miradi hiyo iko wapi. Ukiwa hivyo itasaidia zaidi kuonesha namna gani tunaweza kujadili. Ukisema juu juu unaonekana umekaa kishabiki zaidi, basi sio factual. Karibu.
 
Wapitie upya masharti ya uanzishwaji maduka ya kubadilisha fedha ili iende sambamba na ongezeko ukuaji wa biashara ya utalii.
 
Napenda mtu akisema kitu awe objective sio subjective. Ukisema miradi mingi useme ni upi na upi halafu useme miradi hiyo iko wapi. Ukiwa hivyo itasaidia zaidi kuonesha namna gani tunaweza kujadili. Ukisema juu juu unaonekana umekaa kishabiki zaidi, basi sio factual. Karibu.
Hao viongozi wa juu wote hakuna hata mmoja anayewatajia miradi na mahali ilipo kama unavyotaka wewe, ila inajulikana na wafuatiliaji.
Nenda Kilwa Road kaangalie barabara ya mwendo kasi, nenda daraja la Wami Mandera huu ni mwaka wa ngapi!
 
Back
Top Bottom