Kamati ya Mambo ya Nje ya Umoja wa Ulaya (EU) wataka kujua msaada wa Euro Mil. 27 za COVID-19 kwa Tanzania uliahidiwa kwa vigezo gani?

Lord denning

JF-Expert Member
Jun 3, 2015
13,227
26,047
Amani iwe nanyi tena wadau!

Nimetoka kutazama mjadala mzito unaoihusu Tanzania katika Kamati ya Mambo ya Nje Bunge la EU.



Napenda tu kusema yafuatayo

1. Tanzania tuna hali mbaya sana. Wajumbe wa kamati hii wameijadili vibaya sana Tanzania na wengine kupendekeza hatua kali zaidi zichukuliwe juu ya Tanzania ikiwemo kuondoa kabisa misaada yote ya kifedha kwa Tanzania

2. Mwenyekiti wa Kamati ametoa maelekezo umoja wa Ulaya sasa iuangalie Tanzania kwa jicho makini zaidi na kufuatilia kwa makini zaidi juu ya Tanzania na hali ya kutisha ya Haki kukandamizwa kwa Haki za binadamu na utawala Bora kunakoendelea Tanzania

3. Wamehoji hadi kwanini walitoa ahadi ya fedha kiasi cha Euro Mil. 27[ Zaidi ya Bilioni 74] za ku support harakati za kupambana na COVID19. Wamembana afisa wao kuhusu vigezo gani vilitumika kuona Tanzania inastahili kupewa hela hizo wakati Tanzania haifuati maelekezo ya WHO na wametangaza kuwa nchi iko covid free kutokana na sala.

4. Wamesema sasa waangalie kwa namna gani watatoa msaada wao na hela zao kwa vyama vya siasa vinavyotetea demokrasia na watetezi wa Haki za binadamu waliopo Tanzania na sio kutoa tena hela kwa Serikali.

Sasa kama EU wametoa maelekezo haya sijui ICC watasemaje 😂😂😂😂

Naomba waliopo kwenye list ya ICC wajiandae tu.
===

Bunge la Umoja wa Ulaya limetakiwa kutoa maelezo ya kwanini Jumuiya hiyo ilitoa msaada wa kiasi cha euro milioni 27 za kupambana na Covid19 kwa Tanzania, licha ya kufahamu kuwa nchi hiyo imetangaza kuushinda ugonjwa huo.

Akiwasilisha hoja yake, mbunge wa Jumuiya hiyo kutoka Ujerumani, Bw. David McAllister, amesema anataka kufahamu ni namna gani fedha hizo za walipakodi wa bara la Ulaya zimetumika katika nchi ambayo imekataa kutoa takwimu na kufuata miongozo ya WHO.

"Ningependa uwajulishe wajumbe wa kamati yetu juu ya pesa tulizoipatia Tanzania; kulikuwa na vigezo gani vya kutoa pesa hizi, na ni kipi hasa kinachofanywa kwa kutumia pesa hizi", amesema

McAllister alisisitiza kupatiwa majibu ya papo kwa papo, na kama ikishindikana, basi iwe ni ndani ya saa 48.

------

European Union granted 27mil euros of European taxpayers' money to Tanzania to combat the effects of Covid.

Now we have a regime in the country saying that there is no Covid in the country. We have rather bizzare explanations.

So once again, we have a government who's refused to follow guidelines from the WHO; a government that has refused to provide statistics -- and still we are giving them 27mil euros.

I'd like you to inform members of our committee about the money we have given to Tanzania; what were the criteria for giving this money, and especially what is happening with this money.

We are talking about European taxpayers' money. And I have difficulties that we grant money to a government which is obviously not trying to cooperate in a decent manner.

So could you please answer my question -- and if you're not able now -- I'd expect you to provide details within 48 hours.


Soma pia >

https://www.jamiiforums.com/threads...4-5-za-michango-ya-covid-19-zimeliwa.1786433/

 
Ngoma inogile!

Hapo pia kuna uwezekano wa nchi moja moja kuja na maamuzi yake mbali na yale yatayokubaliwa na EU.

Bado US nao kukamilisha shughuli.

Sitashangaa Benki ya Dunia nayo ikasitisha kutoa mikopo.

Sasa itakuwa ni zamu yao kuandamana kwenda Ulaya na Marekani kutafuta suluhu.

Kweli kadri giza linavyozidi, ndivyo nuru inakaribia.

Je, kuna watu watapigwa chini katika kutafuta suluhu na kuridhisha wahisani?Tusubiri.

NB:Media za kibongo haziwezi kutangaza hizi habari, na hata wakitangaza, basi itakuwa ni kwa kugusigusia tu tena kwa uoga mwingi-ndio tulipofika na sio kosa lao.
 
Kumbe Serikali yetu ilipokea pesa za msaada wa Covid wakati sisi hatuna Corona, sasa watuambie hizo pesa zilipelekwa wapi? na kwanini tukawadanganya wazungu wakatupa pesa wakati sisi ni donor kantre.

Hali yetu huko nje ni mbaya, sasa hilo halina mjadala, sijui tutaweza vipi kuishi kama kisiwa, wakakataa kuwaacha Chadema waende bungeni, sasa wana msalaba mkubwa zaidi wa kuubeba aheri ya wapinzani wangekuwa bungeni.

Zile calculations walizopiga Ndugai na Magufuli kabla ya uchaguzi mkuu zimefeli miserably.
 
Back
Top Bottom