Kamati ya Mrema yakwaa kigingi Ikulu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kamati ya Mrema yakwaa kigingi Ikulu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by nngu007, May 31, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  May 31, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Na Martha Fataely,Tanga

  KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) imehoji hatua ya kurejeshwa kazini kwa Ofisa Ardhi wa Wilaya ya Tanga, baada ya kufukuzwa kazi kwa tuhuma za kuuza viwanja mara mbili, ambapo imeelezwa kuwa amerejeshwa kwa barua ya ikulu.

  Kamati hiyo chini ya mwenyekiti wake, Bw. Agustino Mrema, imesema kuwa imeshangazwa na taarifa ya ardhi katika halmashauri hiyo lakini pia kuhusu kurejeshwa kazini kwa afisa huyo Bw. Makwasa Biswalo aliyehusika na matatizo ya ardhi wilayani hapo.

  Wakichangia hoja kuhusiana na taarifa hiyo wajumbe wa LAAC, Mbunge wa Kigoma Kusini Bw. David Kafulila, Mbunge wa viti Maalum mkoa wa Morogoro Bi. Susan Kiwanga waliikataa taarifa hiyo na kutaka hatua kuchukuliwa.

  Walisema haiwezekani kuwapo na taarifa ya migogoro ya ardhi ambayo imesababishwa na mtumishi huyo lakini iamriwe arudishwe kazini, hivyo ni vyema hatua za awali za kumsimamisha kazi zikachukuliwa tena.

  Katika taarifa yake kwa kamati hiyo Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Bw. Gikene Mahene alisema mtumishi huyo awali alifukuzwa baada ya kubainika kuhusika na utata wa umiliki viwanja.

  Alisema mtumishi huyo alibainika kuwauzia wananchi viwanja zaidi ya mara moja hivyo kusababisha migogoro mikubwa ya ardhi katika halmashauri hiyo lakini pia wananchi kukosa imani na uongozi. Bw. Gikene aliongeza kusema kuwa ushahidi wa zaidi ya viwanja 70 ulipatikana hivyo kuifanya halmashauri kuchukua hatua za nidhamu dhidi ya mtumishi huyo ikiwa ni pamoja na kumfukuza kazi.

  "Baada ya kumfukuza kazi alikata rufaa tume ya utumishi wa umma ambayo hata hivyo iliridhia kufukuzwa kazi kwa mtumishi huyo lakini baadaye ilikuja tume ya rais ya kushughulikia migogoro ya ardhi na kumrejesha kazini,” alisema.

  Alisema mtumishi huyo aliwasilisha barua ya kurejeshwa kazini kutoa ikulu jambo lililowafanya wamrejeshe kazini ambapo mpaka sasa ni afisa ardhi katika halmashauri ya jiji la Tanga.

  Baada ya kuwasilishwa kwa taarifa hiyo Mwenyekiti wa LAAC, Bw. Mrema alitaka barua iliyotoka ikulu kuwasilishwa katika kamati hiyo huku pia akielezea kamati kutoridhishwa na hatua hiyo iliyochukuliwa.
   
 2. Moshe Dayan

  Moshe Dayan JF-Expert Member

  #2
  May 31, 2011
  Joined: Feb 10, 2008
  Messages: 811
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 45
  duuuh!! Asa maendeleo yatakuja kweli kwa kulindana namna hii!!
   
 3. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #3
  May 31, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Huyu afisa ardhi asijekuwa na uhusiano na Biswalo wa mambo ya nje, nadhani ni balozi sasa hivi.

  Hii Tanzania tambarare sana, wahalifu ndio vipenzi vya watawala wetu, khaaaaa!!
   
 4. Najijua

  Najijua JF-Expert Member

  #4
  May 31, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 1,029
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Kama wanafanya kwa dhati hakika kamari za bunge zitaleta changamoto katika maendeleo
   
 5. S

  Siao Member

  #5
  May 31, 2011
  Joined: Jan 4, 2008
  Messages: 96
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ikiwa ni kweli ujinga huu unafanywa na viongozi wetu - utakuwa upuuuuzi sana, na nchi itakuwa kama kawaida yake haina mwenyewe....
   
 6. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #6
  May 31, 2011
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Ikulu ya JK ndio matatizo ya kila kitu, wanashirikiana na hawa maafisa ardhi kuibia watanzania. Kazi unayo mzee wa Kiraracha, huwa unajidai sana kumtetea JK haya sasa ndio huyo anauza viwanja mara mbili mbili. Shame!!!!!!!!!!!!
   
 7. RedDevil

  RedDevil JF-Expert Member

  #7
  May 31, 2011
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 2,287
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Huyo ni sample tu katika maofisa lukuki wa serikali wanaotumia vibaya nafasi zao na kusababisha usumbufu, hasara pamoja na kuiba pesa za serikali kwenye miradi isiyoisha.
   
 8. Chilipamwao

  Chilipamwao JF-Expert Member

  #8
  May 31, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 514
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  mafisadi wako kazini kama kawa, Nchi hii haiwezi kuondokana na ufisadi bila kuiondoa CCM, wamejivua gamba sumu yao imekuwa kali zaidi. Wameendelea kwa mazoea kwa miaka 50, si rahisi kuacha kwani imekuwa tabia ya kulindana.
   
 9. Indume Yene

  Indume Yene JF-Expert Member

  #9
  May 31, 2011
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 2,932
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Mnachoshangaa ni nini wakati uchafu wote umerundikana Ikulu? Kama wakazi wa hilo jengo jeupe ni mafisadi, unategemea nini?
   
 10. P

  Pagi Ong'wakabu Member

  #10
  May 31, 2011
  Joined: Sep 15, 2010
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hilo ndo gamba la kichwa lililowashinda mafisadi wa sisiemu kulivua, kazi ipo si mchezo maana uchafu wote unaanzishwa na BMW & MASWAIBA WAO, upo hapo Mrema nakushabikia kwako chama cha magamba?
  "KALUPUNDU BA MAYU" (vigeregere akina mama) Rais Mkapa, 2005 Tarafa ya Samuye Shinyanga
   
Loading...