kamati ya Nchimbi kuchunguza mauaji ya Mwangosi yatua NYololo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

kamati ya Nchimbi kuchunguza mauaji ya Mwangosi yatua NYololo

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by nkisumuno, Sep 13, 2012.

 1. n

  nkisumuno JF-Expert Member

  #1
  Sep 13, 2012
  Joined: May 22, 2012
  Messages: 209
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Tangu mchana kuanzia saa 6:30 hadi jioni ya leo kamati hiyo imeendelea na mahojiano na makundi tofauti matatu, ilianza na serikali ya kijiji tangu saa 6:45 hadi saa 9:30 imekaa na serikali ya kijiji. Nimehudhuria kikao hicho kama mjumbe mwalikwa. baada ya hapo imekaa na viongozi wa madhehebu ya dini. Jioni hii inatarajiwa kukaa na viongozi wa vyama vya siasa.

  yaliyojiri

  Mimi nimehudhuria mahojiano ya serikali ya kijiji na kamati hiyo. Katika mahojiano hayo nimegundua kuwa wajumbe waliowengi ukiondoa wachache ambao wamekuwa wakweli wengi wao walionyesha uoga na kusema huku wakijipendekeza kwa serikali na kukilaumu CHADEMA kwa kufanya mkutano pasipo kibali lawama kidogo kwa polisi.

  Katika wote waliopata nafasi kuna watu wawili ambao walionekana kuikuna tume hiyo pale tume ilipowaomba wjumbe wapendekeze nini kifanyike. Mwalimu mmoja alisimama na kuomba elimu ya uraia itolewe katika jamii ya Kitanzania ili watu waelewe kwa nini vyama vya siasa vipo, mikutano ya siasa ina maana gani, haki ya maandamano, haki za raia na wajibu wao viwe wazi. Alisema kwa kijijini kama hapa Nyololo wapo watu ambao bado wana dhana kuwa ukiwa upinzani wewe ni adui, akibainisha hoja yake hiyo alisema hata hapa miongoni mwa wajumbe bado wanaongea kwa woga mbele ya tume na kujipendekeza kwa tume ili waonekane ni waaminifu kwa serikali.Aidha mwalimu huyo ameshangazwa sana na nguvu ya polisi iliyotumika kwa kuwa na defender zaid ya sita wakati hapa ni kijijini.

  Akiwageukia askari alisema anashangazwa na kuuwa kwa mwandishi jambo ambalo amehoji kama alikuwa anakosa si angepelekwa mahakamani. Aidha amehoji kwa baadhi ya wajumbe waliosema wanachama wa CHADEMA walisababisha fujo yeye kahoji iweje auawe Mwangosi na si mfuasi wa Chadema? Akaulizwa unajuaje kama hakuwa mpenzi wa Chadema? Akajibu hata kama angekuwa anaipenda Chadema bado hakustahili kuuawa ikizingatiwa kuwa alikuwa kazini.

  Mzee mwingine mstaafu alionyesha umahili wake pale alipoikumbusha kamati hiyo baadhi ya kesi ikiwemo ya Kombe, Kesi ya mbwa ya rukwa pale mtu aliyeng'atwa na mbwa na kumfanya amuue. kesi ambayo ilionekana yule mbwa hakuwa na makosa kwani alimng'ata akiwa kazini hivyo yule aliyeua ndo alikuwa na kosa. Akilinganisha na kesi hiyo alsema hata kama Chadema walifanya mkutano pasipo kibali mwandishi aliuawa kimakosa kwani alikuwa kazini kwake. Ndipo alipoulizwa kwani polisi hawakuwa kazini? Amejibu hata kama walikuwa kazini hakuna mahali ambapo polisi wanaruhusiwa kuua. Jaji alilazimika kutolea ufafanuzi wa baadhi ya kesi kutokana na mzee huyo kuonyesha uelewa wa hali ya juu kwenye maswala ya kisheria japo si mwanasheria bali mhasibu mstaafu.

  Kikao kinaendelea na sasa ni viongozi wa dini kisha Vyama vya siasa nitaendelea kuwajulisha kilichojili mimi nimetoka kwenye kikao cha kwanza lakini update nitazipata kwa vijana wangu.
   
 2. N

  Nguto JF-Expert Member

  #2
  Sep 14, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,660
  Likes Received: 635
  Trophy Points: 280
  Serikali yetu inapoteza bure tu hela za walipa kodi. Kwani wanachunguza nini na wote tumeona ushahidi uliowekwa wazi kuwa polisi ndio wameua? Isitoshe si wamefungua kesi sasa hiyo tume a.k.a. kamati inachunguza nini?? Nchi hii bwana!!!
   
 3. N

  Nguto JF-Expert Member

  #3
  Sep 14, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,660
  Likes Received: 635
  Trophy Points: 280
  Hivi jaji ndio anaongoza hiyo tume a.k.a kamati? Huyo jaji hajui kuwa sheri inakataza polisi kutumia nguvu kubwa hadi ikasababisha vifo isipokuwa kama alikuwa anajihami (self defence)? Kwanini jaji mzima anakuwa mwoga? Alitakiwa amwelimishe hii sheria waziri wake aliyemteua. Kwa kumfungulia kesi muuaji (kama kweli ndiye) hiyo tume a.k.a kamati ni "null and void"!!
   
Loading...