Kamati ya Mahusiano ya Kimataifa ya Bunge la Uingereza yaonya juu ya uwezekano wa kutokea vita vya silaha za nyuklia kati ya nchi zenye silaha hizo

mwanamwana

JF-Expert Member
Aug 1, 2011
1,076
4,113
Kamati ya Mahusiano ya Kimataifa ya Bunge la Uingereza imetoa taarifa inayoonya juu ya uwezekano wa kutokea vita vya silaha za nyuklia kati ya nchi zenye silaha hizo.

Kamati hiyo imeeleza kwamba kutokana na kushindikana ushirikiano wa kidiplomasia kati ya nchi zenye silaha za nyuklia na kadhalika kuendelea kustawishwa kila siku teknolojia na uwezo mpya katika uwanja huo, kumeongeza hatari ya kutokea vita vya silaha za nyuklia dunia. David Howell,

Mkuu wa Kamati hiyo ameitaka serikali ya nchi hiyo kuupa umuhimu wasiwasi wa wawakilishi wa bunge hilo. Aidha Howell ametaka kuongezwa kiwango cha mazungumzo kati ya nchi zenye kumiliki silaha hizo za maangamizi. Ripoti ya kamati hiyo juu ya uwezekano wa kutokea vita vya silaha za nyuklia imetolewa ikiwa ni miezi michache imepita baada ya kutolewa ripoti iliyosema kuwa, Marekani na Russia ambazo ni wamiliki wakubwa wa silaha za nyuklia, zimesimamisha makubaliano muhimu ya silaha baina yao.

Mwezi Februari mwaka huu, serikali ya Marekani kwa kisingizio cha kuwa eti Russia imekiuka mkataba wa makombora kati ya nchi mbili, ilitangaza kwamba imesimamisha Mkataba wa Silaha za Nyuklia za Masafa ya Kati maarufu kwa kifupi kama INF kuanzia tarehe pili Februari na kuanza kutekeleza hatua za kujiondoa kwenye mkataba huo ambazo zitadumu kwa kipindi cha miezi sita.

Kufuatia hatua hiyo, Rais Vladmir Putin wa Russia alisisitiza kuwa hatua hiyo haitakosa jibu na kwamba serikali ya Moscow nayo imesimamisha mkataba hu
 
Hivi wakati wanayagundua hayo madude na hadi kuyajenga walikuwa wanafikiri nini?
 
zipigwe tu ili tuheshimiane
Tukaheshimiane mbinguni?
Kumbuka hii vita haitakuwa na mshindi! Cha zaidi sana sayari dunia itafikia kikomo cha kuweza kuhifadhi uhai tena.

Kwa tecnolojia iliyopo sasa, si Ulaya na Asia tu zitaangamia bali balaa hili litaikumba dunia yote na kutowesha uhai wote duniani

Ni hatari isiyokuwa salama
 
Hivi wakati wanayagundua hayo madude na hadi kuyajenga walikuwa wanafikiri nini?
Walikuwa wana malengo ya kujilinda, kulinda maslahi yao na kuingia taifa lolote lisilokuwa na silaha hizo endapo wakitaka.
Bahati nzuri wakubwa wenye nazo wamegawanyika. Isingekuwa hivyo, leo hii mateso ya wasiokuwa nazo yangekuwa maradufu
Fikiria isingekuwa China na Urusi leo hii mataifa ya Korea Kaskazini na Iran yangekuwaje?
Au isingekua Marekani kuikingia kifua Taiwan angekuwaje mbele ya China?
Mgawanyiko wa haya mataifa makubwa yenye silaha za maangamizi ndio umesababisha mataifa machanga kupata ahueni.

Wanapoongea lugha tofautitofauti ndipo sisi huku tunatakiwa kusonga mbele! Wewe fikiria enzi za ukoloni wangekuwa wamoja tungeweza kupata hata huu uhuru wa maigizo?
 
Tukaheshimiane mbinguni?
Kumbuka hii vita haitakuwa na mshindi! Cha zaidi sana sayari dunia itafikia kikomo cha kuweza kuhifadhi uhai tena.

Kwa tecnolojia iliyopo sasa, si Ulaya na Asia tu zitaangamia bali balaa hili litaikumba dunia yote na kutowesha uhai wote duniani

Ni hatari isiyokuwa salama
Hata itokee technolojia mara 70 zaid ya hii ya unawirishaji wa silaha, still hakuna wa kuweza kuitowesha dunia .
Mpka umri wake aloukadiria mwenye dunia ufike ndio itaisha.
 
Hata itokee technolojia mara 70 zaid ya hii ya unawirishaji wa silaha, still hakuna wa kuweza kuitowesha dunia .
Mpka umri wake aloukadiria mwenye dunia ufike ndio itaisha.
Nimesema kutowesha uhai sio dunia
 
Back
Top Bottom