Pdidy
JF-Expert Member
- Nov 22, 2007
- 55,881
- 29,246
Kamati YA MADINI yataka mfumo mpya sekta ya madini
Mwandishi Wetu
Daily News; Sunday,May 25, 2008 @00:02
Rais Jakaya Kikwete amesema serikali itaifanyia kazi haraka ripoti ya kamati ya madini na amemuagiza Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja ampe maoni yake katika kipindi cha wiki mbili kuanzia jana, ili utekelezaji wa mapendekezo ya Kamati hiyo uanze mara moja.
Kamati hiyo aliyoiunda Novemba 12 mwaka 2007, jana ilimkabidhi ripoti hiyo yenye mapendekezo kadhaa likiwamo la kuanzisha mfumo mpya wa usimamizi na uendelezaji wa sekta ya madini kwa wawekezaji wapya.
Kwa hiyo tunaishauri Serikali kuwashawishi wawekezaji waliopo kuhamia katika mfumo mpya. Utaratibu huu ndio ambao umetumika kwa wenzetu wa Zambia mapema mwaka huu, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mark Bomani alimweleza Rais Kikwete.
Jaji Bomani alimkabidhi Rais Kikwete taarifa kamili yenye kurasa 170, viambatanisho vya taarifa hiyo kurasa 80, na muhtasari wa mapendekezo wenye kurasa 40. Kamati hiyo ilikuwa na jukumu la kuangalia upya mfumo wa usimamizi wa sekta ya madini, na ili kukamilisha kazi hiyo ilikutana na wadau mbalimbali wakiwamo wananchi wanaoishi kwenye maeneo yenye uchimbaji wa madini wakiwamo wa
Maganzo, Lusu, Kakola, Mwendakulima (Buzwagi), Geita, Rwamgasa, Nyakabale, Nyamongo, Buhemba, Mirerani, na Kiwira (Liganga). Ilikutana pia na wataalamu, asasi mbalimbali, viongozi wa kiserikali na kisiasa wa ngazi mbalimbali, wamiliki wa migodi, ilikutana na wananchi wa Dar es Salaam, Mwanza na Arusha.
Kwa mujibu wa Bomani, kamati hiyo pia ilitembelea Zambia, Botswana, Afrika Kusini, Ghana, Canada, Australia, Japan na Thailand. Awali Kamati hiyo ilipewa miezi mitatu kumaliza kazi yake, iliongezewa muda baada ya kuthibitika kuwa kazi ya Kamati hiyo ilikuwa inahitaji muda zaidi.
Mimi nashukuru kuwa kazi hii tumeimaliza, alisema Rais Kikwete na kubainisha kuwa tangu wakati alipokuwa akiiunda kamati hiyo alifahamu kuwa alikuwa amewapa jukumu zito. Serikali imewahi kuunda kamati kama hiyo, ikiwamo ya Jenerali Robert Mboma mwaka 2001, Brigedia Jenerali Mangenya mwaka 2003, Dk Jonas Kipokola mwaka 2004 na ile iliyoongozwa na Lawrence Masha mwaka 2006.
Rais Kikwete alisema, tangu alipoingia madarakani amekuwa akitafuta namna ya kufanya madini yainufaishe Tanzania hivyo serikali itaifanyia kazi haraka ripoti hiyo ili madini yawanufaishe wawekezaji na wenye rasilimali hiyo akimaanisha Watanzania.
Ili kuthibitisha dhamira hiyo, Rais aliuliza kama Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja amepewa nakala za ripoti hiyo akaelezwa kuwa atapewa, akawaambia wampe yeye amkabidhi pale pale lakini asipewe muhtasari kwa kuwa unaweza kusababisha asisome ripoti nzima.
"Waziri usimpe summary, executive summary usimpe Waziri, atafanya uvivu, inatakiwa umpe ripoti na viambatanisho, alisema Rais Kikwete, Bomani akamkabidhi nakala ya ripoti na viambatanisho, naye akamkabidhi Ngeleja.
Baadhi ya wajumbe 11 wa kamati hiyo walihudhuria hafla hiyo Ikulu Dar es Salaam wakiwamo, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige ambaye aliteuliwa kuwa mjumbe wa kamati kabla ya kupewa wadhifa huo, na Mbunge wa zamani wa Ilala ambaye sasa ni mfanyabiashara, Iddi Simba.
Wajumbe wengine waliohudhuria ni Mbunge wa Bariadi Mashariki (UDP), John Cheyo, Mbunge wa Kyela( CCM) Dk Harrison Mwakyembe, Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe, na Mwenyekiti wa Soko la hisa la Dar es Salaam, Peter Machunde.
Wateuliwa wengine katika kamati hiyo walioshuhudia Rais Kikwete akikabidhiwa ripoti hiyo ni Wakili Mwandamizi wa Serikali katika Wizara ya Nishati na Madini, Salome Makange, Kamishna wa Sera katika Wizara ya Fedha na Uchumi, Mugisha Kamugisha na Mkurugenzi Msaidizi, Udhibiti na Usimamizi wa uendeshaji Miji, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Edward Kihunrwa
Mkurugenzi wa Madai na Sheria za Kimataifa katika Wizara ya Katiba na Sheria, Maria Kejo na Mshauri wa kodi katika Kampuni ya PriceWaterhouseCoopers, David Tarimo hawakuhudhuria hafla hiyo kwa kuwa walikuwa na udhuru.
Ni matumaini yetu kwamba taarifa hii na mapendekezo yaliyomo, ikiwezekana hata uamuzi wa Serikali juu ya mapendekezo hayo vitawekwa wazi ili kuondoa hisia kwamba taarifa za kamati mbalimbali huwa hazifanyiwi kazi, alisema mwenyekiti wa kamati.
Bomani alisema, wananchi wana matarajio makubwa na wanaamini kuwa kukamilika kwa kazi ya kamati hiyo ni mwanzo wa utatuzi wa matatizo yao ya siku nyingi katika sekta hiyo. Kwa mujibu wa ripoti ya umasikini na Maendeleo ya Watu ya mwaka 2007 iliyozinduliwa Ijumaa wiki hii jijini Dar es Salaam, sekta ya madini inachangia asilimia 3.7 katika pato la taifa (GDP