Kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) yatembelea Ofisi za Jamii Forums

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,746
11,876
R42V.png

Kamati ya Maudhui ya TCRA ikiongozwa na Makamu Menyekiti wake, Ndugu Joseph Mapunda, imetembelea ofisi za Jamii Forums ikiwa na lengo la kujifunza mambo kadha wa kadha kuhusu Taasisi na kujionea namna huduma inavyotolewa kwa wananchi. Kamati hiyo ilipokelewa na watendaji wa Jamii Forums wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji, Ndugu Maxence Melo.

Wakiwa katika ofisi za Jamii Forums, Wajumbe wa Kamati ya Maudhui wamepata fursa ya kujifunza kuhusu utendaji wa Taasisi ya Jamii Forums inayofanya kazi kama Taasisi isiyo ya Kiserikali (NGO), na kupata uelewa wa namna inavyofanya uchechemuzi wa masuala anuai ikiwemo Haki za Kidijitali, Uhuru wa Kujieleza, Demokrasia, Uwajibikaji, Utawala Bora nk.

Katika kikao cha pamoja na watendaji wa Jamii Forums, Kamati ya Maudhui ilipata fursa ya kueleweshwa mambo yafuatayo:-
  1. Historia ya Jamii Forums (Taasisi) na mahusiano kati ya Taasisi na JamiiForums.com (tovuti)
  2. Mpango Mkakati wa miaka mitano (5) wa Taasisi (2020-2024)
  3. Sera ya Uhariri na jinsi inayotumiwa na Wasimamizi wa Maudhui wa JamiiForums
  4. Muongozo wa Uendeshaji wa Mijadala ndani ya JamiiForums.
Ziara hii imeongeza uelewa kwa pande zote mbili, kwa watendaji wa Jamii Forums kuelewa jinsi Kamati ya Maudhui inavyofanya kazi na kwa upande wa Kamati kufahamu namna ambavyo Taasisi ya Jamii Forums inafanya kazi na kutoa huduma kwa wateja wake kama mdau wa mawasiliano.

Watendaji wa Jamii Forums waliweza kutoa mapendekezo ya uboreshaji kwa Kamati ya Maudhui hususani katika usimamizi wa watoa huduma na utoaji wa elimu kuhusu kanuni na taratibu za mawasiliano.

Akizungumza wakati wa kikao na Kamati hiyo, Mkurugenzi Mtendaji, Maxence Melo alisisitiza kuangaliwa upya Kanuni za Maudhui Mtandaoni (2020) na kurekebishwa ili zisiue ubunifu nchini. Kamati imesema imepokea mapendekezo hayo na yatafikishwa sehemu husika.
 
Hongera sana Maxence.

Kwa mbaali naona kama Serikali imeanza kuikubali Jamiifoums as an alternative observer na peoples voice katika masuala mbalimbali.

Of course ingekuwa kwa amri, kuna watu serikalini ambao wangetaka JF ife.

Hata hivyo ukiacha michango ya kijingajinga inayotolewa na members wachache wa JF, michango mingi ni ya kujenga na hata kuwa kama whistle blowers katika masuala mbali mbali.

Tunajua kuwa kisirisiri viongozi wengi wanaperuzi JF, tuna washauri tu wapuuze mambo ya kijinga na wayachukue yale yatakayowajenga.

Tupo wengi ambao ni wazalaendo, watu ambao tungependa kutoa maoni juu ya masuala yanayotokea kwenye jamii yetu.
 
Swadakta....

Hayo ndiyo mambo tunayoyataka vijana.

Kutembeleana, kusikilizana kistaarabu ili kila mdau ajiboreshe kwa mustakabali mwema wa Taifa Letu.

Kudos TCRA
Kudos Maxence Mello et al
Kudos JF.

Maendeleo hayana vyama!
 
Kwenu JF...

Najua hakukukosekana kuongelewa suala la VPN na Sheria yetu yenye kukataza hayo.
 
Hongera sana Maxence.

Kwa mbaali naona kama Serikali imeanza kuikubali Jamiifoums as an alternative observer na peoples voice katika masuala mbalimbali...
Hebu kuwa na adabu wewe, hakuna ujinga ulio ujinga mtupu, hata kwenye wajinga walio werevu wana la kujifunza. Tatizo mnapenda sana kupangiwa kila kitu cha kuongea.

Sent from my TECNO L9 Plus using JamiiForums mobile app
 
Jambo jema, kuliko kutumia Mahakama kujadiliana mnaweza kutumia ofisi ili kuokoa rasilimali fedha na muda.
 
17 Reactions
Reply
Back
Top Bottom