Kamati ya Msiba Mwili ukienda Dodoma, baadaye jioni tuitane chemba na tukosoane kwa uzembe wa hali ya juu ulioonekana leo Uhuru

Hahahah yani hili jitu ni hovyo sijawahi kuona Kamati imeundwa na Rais afu linamshauri CDF aingilie kati yani lina mshauri CDF afanye jambo la kihaini, Kiusalama hali ingekua mbaya zaidi kama watu wasingeruhusiwa kumuuaga mpendwa wao....

Mnaumizwa hadi na maiti nyie mijitu mbona ya hovyo sana
Wewe ni chura tuliza akili zako za kichura. Huna ujualo. Hapo ikitokea lakutokea huoni kama maelfu ya watu watakufa? Kubwa jinga wewe.
 
Lakini watanzania na sisi tuna vichwa vigumu hebu fikiria mtu anakwenda pale taifa na watoto watatu na housegirl sasa kwanini asiende mmoja tu kwani lazima nyumba yote mwende? Kaeni majumbani muangalie kwenye TV
Labda wao wamechukulia ni outing sababu ni weekend.
 
Wewe ni chura tuliza akili zako za kichura. Huna ujualo. Hapo ikitokea lakutokea huoni kama maelfu ya watu watakufa? Kubwa jinga wewe.

Wewe ni chura tuliza akili zako za kichura. Huna ujualo. Hapo ikitokea lakutokea huoni kama maelfu ya watu watakufa? Kubwa jinga wewe.
Ndo anaagwa kwa heshima mtake mstake utaratibu umewekwa vizuri ila kwa mnayoiita stampede watu wamefosi kuingia ....J alikua na anapendwa nyie endeleeni na roho zenu za kifirauni
 
Wote msiba umetugusa
Lakini watanzania na sisi tuna vichwa vigumu hebu fikiria mtu anakwenda pale taifa na watoto watatu na housegirl sasa kwanini asiende mmoja tu kwani lazima nyumba yote mwende? Kaeni majumbani muangalie kwenye TV
 
Ndo anaagwa kwa heshima mtake mstake utaratibu umewekwa vizuri ila kwa mnayoiita stampede watu wamefosi kuingia ....J alikua na anapendwa nyie endeleeni na roho zenu za kifirauni
Unadhani wote wanaokwenda kumuangalia wanahuzuni nae sana?
 
Mmmh mnamuonea wivu hadi Marehemu. Hao watu hawajalazimishwa mkuu,hapo ni dar tu bado dom na kwengineko si mtapovuka sana na kujaza server za JF
Mwenzio kashauri utaratibu mzuri wa usimamizi watu wamuage rais wao we umekuja na mihemko tofauti kabisa dah
 
Naheshimu mawazo yako piaila hao wamama wenye watoto akili ndogo,walitakiwawajiongeze wabaki majumbani
Wale wa kwa Mwamposa ni watanzania kama hawa walioko uwanja wa uhuru. Kibaya ni kwamba hawa walioko uwanja wa uhuru wako na majonzi, they're emotionally disturbed. Sio rahisi kufuata utaratibu.

Point ya msingi zaidi, wamama wengi wamebeba watoto wadogo katikati ya huu msongamano. Sidhani kama ilikua busara kuruhusu hili. Anyway, naheshimu mawazo yako!
 
Nilitegemea kabisa kuwa Zoezi hili hasa la Leo Siku ya Pili mngeliratibu Kiutaalam na Kiuweledi kabisa ila mmeonyesha Mapungufu makubwa.

Binafsi nilitegemea Tukio kama hili kama Kwenu ni geni basi mngeweza tu kufanya Consultation na wale Waliosimamia Zoezi zima la Kuuaga Mwili wa Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere hapo hapo Uwanja wa Uhuru ili nanyi mpite mule mule ila kwa Upuuzi wenu hilo hamkulifanya.

Kuna Hatari moja ya kutokea kwa Stampede nilikuwa naanza Kuiona Leo Uhuru Stadium (ila naona Malaika ) wameiepusha hata hivyo kama Umakini hautazingatiwa huenda Leo Marehemu (Hayati) Dkt. akasindikizwa na Watanzania wengine Mavumbini kutokana na Uzembe ninaouona sasa.

Hivi inaingia Akilini kweli mnajua kabisa kuwa Capacity ya Uhuru Stadium ni Watu 40,000 halafu nyie hao hao Kutwa huku Mitaani mnahimiza Watu wajitokeze kwa Wingi na wamejitokeza almost 60,000 to 70,000 (wa ndani na nje) halafu Wanawashinda Kuwasimamia na mnaanza tena Kuwaambia wasubirie nje huku wengine mkiwaambia warejee Majumbani.

Na Wewe DC wa Temeke Godwin Gondwe acha kila mara Kutupigia Kelele zako za Kutupanga hapa Uwanjani kwani Wewe na Kamati yako (yenu) nzima iliyo na RC wa DSM Kunenge, Premier Majaliwa na Waziri (ambaye sijawahi Kumuelewa) Jenister Mhagama mlitaka Uwanja ufurike hivyo ( Kilazima ) ili Mataifa mengine duniani yajue kuwa Marehemu (Hayati ) alikuwa anapendwa sana. Acheni tu tufurike na Tufe ili Msiba huu uzidi kupata Vibe na Lengo lenu litimie.

Hili Zoezi lingeachwa 100% lisimamiwe na JWTZ kama walivyoaminiwa katika Msiba wa Mwalimu Nyerere 1999 wala Upuuzi huu usingetokea. Mnang'ang'ania Kusimamia Misiba wakati hamna Uwezo wa Kuiratibu Kiusalama zaidi na Kiitifaki.

Mnaona kabisa akina Mama tena Wamebeba Watoto Migongoni na Watoto wengine wadogo kabisa wamepanga Mstari katika hali ya Kubanana na wanapumua kwa taabu mnaacha na Kusifu kuwa wamekuja Kuaga wakati hiyo ni Hatari mno Kwao. au Marehemu ( Hayati ) aliwaachieni Wosia kuwa mumtafutie wa Kuondoka nae? Mlishindwa nini tu Kuzuia akina Mama wenye Watoto wadogo na Watoto wasije na wabakie Majumbani mwao?

Na Wewe Kaka yangu CDF Jenerali Mabeyo acha sana Upole Kaka ingilia kati na toa Maelekezo yako ya Kijeshi kuwa Zoezi zima sasa litaratibiwa Kijeshi ili Kuokoa Maisha ya Watu yanayohatarishwa hapo na muda mwingi pia Kupotezewa. Na nakuomba sasa CDF Jenerali Mabeyo hata huko Dodoma, Zanzibar, Mwanza na Geita Jeshi lako zuri la JWTZ ndiyo liwe in charge katika Uratibu wote na msiwaachie tena hao Wapuuzi kama hawa wa Dar es Salaam whom they've proved Failure mpaka sasa.

Sifa zenu na Kiherehere chenu cha Kuwaalika Watu wote Uwanjani huku mkiwa hamjajipanga na mna hao Mgambo na Scouts wenye Njaa ( hawajala ) na Miili yao yenyewe ni Fidodido ( Kimbaumbau ) tupu mtakuja kusababisha Maafa ambayo yatawagharimu pia.


JWTZ na FFU tafadhali simamieni Kibabe hili zoezi na anayekaidi Amri zenu hapo Uwanjani piga Rungu la Ugokoni au Kichwani ili Akili ziwachangamke na walio nyuma Mstarini hapo wenyewe watasalimu Amri. Acheni Kubembeleza kama afanyavyo DC Gondwe na huyo Dada MC mzuri mzuri hapo Uhuru Stadium sasa.

Na mpaka All - Rounder nawasema ( nawakosoa ) hivi huku pia nikiwashauri jueni kuwa Nawapenda kuliko Maelezo japo najua mtanichukia na Kuninunia sana tu. Badilikeni na Mjirekebishe kwani bado hamjachelewa.

Imeisha hiyo!!
Mwandiko wa GENTA huu.
 
Unadhani wote wanaokwenda kumuangalia wanahuzuni nae sana?
Asilimia kubwa yes ingawa wapo wanaoenda kwa ajili ya adventure, kupoteza mda na Kwa Unafiki.

Tuache hayo turudi kwenye kiini cha hoja je ni kweli Uratibu wa zoezi Zima la Kuaga Mwili hauko vizuri? Ukichunguza kwa makini utagundua si kweli bali mtoa uzi ana viashiria vya uchonokozi na uchonganishi Mosi kwa kuzingatia Wingi wa watu Dar imepewa siku mbili(hii ni ishara ya kwanza ya Umakini katika kuratibu). Pili Kutumia Uwanja wa Uhuru ambao sio tu una uwezo wakuchukua waombolezaji 40k+ bali pia una historia ya Kuaga Miili ya viongozi wengine kama Hayati BM na JKN hivyo kuwa muendelezo mzuri wa tunu ya historia (Hii ni sababu ya Pili kuwa Zoezi la Uratibu lipo sawa) nyongeza Uwanja wa Uhuru upo Chini (height) na una angles chache kulinganisha na Taifa hivyo kiusalama ni rahisi kusecure paramaters mbili kwa wakati mmoja yani land and air paramaters (desa la bure kuassasinate kupitia Uhuru ni changamoto kuliko taifa) .Jambo la tatu muhimu lililozingatiwa ni mda Uwanja umefunguliwa tangu sa kumi na mbili ili kuruhusu idadi kubwa ya watu kumuaga kipenz chao sema changamoto ya waswahili wanaelekezwa ukishaaga uende nyumban mazima kupisha wengine wao wanaaga afu wanarudi tena ndani.Pamoja na kwamba Kamati imezingatia haya lakin drawbacks huwa hazikosi kama watu kutokuondoka eneo la tukio baada ya Kuaga lakin ukumbuke kuna walemavu, wamama na Watoto ambao speed yao kwenye Kuaga si kali hivyo kudhohofisha ufanisi.

Tukija kwenye hoja ya Pili aliyoitoa kichaa All-rounder ashakum si matusi. Eti CDF aache uoga aingilie kati wabebe zoezi Lao si tu ni upunguani bali umajinuni Kamati imeundwa na Rais ambaye ni mkuu kwa CDF kumshinikiza CDF atumie mabavu kupoka utaratibu aliouinitiate CIC ni kuchochea uhaini. Lakini pia ukiangalia kuanzia kuutoa Mwili Lugalo,kuuingiza Uhuru na kuuondoa vyote vimefanywa na kusimamiwa na JWTZ ChinI ya coordination ya Kamati. Mtu kuibuka na kusema limefanywa na viherehere wasio wanajeshi unaona kabisa ni hoja za kihaini tu zimetawala eti bwana Donie Yen kwenye lile Ceremonial Limousine lililokua linapull casket uliona wamepanda kina Gondwe na Mhagama???
 
Lakini watanzania na sisi tuna vichwa vigumu hebu fikiria mtu anakwenda pale taifa na watoto watatu na housegirl sasa kwanini asiende mmoja tu kwani lazima nyumba yote mwende? Kaeni majumbani muangalie kwenye TV
Suala zima la kuuzungusha mwili sehemu tofauti ni kituko.

Mwili wa Magufuli umefanywa kama circus freakshow.

Kawaida watu hufuata mwili kutoa heshima za mwisho, mwili haufuati watu.
 
Mmmh mnamuonea wivu hadi Marehemu. Hao watu hawajalazimishwa mkuu,hapo ni dar tu bado dom na kwengineko si mtapovuka sana na kujaza server za JF
Marehem aoneww wivu gn? Hata hivyo huu utaratibu wa Kufanya mainyesho maiti n ujinga na kuna watu watakuja kujibu..... Mtu akishafariki wajibu n kuzikwa Tena Haraka na mapema Sana..... Ktk uislamu huu utaratibu haupo.
 
Back
Top Bottom