Kamati ya Mwakyembe si ilitoa ushauri Hosea afukuzwe kazi? Kulikoni? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kamati ya Mwakyembe si ilitoa ushauri Hosea afukuzwe kazi? Kulikoni?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Jul 26, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Jul 26, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,408
  Likes Received: 81,440
  Trophy Points: 280
  Date::7/25/2009
  Dk Hoseah aonywa, Karamagi, Msabaha bado wachunguzwa

  Na Kizitto Noya, Dodoma
  Mwananchi

  SERIKALI imempa onyo Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru), Dk Edward Hoseah kwa kutokuwa makini katika utendaji wake wa kazi wakati anachunguza mkataba tata kati ya kampuni ya Richmond na Tanesco.

  Hata hivyo, serikali imesema mamlaka yake (Hoseah) ya nidhamu imeona hana hatia kijinai kwani sheria ya Takukuru wakati huo, ilikuwa na mapungufu katika kubaini viashiria vya rushwa kwenye mchakato wa zabuni.

  Akiwasilisha bungeni taarifa ya utekelezaji wa maazimio ya Bunge kuhusu sakata hilo, Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Adam Malima alisema Dk Hoseah alipaswa kujiridhisha kama kweli kampuni ya Richmond Development Company (LLC) ilisajiliwa nchini au la kabla hajatoa taarifa yake kwa umma.

  "Ingawa sheria ilikuwa na mapungufu, mamlaka yake ya nidhamu imebaini kuwa wakati wa kupitia taarifa ya uchunguzi iliyofanywa na wataalamu wake wa Takukuru na kabla hajaitoa kwa umma, alipaswa kujiridhisha kwamba kweli kampuni ya Richmond Development Company (LLC) ilikuwa imeandikishwa hapa nchini au hapana.

  "Hivyo mamlaka iliamua apewe onyo kwa kutokuwa makini katika uchambuzi wa taarifa zinazowasilishwa kwake na wataalamu wake, ili kuleta usimamizi wenye tija ndani ya Takukuru."

  Lakini serikali imesema bado haina majibu ya maazimio namba nane na 14 ya Bunge yaliyoitaka iwawajibishe viongozi wenye dhamana ya kisiasa waliokuwa mawaziri Dk Ibrahim Msabaha na Nazir Karamagi kwa kuwa uchunguzi dhidi yao haujakamilika.

  "…Hadi sasa suala hilo halijafikia tamati kwa kuwa linashughulikiwa zaidi na Takukuru na ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka," alisema Malima.


  Mbali na Dk Hoseah watumishi wengine wa umma waliohusika na mkataba huo wamesafishwa kuwa hawakutenda kosa lolote la jinai.

  Miongoni mwa watumishi hao ni Mwanasheria Mkuu wa serikali, Johnson Mwanyika ambaye amesafishwa kwamba hakuna ushahidi unaodhihirisha kuwa hawakutumia utaalamu na uzoefu wake kuishauri vizuri serikali katika mchakato mzima wa upatikanaji wa zabuni hiyo.

  "Kwa mantiki hiyo, Mamlaka zao za nidhamu zimeridhika na utetezi uliotolewa na watumishi hao na kuwaondolea mashtaka. Hata hivyo watumishi hao wamekumbushwa kuhusu umuhimu wa kuwa makini na thabiti zaidi katika utekelezaji wa majukumu wanayopewa na serikali," ilisema.

  Mwanyika ambaye mamlaka yake ya nidhamu ni Rais, taarifa hiyo ilisema, hakuwa na kosa lolote katika mchakato mzima wa kuipa kampuni ya Richmond zabuni ya kuzalisha umeme.

  "…Kwa maelezo tuliyonayo, hakuna kosa lolote la kisheria au kinidhamu ambalo alilifanya katika nafasi yake kama mwanasheria mkuu wa serikali katika mchakato mzima ulioipa ushindi kampuni ya Richmond Development Company LLC Development Company kisheria au kinidhamu," ilisema.

  Hata hivyo, Malima alisema kwa kuwa kuna shauri mahakamani dhidi ya wamiliki na wawakilishi wa Richmond, iwapo mtumishi yeyote wa umma atatajwa na watuhumiwa hao kwamba alihusika katika makosa ya jinai, serikali haitasita kumfikisha mahakamani.

  Alisema serikali imetekeleza Azimio namba 11 lililoitaka ifanyie marekebisho ya sheria ya maadili ya viongozi wa umma kwa kuunda kikundi kazi ambacho tayari kimefanya utafiti na kupitia upya sheria hiyo ya mwaka 1995 kubaini mapungufu yake.

  Serikali pia imetekeleza azimo la 12 lililoitaka ijiepushe na matumizi ya mawakala katika manunuzi ya umma kwa kukamilisha utaratibu mpya wa manunuzi ya umma chini ya usimamizi wa Mamlaka ya Manunuzi ya Umma (PPRA).

  Katika hatua nyingine serikali imetekeleza Azimio namba 13 lililoitaka isizihusishe Kamati za Bunge kupitia mikataba mikubwa ya kibiashara na ya muda mrefu kwa kuunda timu ya wataalamu ambao wanaandaa utaratibu mwafaka kwa kufanya utafiti katika mabunge ya nchi za Jumuiya za Madola.

  Katika kutekeleza maazimio namba 18 na 20, serikali iliunda kamati maalumu ya vyombo vya dola kushughulikia uchunguzi na upelelezi na kumfikisha mahakamani mmoja wa wawakilishi wa Richmond LLC, Naeem Adam Gire.

  Hii ni mara ya nne kwa serikali kutoa taarifa inayohusu suala la Richmond, taarifa ya kwanza iliwasilishwa Aprili 25 mwaka 2008, ya pili Agosti 28 mwaka jana na taarifa ya tatu Februari 11 mwaka huu.
   
 2. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #2
  Jul 26, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,546
  Likes Received: 18,204
  Trophy Points: 280
  Asante BAK.
  Utekelezaji huu ni mzuri sana maana umekaa kisanii kama mchezo wa kuigiza ya aina ya true life drama.
  Nilipoisoma ile barua ya Hosea kwenye kamati ya Mwakiembe, niligundua straight away sio Hosea, ni mkulu mwenyewe, Mwakiembe hakuliona hilo, eti anatumia azimio la Bunge kumtaka mkulu amuwajibishe kijana mpendwa wake anayependezwa nae!.
  Huu ndio utekezaji wenyewe.
   
 3. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #3
  Jul 26, 2009
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  And we keep on saying serikali ya awamu ya nne chini ya JK ipo seriaz na suala zima la rushwa. Anywayz watanzania tusikate tamaa history is on our side.
   
 4. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #4
  Jul 26, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  na huyu EDDO?.........is he exempted?
   
 5. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #5
  Jul 26, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Usiende kinyume na title ya thread: Kamati ya Mwakyembe ilitoa ushauri! Unajua maana ya neno 'ushauri?'
   
 6. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #6
  Jul 26, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Mauza uza haya mie niliyategemea ndiyo maana nikawa naendelea na Kilimo tu kwa nguvu zangu hakuna cha kupambana na rushwa bali ni kukuza ulaji
   
 7. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #7
  Jul 26, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Kamati ya Mwakyembe ilitoa maoni na sio maamuzi!
   
 8. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #8
  Jul 27, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,408
  Likes Received: 81,440
  Trophy Points: 280
  Richmond yalivuruga Bunge
  • Taarifa ya serikali bungeni yaibua mambo mapya


  na Mwandishi Wetu
  Tanzania Daima
  Sauti ya Watu

  [​IMG]
  SIKU moja baada ya Bunge kuwasilisha taarifa ya utekelezaji ya maazimio ya Bunge kuhusu hatua zilizochukuliwa dhidi ya waliohusika kuingia mkataba kati ya Shirika la Umeme nchini (TANESCO) na Kampuni ya kufua umeme wa dharura ya Richmond Development (LLC), maoni mbalimbali yametolewa huku baadhi wakieleza kutoridhishwa na hatua hiyo.

  Moja ya kundi lililoonyesha kutoridhishwa na hatua hiyo ya serikali ni wajumbe wa kamati teule ya Bunge, iliyopewa jukumu la kuchunguza kashfa ya Richmond, chini ya Mbunge wa Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe.

  Akizungumza na Tanzania Daima kwa njia ya simu kutoka mjini Dodoma, mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo, Mbunge wa Nzega, Lucas Selelii (CCM), alisema kamati yake haijaridhishwa na hatua hizo na kwamba inajiandaa kutoa taarifa nzito bungeni.

  "Bado hatujaisoma taarifa hiyo, lakini kwa haraka nasema hatujaridhika na imetushangaza sana, kwa sasa tuko kikaoni kuijadili taarifa hiyo kwa kina na tutatangaza msimamo wa kamati yetu kuhusu suala hilo," alisema Selelii.
  Kwa upande wake, Mbunge wa Kigoma, Kaskazini, Zitto Kabwe, (CHADEMA), alisema taarifa hiyo ya serikali ya utekelezaji wa mapendekezo ya Bunge, imeonyesha mgongano wa wazi na mkubwa kati ya Bunge na Serikali.
  Alisema wakati Bunge lilitoa mapendekezo ya hatua za kuchukuliwa waliohusika na sakata hili, serikali imekuja na taarifa ambayo inaonyesha dhahiri kwamba watendaji wake hawakuwa na kosa.

  Alisema ili suala la kashfa ya Richmond limalizwe, anakusudia kuja na hoja binafsi wiki hii kuliomba Bunge limruhusu rais aunde tume huru ya majaji itakayoongozwa na Jaji Mkuu, ili ipitie taarifa ya mchakato mzima wa manunuzi ya mitambo ya Richmond, taarifa ya kamati ya Dk. Mwakyembe na taarifa ya serikali ya utekelezaji wa maazimio ya Bunge na kutolea uamuzi.

  "Nimeisoma taarifa ya serikali ya jana, nimeona kuna mkanganyiko mkubwa kati ya Bunge na Serikali, Bunge baada ya kupitia ripoti ya Mwakyembe, lilitoa maelezo na mapendezo ya watumishi wanaopaswa kuwajibishwa, leo serikali imetoa taarifa kuwatetea watumishi wake. Lazima kuwe na chombo kingine kuangalia mgongano huo.
  "Hivyo wiki hii nakusudia kuwasilisha hoja binafsi bungeni ili iundwe tume huru ya majaji kupitia ripoti, kuanzia mchakato mzima wa manunuzi, ripoti ya Mwakyembe na hii taarifa ya serikali ya utekelezaji wa maazimio ya Bunge na waliotuhumiwa wawe na uhuru wa kupeleka mashahidi wao.

  "Vinginevyo wabunge tutaendelea kubishana na serikali kwamba sisi tuko sahihi na serikali nayo itasema iko sahihi kuchukua hatua hizo. Nitamwomba rais aunde tume huru ya majaji na hili linawezekana, kwani hata wenzetu Kenya walifanya hivi na hapo ndipo utakuwa mwisho wa sakata la Richmond," alisema Zitto.

  Akitoa maoni yake kuhusiana na taarifa hiyo, Mbunge wa Simanjiro, Christopher ole Sendeka (CCM), alisema hajaisoma ripoti hiyo lakini ana hamu kubwa ya kujua yaliyomo ndani yake.
  "Ikiwa nilichokisoma kwenye vyombo vya habari kwamba Dk. Hosea na Mwanasheria Mkuu Mwanyika, wamepewa onyo tu bila hatua nyingine, safari hii bungeni hapatatosha kweli," alisema Ole Sendeka.

  Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, katika mahojiano yake na Tanzania Daima jana, alisema anashangazwa na hatua hizo, kwani hazionyeshi kama kuna kosa katika uingiaji wa mkataba wa kampuni hiyo iliyokuwa gumzo nchini.

  "Mimi nashangaa jinsi serikali ilivyolishughulikia suala hili, ni kama vile hakuna aliyekosea, hii imenishangaza sana," alisema Profesa Lipumba ambaye alisisitiza kutokubaliana na hatua hiyo.
  Alisema taarifa hiyo ya serikali, imeonyesha ni kwa jinsi gani serikali isivyo na nia ya kukabiliana na vita dhidi ya ufisadi, kwani kinachofanyika sasa ni kuwaghilibu Watanzania waone kama serikali imedhamiria kupambana na ufisadi.

  "Namwonea huruma ndugu yangu Mwakyembe na kamati yake teule ya Bunge, wamefanya kazi kubwa, lakini haina maana na kibaya zaidi, wamejipalia makaa na wanaonekana wabaya mbele ya wote waliowachunguza, hii ni mbaya sana," alisema Profesa Lipumba.

  Mwenyekiti huyo wa CUF, aliwataka wabunge wote kutokubaliana na hatua zilizochukuliwa na serikali dhidi ya wahusika wa sakata hilo, kwani hazionyeshi dhamira ya kweli ya taifa kutaka kupambana na ufisadi.
  Ripoti hiyo iliwasilishwa bungeni juzi na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Adam Malima, kwa niaba ya Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja.
  Pamoja na mambo mengine, ripoti hiyo imemsafisha Mwanasheria Mkuu, Johnson Mwanyika na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Dk. Edward Hosea. Dk. Hosea, ameonywa kwa kutokuwa makini wakati akifanya uchunguzi wa mchakato uliofanikisha kuipa zabuni ya kuzalisha umeme wa dharura Kampuni ya Richmond Development (LLC).

  Mbali na Dk. Hosea, mwingine aliyeonywa ni aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya majadiliano ya wataalamu, Singi Madata.
  "Hata hivyo ingawa sheria ilikuwa na upungufu kwa upande mmoja, mamlaka yake ya nidhamu imebaini kuwa wakati wa kupitia taarifa ya uchunguzi uliofanywa na wataalamu wake wa TAKUKURU na kabla ya kuitoa kwa umma, alipaswa kujiridhisha kwamba kweli Kampuni ya Richmond Development LLC ilikuwa imeandikishwa hapa nchini au hapana," alisema Malima.
  Kwa mujibu wa serikali, taarifa ya Dk. Hosea haikuonyesha bayana tofauti baina ya Kampuni ya Richmond Development (LLC), RDEVO na Richmond Development Company (RDC), jambo ambalo lilijitokeza baadaye wakati kamati teule ya Bunge ilipofanya uchunguzi wake.
  Kuhusu Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambaye mamlaka yake ya nidhamu ni Mheshimiwa Rais, taarifa hiyo ilisema hakuna kosa lolote la kisheria au kinidhamu ambalo alilifanya katika nafasi yake kama Mwanasheria Mkuu wa Serikali, katika mchakato mzima ulioipa ushindi kampuni hiyo ya LLC katika zabuni ya kuzalisha umeme wa dharura.
  Kuhusu watumishi wa umma waliohusika katika majadiliano ya mchakato mzima wa mkataba huo, serikali imewawajibisha watendaji wake, wakiwamo maofisa waandamizi ambao ni aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi, Gray Mgonja na Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, waliofunguliwa mashitaka ya nidhamu kwa mujibu wa kanuni namba 49(1) ya sheria ya utumishi wa umma ya mwaka 2002.
  Serikali iliongeza kuwa vilevile watumishi waliofanya uchunguzi kuhusu suala hilo walifunguliwa mashitaka ya nidhamu kwa mujibu wa sheria ya utumishi wa umma ya mwaka 2002, na kuwa watumishi hao waliwasilisha utetezi wao kwa mamlaka zao za nidhamu.
  Kuhusu azimio namba nane na 14 la Bunge kutaka serikali kuwawajibisha viongozi wenye dhamana ya kisiasa waliokuwa mawaziri wa Wizara ya Nishati na Madini, Dk. Ibrahim Msabaha na Nazir Karamagi, taarifa hiyo ilisema kama ilivyoelezwa katika mkutano wa 18 wa Bunge kwamba vyombo vya dola vimekuwa vikiendelea na uchunguzi wake kuhusu suala hilo.
  Kwa mujibu wa taarifa hiyo, hadi sasa suala hilo halijafikia tamati, kwa kuwa linashughulikiwa zaidi na taasisi ya TAKUKURU pamoja na Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka nchini, DPP.
  Sakata la Kampuni ya Richmond, lilifanya Bunge kuunda kamati teule, chini ya Mbunge wa Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe (CCM), kuchunguza mchakato wa utoaji wa zabuni kwa kampuni hiyo iliyokuwa ikilipwa sh milioni 152 kwa siku, huku ikidaiwa kutokuwa na uwezo wa kuzalisha umeme kama mkataba wake ulivyobainishwa.
  Taarifa ya Dk. Mwakyembe, iliwahusisha watendaji kadhaa wa serikali, akiwamo aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, ambaye aliamua kujiuzulu. Hata hivyo jina la Lowassa halikuwa miongoni mwa watendaji waliopendekezwa kuchukuliwa hatua.
  Mbali na Lowassa, mawaziri wengine waliojiuzulu ni Nazir Karamagi (Nishati na Madini) na Ibrahim Msabaha (Ushirikiano wa Afrika Mashariki).
  Agosti mwaka jana, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alitoa taarifa ya serikali bungeni kuhusu utekelezaji wa mapendekezo yaliyotolewa na kamati ya Dk. Mwakyembe, ambapo alisema baadhi ya watumishi waliandikiwa barua za kujieleza.
  Kwa mjibu wa Pinda, walioandika barua za kujieleza ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Arthur Mwakapugi na Mkurugenzi wa TAKUKURU, Dk. Hosea.
  Alisema Karamagi na Dk. Msabaha wanaendelea kuchunguzwa na taarifa iliyotolewa na serikali juzi, imeeleza kuwa bado wanachunguzwa, ikiwa ni takriban mwaka mmoja sasa.
  Kuhusu Mwanyika, Pinda laisema suala lake limekabidhiwa kwa Ofisi ya Rais Ikulu, ili kuona ni jinsi gani wataweza kumchukulia hatua za kisheria kama itaridhika kuwa alihusika katika sakata hilo. Aliwaambia wabunge kuwa baadhi ya maazimio yanaendelea kufanyiwa kazi kadiri inavyowezekana.
   
 9. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #9
  Jul 27, 2009
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Season 5 Episode 1
   
 10. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #10
  Jul 27, 2009
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Mchango wango:-

  1. Bunge lazima lielewe role yake ni kupendekeza aka kushauri! katiba inasema hivyo, sio polisi wala kuamrisha.
  2. Ninasikitishwa na wajumbe wa iliyokuwa kamati ya Mwakyembe kuendelea kushikilia as if hiyo kamati ni ya kudumu. Kamati hiyo ilishavunjika siku ile ilivyokabidhi ripoti yake.
   
 11. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #11
  Jul 27, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,098
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  lazima washikilie kaka kwani jambo lile limewapa sifa kama kamati ya kudumu.

  ninapata uelewa mzuri kuwa kamati ile ilimwihitaji fulani afaidhaishwee sanaaa...

  kwa mwendo wa majibu ya serikali, EL ni jasiri aliyeweka mbele dhana ya uwajibikajii kwa dhati kwa kuwajibika kwa nafasi yake..
   
 12. h

  hamnazo New Member

  #12
  Jul 27, 2009
  Joined: Jul 12, 2009
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mimi nadhani haya maoni yanayotolewa na watu wengi kuhusu HOSEA ule ujuaji tu wa watu ambao maranyingi wao huwa wanangojea mtu fulani akosee ndo wapate la kuongea maana ukweli hapo uko wazi kabisa ....pole kaka HOSEA lakini komaa tu na hawa wabongo maana wana njaa hao....!
   
 13. Haki.tupu

  Haki.tupu JF-Expert Member

  #13
  Jul 27, 2009
  Joined: Apr 25, 2008
  Messages: 254
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Unataka kusema BUNGE ni kijiwe tu cha kutoa ushauri na serikali kuamua kuuchukua au kuukataa huo ushauri! Accountability ya serikali itakuwa wapi sasa!

  I find the the gvt response so disrespectful to serious efforts! Kama na wabunge nao wasipo react vilivyo nitaona wote wanacheza bao tu.
   
 14. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #14
  Jul 27, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Kwa mtazamo wangu sijui tunaelekea wapi??? Kwa sababu lengo ni kusafisha baadhi ya watendaji isingekuwa rahisi kusema kwa Hosea alikosea. Kwa kusema hivyo ni jibu la moja kwa moja kuwa EDO et al wana makosa!!! Hapo ni kusafishana kiaina tu!!! Kwa hiyo unataka kuniambia ripoti ya kamati ya Mwakyembe et al ni sawa na ile ya PCB enzi zile ila tu Hosea hakusoma vizuri?? Hii hainingii akili kabisa!!!! Tz bora liende tutafika tu hata kama tutafika kwa kupanda mti ukiwa umevaa viatu!!! Naamini siku moja watanzania wataamua kuvua viatu na kupanda mtu pekupeku!!! Kila kitu kina mwisho wake, mzuri au mbaya, the choice is yours!!!
   
 15. F

  FrankGM Member

  #15
  Jul 28, 2009
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kulingana na suala lenyewe lilivyokuwa, Hosea alitakiwa ajiuzulu au PCCB ivunjwe. Kwa taasisi nyeti kama PCCB kufanya kosa kubwa la kiufundi katika kiwango kile ni jambo lisilokubalika kabisa.
  Lisipofanyika moja kati ya hayo basi hata kujiuzulu kwa Lowasa hakukuwa na maana kubwa na itaonekana umuhimu wa chombo chenyewe (PCCB) kuwa na manufaa kidogo sana. Kama hata suala zito kama hili PCCB haikuweza kulishughulikia ilivyopaswa tutegemee nini kutoka kwao? Hii ni fedheha kubwa mno!!! Ili PCCB ijisafishwe ilipaswa mtendaji mkuu wa taasisi hiyo ajitoe kwa maslahi ya taifa kama tume ilivyopendekeza.

  Kuna wakati inasemwa kuwa kiongozi fulani kafanya uamuzi mbovu kwasababu ya washauri wabaya LAKINI hapa kashauriwa vizuri atekeleze. Asingeshauriwa hivyo angekuwa na kigezo cha kujitetea kuwa hakuna aliyemshauri hivyo.
  Hosea ni bora aondoke kwa kuisafisha PCCB!!!!!
   
 16. Jumboplate

  Jumboplate Senior Member

  #16
  Aug 5, 2009
  Joined: Jul 29, 2008
  Messages: 133
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kama mnataka Hosea afukuzwe basi hakuna umuhimu wa kuwepo kanuni/miongozo/sheria n.k za utumishi wa umma...onyo ni kitu cha kawaida mtu anapofanya uzembe kazini na suala la kumfukuza kazi mtumishi lina taratibu zake, kwaiyo kama hatuzipendi taratibu hizo tufanye jitihada zibadilishwe na sio kutaka mtu mmoja aondolewe halafu kanuni/miongozo/sheria mbovu ziendelee kuwepo.
   
Loading...