Kamati ya Ndugai yameguka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kamati ya Ndugai yameguka

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ng'wanza Madaso, Dec 6, 2009.

 1. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #1
  Dec 6, 2009
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Kamati ya Ndugai yameguka

  Na Mwandishi wetu
  6th December 2009

  [​IMG] Yadaiwa wapo wabunge wanaoibeba OBC
  [​IMG] Mlingwa adaiwa kumkoromea Job Ndugai  [​IMG]
  Pori tengefu la Loliondo mkoani Arusha
  Kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira inadaiwa kugawanyika kutokana na baadhi ya wabunge kuonyesha azma ya kulinda maslahi ya mwekezaji katika pori tengefu la Loliondo mkoani Arusha.

  Taarifa za ndani ya kamati hiyo zilizolifikia Nipashe Jumapili, zimebaini kuwepo mgawanyiko huo ambao umetokea tangu wabunge hao walipotembelea ofisi za Ortello Business Corporation (OBC) Limited ya Umoja wa Falme za Nchi za Kiarabu (UAE).

  Kamati hiyo ilitembelea ofisi za OBC Novemba 26, mwaka huu, kisha kuzungumza na wana-vijiji wa maeneo kadhaa yaliyopo Loliondo.

  Akizungumza kwa sharti la kutotajwa jina lake gazetini, mbunge mmoja wa kamati hiyo inayoongozwa na Job Ndugai, alisema baadhi ya wabunge (anawataja), walikuwa na msimamo wa kutotaka OBC ibanwe ili kutoa maelezo ya kina.

  Kwa mujibu wa taarifa hizo, hali hiyo ilizusha malumbano na mzozo kati ya
  Ndugai na Mbunge wa Shinyanga Mjini (CCM), Charles Mlingwa.

  Mzozo kati ya Ndugai na Mlingwa unaelezwa kutokea wakati wajumbe wa kamati hiyo walipotembelea ofisi za OBC zilizopo Loliondo.

  Kwa mujibu wa chanzo hicho cha habari, asili ya mzozo huo ni Mlingwa kupinga hatua ya Ndugai, kuhoji baadhi ya mambo muhimu ambayo yangesaidia utekelezaji wa majukumu yake.

  ''Mlingwa alionyesha kutotaka Ndugai ahoji baadhi ya mambo kwa madai kuwa yalikuwa nje ya uchunguzi kuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu,'' chanzo chetu kilieleza.

  Hata hivyo, alipohojiwa kuhusu mzozo huo baada ya mkutano uliofanyika kijijini Soitsambu, Ndugai alisita kujibu moja kwa moja, kisha akakana kuwepo kwa tukio hilo.

  ''Sisi tunashirikiana vizuri kama kamati na tunaelewana, hilo la kulumbana na Mlingwa niseme tu kwamba halipo,'' alisema.

  Licha ya Ndugai kuukana mzozo huo, taarifa zaidi zinadai kuwepo mashinikizo kadhaa kutoka baadhi ya wajumbe dhidi yake.
  Hata hivyo haikujulikana mara moja mashinikizo hayo yalihusu kitu gani.

  Taarifa hizo zinadai kuwa wabunge wanaoitetea OBC walipanga kuwadhibiti wafugaji wa Kimasai, ili washindwe kueleza kwa ufasaha kuhusu unyanyasaji uliofanywa na askari wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) kwa kushirikiana na maofisa wa kampuni hiyo.

  Hatua hiyo inadaiwa kutekelezwa kwa kuwauliza maswali na kutoa shutuma dhidi yao.

  Miongoni mwa kauli zinazodaiwa kutumiwa kwa lengo la kuilinda OBC ni pale Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Hassan Khatib, alipowataka wafugaji hao kushirikiana na OBC.

  Akihutubia katika mkutano wa hadhara uliofanyika kijijini Oloipili, Khatib alisema maelezo yaliyotolewa kuhusu kijiji hicho kutoathirika na operesheni `choma maboma' iliyofanyika Julai mwaka huu, ilirahisisha utendaji kazi kwa kamati hiyo.

  Kisha akasema, "mmetupa urahisi wa kufanya shughuli yetu kwa makini, tumeiona hali halisi na kamati inalichukua hilo, sasa mshirikiane na OBC ili kupata maendeleo ndani ya kijiji chenu."

  Wakati Khatib akisema hayo, sehemu kubwa ya vijiji vilivyotembelewa na kamati hiyo, ilionyesha kuwepo vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu.

  Ndugai anathibitisha hilo katika maelezo yake kwa waandishi wa habari baada ya kumaliza mkutano wa mwisho wa hadhara katika kijiji cha Soitsambu.

  Mbali na Khatib, kauli ya Mlingwa na hatua ya kuwashutumu wafugaji hao kwa madai kuwa wanatumika kwa maslahi ya watu wachache, inachukuliwa kama kielelezo cha ukiukwaji wa kanuni zinazoongoza mchakato wa uchunguzi huo.

  Mlingwa alisema hayo katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kijiji cha Ololosokwani, ambacho ni miongoni mwa maeneo yaliyoathiriwa na `choma maboma' iliyofanyika.

  Mlingwa akasema inashangaza kuona kuwa wafugaji hao wanailalamikia OBC inayomilikiwa na Mwarabu, huku wakiunga mkono kampuni ya Klein's camp ambayo ni mali ya wazungu.

  Mbunge huyo aliyewahi kuwa Naibu Waziri wa Mifugo akasema kijiji hicho kilikosea kufuta makubaliano kati yake na kampuni ya Tanzania Cattle Product iliyokusudia kulitumia eneo hilo kwa shughuli za shamba la mifugo, badala yake kulikabidhi kwa Kleins's camp.

  "Niseme wazi...mlikubali kumtetea mzungu ambaye si mtanzania lakini huyu mwarabu hajawanyang'anya ardhi anakuwa mbaya wenu...nimeongea kwa uchungu, mnapotoshwa na watu wachache, sisi wabunge hatuwezi kukubali wananchi kupotoshwa kama mlivyopotoshwa," akasema.

  Mjumbe mwingine wa kamati hiyo anaikosoa kauli ya Mlingwa, kwa madai kuwa inatoa hukumu kabla ya kuwasilishwa kwa ripoti ya mwisho bungeni.

  ''Huu si uadilifu, inaonekana kama hatuwatendei haki hawa wafugaji maana kila wanachokisema, kinapingwa ama kuhojiwa kwa nguvu kubwa na wenzetu...ndio maana mimi siongei,'' anasema mjumbe mwingine.

  Aliyekuwa Mwenyekiti wa kijiji cha Ololosokwani wakati wa mabadiliko hayo, Julius Kaura, ni miongoni mwa wafugaji waliopata ujasiri wa kueleza usahihi wa mkanganyiko ulioibuliwa na Mlingwa.

  Kaura akasema kampuni ya Tanzania Cattle Product iliyotetewa na Mlingwa, ilikiuka makubaliano, hali iliyochagiza kijiji hicho kushinda kesi iliyohusiana na kuvunjwa kwa makubaliano hayo.

  Alisema awali Tanzania Cattle Product ilitakiwa kuanzisha shamba la mifugo, badala yake ikaibua mradi wa ujenzi wa hoteli.

  Kuhusu uchomaji moto maboma, Kaura alisema tukio hilo lilitokana na amri halali ya Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Elias Wawa-Lali kutaka raia wa Kenya waliovamia eneo hilo kuondoka na kila mkazi kukaa katika eneo lake la asili. Kauli ya Kaura inachukuliwa na wachambuzi wa masuala yanayohusiana na mzozo uliopo Loliondo kuwa pigo kwa Mlingwa.
  '
  'Unaona athari za kutoa kauli zisizokuwa na ukweli, sasa Mbunge anakosolewa na Mwenyekiti wa kijiji...lazima tuwe kamini,'' anasema Mbunge mmoja wa viti aliyepo katika kamati hiyo.

  Mbali na kauli hiyo, baadhi ya wabunge wanadaiwa kuonyesha ishara mbalimbali zilizoashiria kumuunga mkono mwekezaji huyo.

  Mathalani, inadaiwa kuwa kuna wakati Mbunge wa Viti Maalum, Khadija Saleh Ngozi, alibainika akipiga makofi kama ishara ya kushangilia hoja zilizotolewa kwa maslahi ya OBC.

  Picha kadhaa zimeonyesha Ngozi akipiga makofi pale wakazi wa kijiji cha Soitsambu walipojitokeza katika hatua za mwisho kabla ya kufungwa mkutano, wakiipongeza OBC.

  Kitendo hicho kinatafsiriwa kama sehemu ya kuunga mkono mkakati wa kuhakikisha kuwa OBC inawekwa pembeni mwa shutuma zilizotolewa na Mbunge wa Ngorongoro, Kaika Ole Telele.

  Pia kauli za Ngozi kama vile kuwataka waandishi wa habari kutoa kipaumbele kwa taarifa zilizoshindwa kuthibitishwa na baadhi ya wanavijiji, zikiwemo za ubakaji unaodaiwa kufanyika wakati wa operesheni hiyo, zinaelezwa kuwa miongoni mwa viasharia vya `kuikingia kifua' OBC.
  akanuni na taratibu za Bunge.

  Anakiri kwa waandishi wa habari katika kijiji cha Soitsambu, kuwa vitendo kadhaa vinavyoashirikia ukiukwaji wa haki za binadamu vilidhihirika huko Loliondo.

  Lakini anasema viwango vya ukiukwaji huo vitaanishwa katika ripoti itakayowasilishwa bungeni mwanzoni mwa Februari mwakani.

  Anasema hayo yalidhihirika katika mikutano ya hadhara na kukutana na jumuiya mbalimbali ikiwemo kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Arusha.

  Pia kamati hiyo, kwa mujibu wa Ndugai ilikutana na viongozi wa OBC.

  "Kuna mambo mengi tumeyabaini, lakini lililojionyesha dhahiri ni baadhi ya vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu, hili si jambo jema lakini hayo yatafafanuliwa zaidi katika taarifa rasmi tutakayoitoa bungeni mwanzoni mwa Februari mwakani," anasema.


  CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
   
Loading...