Synthesizer
JF-Expert Member
- Feb 15, 2010
- 11,143
- 18,774
Baada ya tamko toka Ikulu (sijui kama ni la kweli au fake) kwamba inasikitishwa na azimio la Bunge la kukataa kufanya kazi na CAG, azimio ambalo si tu linaleta mgogoro wa kikatiba, bali pia linamshushia hadhi raisi kwa namna ya kumwambia Bunge linaweza kuingilia mamlaka yake. Bunge limetoa tamko la kumgomea raisi! Labda tujiulize kama Bunge linafanya hivyo kwa kuwa mara kadhaa raisi ameonekana akiingilia mamlaka ya Bunge.
Jambo la pili, inafikia mahali ijulikane wazi kwamba Ndugai amekuwa mkubwa kuliko viatu vyake. Ndugai amekuwa na silka ya kujipa mamlaka kupita kiasi, pamoja na kuwadhalilisha wabunge. Tunakumbuka jinsi alivyotoa mwito wa kumwita CAG kwa namna ya dharau. Tunakumbuka kauli yake ya kebehi kwa Lema.Ndugai amekuwa akiwachukulia wabunge kama mwalimu mkuu na watoto wa shule ya msingi.
Kwa hiyo basi, lazima kamati ya nidhamu ya Bunge, na spika Ndugai, kwa namna moja au nyingine, wawajibishwe kwa walilofanya. Wao wamezoea sana kuwawajibisha watu kwa vitu vidogo visivyo na msingi, na imefika mahali wanyweshwe dawa waliyotengeneza wenyewe!
Ni wazi Bunge lina udhaifu mkubwa, katika utendaji na uongozi.