Kamati ya Nchimbi Inaingilia Uhuru wa Mahakama | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kamati ya Nchimbi Inaingilia Uhuru wa Mahakama

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Communist, Sep 13, 2012.

 1. Communist

  Communist JF-Expert Member

  #1
  Sep 13, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 5,391
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Tayari katika vyombo mbalimbali vya habari, tumepata taarifa ya kufunguliwa kesi ya mauaji ya Iringa.

  Vilevile inaonyesha Waziri chimbi jana ametoa waraka unaelezea tuhuma za mlalamikiwa. Sasa kama

  hata Bunge letu tukufu huwa haliruhusiwi kuzungumzia suala lililo mahakamani, inakuwaje basi hii tume

  ya Nchimbi, kuhusu suala hilo hilo iendelee kufanya kazi ambayo mahakama inaifanya. Ina maana Waziri

  hana imani na mahakama? Je hapa huu muhimili mkuu katika ile mihimili mitatu hauingiliwi kiutendaji?

  Naomba wataalamu na Thinkers mnisaidie hapa naona kama kuna tatizo.

  Nawakilisha.

  [​IMG]
  Nafikiri mahakama inaweza kutumia vielelezo vilivyopo na ikamliza hii kazi, hizo pesa za kamati zipelekwe mahakamani


  Katiba:
  107B. Katika kutekeleza mamlaka ya utoaji haki, mahakama zote zitakuwa huru na zitalazimika kuzingatia tu masharti ya
  Katiba na yale ya sheria za nchi.

  Na hii jee haingilii uhuru wa mahakama
  [​IMG]
   
 2. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #2
  Sep 13, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Pengine ndio maana wakaita ni kamati.

  Labda hii kamati inaangalia tu kwanini fujo zilitokea bila kuangalia issue ya Mwangosi.

  Ila kimsingi hii kamati haitakiwi kuwepo.
   
 3. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #3
  Sep 13, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Na amemuamuru DPP(na sio DCI) kumfungulia mashtaka huyo askari.....hii si kazi yake!
   
 4. Communist

  Communist JF-Expert Member

  #4
  Sep 13, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 5,391
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Hebu funguka zaidi, unajua sisi wengine hii JF ndio shule yetu. Hebu weka ufafanuzi kidogo tu.
   
 5. m

  mezanane Member

  #5
  Sep 13, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 88
  Likes Received: 79
  Trophy Points: 25
  Its obvious Kamati inaingilia uhuru wa Mahakama. Lakini nadhani serikali ina hahaha kwani ukiangalia kuna vitu vinakinzana:-

  1. Kwanza Mwanzo taarifa ya kwanza ya polisi ilisema Mwongosi amepigwa na kitu cha ncha kali kutoka upande waliokuwa wananchi au wafuasi wa chadema
  2. Picha zilipotoka kuonyesha hali halisi ya tukio hii story ikapotezewa na wakakurupukua kuunda Kamati
  3. Kamati imeundwa lakini imepingwa vikali kutokana na composition yake wakaamua wapeleke Mahakamani

  Maswali ya kujiiuliza yote hayo matatu yanafanywa na serikali hiyo hiyo na ni dhahiri yanaoshesha hali ya kutokuwa na maamuzi dhabiti kama si kupagawa na kuwa katika "state of fear". Kwa mtizamo wangu Kamati kwa vile imeundwa na serikali ilipaswa kumaliza kazi yake na ndipo hatua za kisheria zifuatwe kama ingependekezwa hivyo. Hili lilifanyika wakati wa Zombe pia. Lakini Kamati na Mahakama haviwezi kufanya kazi kwa pamoja hata kidogo. Kisheria Kamati sasa haina kazi tena maana mambo yapo mahakamani na Kamati haina tena Mamlaka ya kufanya shughuli hiyo....
   
 6. Communist

  Communist JF-Expert Member

  #6
  Sep 13, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 5,391
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Kwa kifupi naona kama Nhe Dr Nchimbi anachanganya sana mambo hapa. Labada angebaki kuwa mbunge tu ingetosha. Hii wizara inatakwa kichwa.
   
 7. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #7
  Sep 13, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Mmmmmm mbona hii sasa imekuwa kizungumkuti. Waziri atapona kweli.
   
 8. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #8
  Sep 13, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Mbona hatuwaoni kusema na kuyashikia bango ya Ally kijana muuza magazeti wa Morogoro? Jee, ni ubaguzi au maslahi ya kisiasa?
   
 9. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #9
  Sep 13, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  ASKARI polisi aliyefyatu bomu lililomlipua na kumuua kinyama mwandishi wa habari wa Kituo cha Televisheni cha Channel Ten, David Mwangosi (40), amefikishwa katika mahakama ya kijeshi na kuvuliwa uaskari.

  Vile vile, askari huyo mwenye cheo cha PC anatarajiwa kufikishwa
  katika mahakama za kiraia kujibu mashitaka yanayomkabili.

  Habari kutoka ndani ya jeshi hilo mkoani Iringa zilimtaja askari huyo kuwa ni PC Pacificus Cleophace Simon (23), mwenye namba G2372. Ni askari wa FFU Iringa, na hajafikisha miaka mitatu kazini.
   
 10. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #10
  Sep 13, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Soma hapa labda utafunguka mkuu

  Anayedaiwa kumuua Mwangosi kizimbani
   
 11. Communist

  Communist JF-Expert Member

  #11
  Sep 13, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 5,391
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Huyo Ally ndio angeundiwa tume maana hii ya kwake haijafika mahakamani. Labda wabadilishe hadidu za rejea, ili hii tume kamati iwe ya Ally Zonna.

  Naunga mkono hoja 75%
   
 12. Communist

  Communist JF-Expert Member

  #12
  Sep 13, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 5,391
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
 13. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #13
  Sep 13, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Jana ulibishia sana ombi la Dr Slaa kwa Rais kuunda tume maalum kuchunguza mauwaji yote yanayohusihwa na Polisi yaliyowahi kutokea nchini. Leo vipi tena?
   
 14. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #14
  Sep 13, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Ally ameundiwa tume na maaskari wameshikwa, cha kushangaza hakuna aneshikilia bango wala kuongelea hilo. Jee, ni ubaguzi au maslahi ya kisiasa?
   
 15. Communist

  Communist JF-Expert Member

  #15
  Sep 13, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 5,391
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Huyu jamaa anajiita system at work, Hii system yake Duhhh, ime-corrupt atafute antivirus.
   
 16. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #16
  Sep 13, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
 17. Communist

  Communist JF-Expert Member

  #17
  Sep 13, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 5,391
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Funguka zaidi, nani kashikwa. Maana sijaona hizo taarifa. Isije ikawa changa la macho la system
   
 18. F

  FJM JF-Expert Member

  #18
  Sep 13, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Serikali ina wajibu wa kulinda raia wote regardless mtu anafanya nini au ana cheo gani. Ally Zona aliuwawa kabla ya Daudi Mwangosi. Nchimbi anaweza kuumbia umma ofisi yake imefikia wapi kuhusiana na kifo hicho cha Ally?
   
 19. james chapacha

  james chapacha JF-Expert Member

  #19
  Sep 13, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 942
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  swala la Ally lipo mahakamani,na si la Ally tu,kuna Dr.Ulimboka,yule mbunge wa ccm aliyepokea mlungula,EPA,nk.mambo nimengi tumeacha kuyazungumzia kwasababu kesi zake zipo mahakamani.
   
 20. Communist

  Communist JF-Expert Member

  #20
  Sep 13, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 5,391
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Atoe waraka mwingine, Kuhusu Ally Zonna, Sijui ataogopa?
   
Loading...