Kamati ya Mo Ibrahim iliona Mkapa hana sifa, Kikwete kaonaje anazo sifa za Uadilifu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kamati ya Mo Ibrahim iliona Mkapa hana sifa, Kikwete kaonaje anazo sifa za Uadilifu?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kibunda, Dec 12, 2011.

 1. k

  kibunda JF-Expert Member

  #1
  Dec 12, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 403
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Ndugu wana JF,

  Mjadala wa JK kutoa nishani bado unaendelea. Hivi sasa ninajiuliza kama Kamati ya Mo Ibrahim iliona Mkaba hana vigezo vya uadilifu, hivyo hawakumpa Tuzo za marais wa Afrika, hivi Kikwete ametumia vigezo gani kumuona anasifa? Ama ndiyo usanii unaendelea?
   
 2. F

  FJM JF-Expert Member

  #2
  Dec 12, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Wakati Kikwete anaingia madarakani 2005 kulikuwa na dalili za wazi kabisa za chuki fulani kwa Mkapa na hata bungeni Mkapa alikuwa 'hoja'. Wabunge walimshambulia kama kitoe. Lakini sasa naona jiwe walilokataa waashi linakuwa jiwe kuu... Kupitia vyombo vya hahari tunambiwa kuwa Mkapa ndiye aliyemwokoa Kikwete huko Dodoma wakati wa kikao cha NEC! Kwa hiyo Nishani inaweza kuwa sehemu ya shukrani (personal) toka kwa Kikwete kwenda kwa mwokozi wake Mkapa. Wanasema rafiki wa kweli ni yule akujuaye wakati wa njaa. Hata mimi ningekuwa Kikwete ningempa Mkapa something. NEC ilikuwa moto!
   
 3. AirTanzania

  AirTanzania JF-Expert Member

  #3
  Dec 12, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 1,127
  Likes Received: 678
  Trophy Points: 280
  Uadilifu wa Ufisadi, kumbuka kikwete anaendeleza Ufisadi ulioachwana Fisadi Mkapa  Hekima ni Busara, PAW
  Ficha Upumbavu wako; Usiifiche Hekima yako!
  [​IMG][​IMG]
  Kuwa na Busara
   
 4. kajwa

  kajwa Member

  #4
  Dec 12, 2011
  Joined: Oct 26, 2011
  Messages: 48
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Sipendi Mkapa jamani......
  Kuliko marais wote wa nchi hii
   
 5. Imany John

  Imany John Verified User

  #5
  Dec 12, 2011
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 2,777
  Likes Received: 262
  Trophy Points: 180
  Katika unywaji kuna kugonganisha vinywaji(ishara ya kujipongaza )

  Hata katika ulaji wa nchi,kuna kupeana nishani(ishara ya kupongazana kwa jinsi ulivo ila nchi)
   
 6. Tony Almeda

  Tony Almeda JF-Expert Member

  #6
  Dec 12, 2011
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 397
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hizi nishani zao za zinainshu gani! zaidi ya kujuana, na kama ni vipi watutajie kamati ilioundwa na vigezo walivyotumia kuwachagua hao waliowapa nishani!

  Kama ujaambiwa ni Wassira na Lukuvi wataalamu wa mipasho na majungu!
   
 7. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #7
  Dec 12, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  nyerere=mwinyi=mkapa=kikwete. Period.
   
 8. D

  Danniair JF-Expert Member

  #8
  Dec 12, 2011
  Joined: Feb 18, 2011
  Messages: 361
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ikulu wamezoea kufichiana makosa yao,, Source: kamati teule ya bunge kwenye sakata la Jairo na Katibu mkuu kiongozi.
   
 9. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #9
  Dec 12, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,754
  Likes Received: 82,732
  Trophy Points: 280

  Kinachoshangaza Mkapa naye amepata hiyo nishani pamoja na kuwa na kashfa chungu nzima. Kashfa ya kufanya biashara akiwa Ikulu, kashfa ya ununuzi wa ndege ya Rais, helicopters za jeshi na magari ya jeshi, mkataba wa kuingiza Makaburu kutoka RSA na kuwapa management positions pale TANESCO, kashfa ya mkataba wa madini ambapo tunaambulia 3% tu, kashfa ya uuzwaji wa nyumba za Serikali, kashfa ya wizi uliofanywa na Mkapa wa Kiwira Coal Mining, kashfa ya wizi wa EPA, Meremeta na Kagoda ambao hizo zpte zilitokea wakati wa Mkapa na kashfa ya ununuzi wa rada. Pamoja na kashfa zote hizi za Mkapa, msanii Kikwete kaamua kumtunuku Mkapa nishani hiyo!!!! Kweli Kikwete ni msanii wa hali ya juu!!!
   
Loading...