Kamati ya miundombinu yahimiza nguvu zaidi taasisi ya teknolojia ya ujenzi - ICoT

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
666
835
KAMATI YA MIUNDOMBINU YAHIMIZA NGUVU ZAIDI TAASISI YA TEKNOLOJIA YA UJENZI - ICoT

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu imeiagiza Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, kuongeza nguvu kwenye Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICoT), kwa kuitengea fedha za kutosha ili iweze kujiendeleza kwa kuwa na vifaa na mitambo ya kisasa, vitendea kazi, majengo na rasilimali watu kwa ajili ya kuwezesha kuzalisha mafundi wenye uwezo na ujuzi.

Hayo yamesemwa mkoani Morogoro na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Selemani Kakoso, mara baada ya kupokea taarifa ya Taasisi hiyo iliyoanzishwa kwa kuunganisha Chuo cha Taifa cha Ujenzi cha Morogoro na Chuo cha Teknolojia stahiki ya nguvu kazi cha Mbeya na kusisitiza uhitaji wa taasisi hiyo kuongezewa bajeti.

“Kamati inaomba Wizara muwe na dhamira ya dhati ya kukisaidia Chuo hiki ili kiweze kuimarika kwani kufanya hivyo mtazalisha waatalamu wa kutosha wenye ujuzi na uwezo wa kufanya kazi kwa vitendo kwa kutumia teknolojia stahiki”, amesema Mhe. Kakoso.

Aidha, Kamati hiyo imesisitiza kuwa Taifa linategemea sana vyuo hivo kwani ndio msingi wa kupata mafundi wa ngazi ya kati na kuendeleza kusimamia na kuboresha miradi ya barabara na reli inayoendelea.

Kamati imeiagiza Wizara kuhakikisha Taasisi hiyo inapata wakufunzi wa kutosha wa fani zote ili kuongeza nguvu na ujuzi kwa wanafunzi watakaopata fursa ya kujiendeleza katika Taasisi hiyo na kusaidia Chuo kuongeza kutambulika Zaidi.

Awali akitoa taarifa kwa Kamati, Mkuu wa Taasisi hiyo Eng. Mahmoud Chamle, ameieleza kamati kuwa uanzishwaji wa taasisi hii utachangia kupunguza changamoto ya ukosefu wa ajira kwa vijana kwani mafunzo yanayotolewa hapo yatawaandaa wahitimu kujiajiri zaidi.

Ameongeza kuwa Taasisi yake inatoa mafunzo ya muda mrefu katika fani za ujenzi, umeme, na mitambo katika ngazi ya Astashahda na Stashahada lakini pia inatoa mafunzo ya muda mfupi na mafunzo maalum kwa wahitimu wa fani za kihandisi na zinazoendana ili kuwaandaa na kuwajengea uwezo.

Ameendelea kusema kuwa kwa sasa Taasisi inaendesha mafunzo juu ya matumizi ya Teknolojia Stahiki ya Nguvu kazi katika kazi za ujenzi, matengenezo na ukarabati wa barabara.

Kamati ya Miundombinu ipo Mkoani Morogoro katika ziara yake ya kukagua Miradi na kazi zinazofanywa na taasisi zilizo chini ya wizara ya Ujenzi na uchukuzi
 

Attachments

  • IMG-20230316-WA0768(1).jpg
    IMG-20230316-WA0768(1).jpg
    150.3 KB · Views: 2
  • IMG-20230316-WA0769(1).jpg
    IMG-20230316-WA0769(1).jpg
    87.6 KB · Views: 2
  • IMG-20230316-WA0771(1).jpg
    IMG-20230316-WA0771(1).jpg
    158.5 KB · Views: 2
  • IMG-20230316-WA0772(1).jpg
    IMG-20230316-WA0772(1).jpg
    65.3 KB · Views: 2
  • IMG-20230316-WA0773(1).jpg
    IMG-20230316-WA0773(1).jpg
    168.7 KB · Views: 2
  • IMG-20230316-WA0774(1).jpg
    IMG-20230316-WA0774(1).jpg
    118.9 KB · Views: 2
  • IMG-20230316-WA0775(1).jpg
    IMG-20230316-WA0775(1).jpg
    100.1 KB · Views: 2
Mkuu 'JUMA JUMA', najua nia ni njema kuhusu haya yanayohimizwa na hii kamati ya Bunge, lakini haya hayana tofauti yoyote na mengi mazuri yaliyopendekezwa katika maeneo mbalimbali kwa manufaa ya taifa letu.

Tatizo la nchi yetu ni kutokuwa na lengo maalum na kuhakikisha juhudi zinafanyika kulitimiza lengo tulilonuia.

Nikitumia mfano wa haya yaliyohimizwa na hiyo kamati, halafu ukatazama mifano ya nchi zilizodhamiria na kufanya mambo kama hayo yetu na kufanikiwa itasaidia kuona picha yetu ilivyo mbovu.
Mfano ni China na mashirika yao ya ujenzi yanayofanya miradi mbalimbali duniani kote katika miaka hii.

Sisi tunagusagusa tu, tunapapasa papasa tu na kusema maneno mengi sana, lakini matokeo hakuna kabisa. Hapo hao wabunge wamemaliza kazi yao, na hutasikia chochote tena juu ya jambo hilo.

Hatutaweza kamwe kuiendeleza nchi kwa mtindo huu wa uongozi.
 
Back
Top Bottom