Kamati ya Madini ya Bunge yahongwa kupitisha Bajeti ya madini?

Sasa mheshimiwa badala ya kutumia vyombo vyako ulivyo navyo kupata taarifa unasubiri hadi uletewe tarifa???
 
na hao wabunge waliopokea mlungula watajwe ili wapiga kura wao wawahukumu siku ileeeee.....
 
Watutajie majina ya wabunge walopokea mlungula ili tuwajue! Kwa hili mpaka mmoja atoe damu
 
Yani huyu pinda hata huwa simuelewi kabisa, yeye mda wote anakuwa mnafiki,anapokuwa bungenia anatetea upuuzi ili
apigiwe makofi na wabunge wa CCM akiwa nje ya bunge anaongea tofauti ili apigiwe makofi wa wananchi, mbona huyu pinda hana msimamo???
 
Hii ni zaidi ya hatari kuna nini kwenye hiyo bajeti mpaka watu watoe pesa na je afisa mdogo tu anawezaje kujichukulia maamuzi ya kuhonga wabunge wa kamati bila maelekezo ya wakubwa wake?
Na hawa wabunge wa safari hii ni mzigo mkubwa kwa nchi na wapiga kura wa majimbo yao! Na katika staili hii maendeleo yatatokea wapi
 
habari za kusadikika zimetoka bungeni, huku waziri mkuu Mizengo Pinda akithibitisha kuwa Wizara ya Nishati na Madini inayoongozwa na mjukuu wa wa Mapcha wa magamba Ndugu Ngeleja, ikiwa imewahaonga wajumbe wa kamati ya Nishati na Madini ya bunge la JMT. Kamati hii inasadikika kula mlungula ili kuwadhulumu watanzania haki yao ya msingi ya kuibana serikali ili umeme uwake.

Maswali.
Kwanini wizara itoe rushwa kwa wabunge inaficha nini?
Je kwanini tuwe na wabunge kama wao kazi yao ni kula rushwa na kuacha kufanya kazi ya kuiwajibisha serikali.
Je takukuru walikuwa wapi?
Usalama wa taifa/CCM walikuwa wapi?
Kwanini hawa wabunge bado wapo bungeni?
Kwanini Ngeleja bado ni waziri?


Ninafikiri inabidi nguvu ya umma iingilie kati kumwajibisha ngeleja na kurugenzi yote ya wizara ya Nishati na madini. Vilele kama wajumbe wa hiyo kamati hawatajitakasa, nao wakimbizwe wote kwani ni wezi na wasioitendea nchi mema. Ni wahujumu wakubwa wa uchumi.
 
Mtu yeyote asiye msafi hawezi kujiamini hasa anapokutana na watu makini...
hivyo wizara husika inajua kuwa haina usafi ndo maana inataka kupitia njia
za mkato katika kukubalika kwenye jamii...

Mungu ibariki Tanzania
 
WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda amekiri kupata taarifa za tuhuma zinazowahusisha maofisa wa Wizara ya Nishati na Madini kuwahonga baadhi ya wabunge katika Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini kwa lengo la kutaka urahisi wa kupitishwa kwa bajeti yake.Pinda aliliambia Mwananchi kwa simu jana kuwa “……niseme kwamba jambo hilo nimesikia likizungumzwa, zungumzwa pale bungeni, lakini si kwamba lililetwa rasmi kwangu kwa maana ya kulishughulikia”.

Jana gazeti hili lilichapisha habari kuhusu tuhuma dhidi ya maofisa hao, huku kukiwa na taarifa za Waziri Mkuu, Pinda kufikishiwa taarifa hizo na kuahidi kwamba angelishughulikia baada ya kuwa amewasiliana na Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja.

Waziri Ngeleja alipohojiwa juzi kuhusiana na tuhuma hizo, hakukubali wala kukanusha na badala yake alisisitiza kwamba anayeweza kuzizungumzia ni mwenyekiti wa kamati akimaanisha January.

Mwingine ambaye alitajwa kuarifiwa kuhusu wabunge hao kuhongwa ni Spika wa Bunge, Anne Makinda na kwamba kamati ya uongozi ya bunge anayoiongoza pia ilikuwa imeishapewa taarifa husika.

Hata hivyo Makinda aliliambia Mwananchi juzi kwamba hakuwa na taarifa za tuhuma hizo. "Mimi ndiyo nazisikia kutoka kwako, pengine kama zimeletwa kwa barua sijaiona, lakini sifahamu kitu kama hicho," alisema Makinda alipozungumza kwa simu na Mwananchi.

Habari zilizolifikia Mwananchi zilidai kwamba, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, January Makamba ndiye aliyewashtaki wajumbe wa kamati yake kwa Spika huku akiwachongea watumishi wa Wizara ya Nishati na Madini kwa Pinda kutokana na kujihusisha na vitendo vya rushwa.

Lakini jana Pinda alisema, tuhuma kwamba baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo walihongwa alizisikia na kwamba suala hilo ni kama liliachwa mikononi mwa kamati za bunge na uongozi wa bunge kwa ujumla ili liweze kushughulikiwa.

“Jambo kubwa ni kwamba hizi tuhuma zinapotolewa mara nyingi huwa kama rumors (uvumi) hivi na mimi kama Waziri Mkuu ni vigumu kushughulikia uvumi, inapofikia hapo unawaachia kwanza wahusika walishughulikie,” alisema Pinda.

Kwa mujibu wa Waziri Mkuu, mbali na kusikia jambo hilo likizungumzwa katika vikao bungeni (japokuwa hakutaja vikao hivyo) hakuna taarifa rasmi wala malalamiko ambayo amekwishapelekewa ili ayashughulikie katika nafasi yake.

“Sina taarifa yoyote ya maandishi, maana ili niweze kuact (kuchukua hatua) lazima kuwepo na malalamiko rasmi, kwamba mtu analalamikia jambo hilo halafu mimi nalifanyia kazi, lakini katika mazingira ya sasa hakuna taarifa yoyote zaidi ya maelezo hayo niliyokupa,”alisema Pinda.

Hata hivyo Waziri Mkuu huyo alisema pale malalamiko ya rushwa yanapokuwa na ukweli ndani yake suala la msingi ni kuchukua hatua kwa mujibu wa sheria.

Alipoulizwa kwamba hatua ya maofisa kutoa rushwa kwa baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini huenda imetokana na woga wa kukwama kwa bajeti yao, Pinda alijibu:

“Hiyo haiwezi kuwa excuse (utetezi) kwani rushwa ni rushwa tu, ndiyo maana mimi nasema kwamba kama kuna ushahidi upo basi hatua za kisheria zichukuliwe dhidi ya wahusika na vyombo vya kuchukua hatua vipo.

Kashfa hiyo imeikumba wizara hiyo katika kipindi kigumu ambacho nchi iko gizani huku watendaji wake wakilaumiwa kutokana na uhaba wa nishati ya umeme, huku Waziri Ngeleja akitangaza hali hiyo kuwa ni “janga la kitaifa”.

Kwa ujumla wabunge wengi wamekuwa wakieleza wazi kutofurahishwa na kile wanachodai kwamba ni ulegevu katika wizara hiyo na kuna taarifa kwamba huenda Waziri Ngeleja akapata wakati mgumu atakapowasilisha bajeti ya wizara yake bungeni.

Wizara ya Nishati na Madini inatarajiwa kuwasilisha makadirio ya matumizi bungeni Agost 19 na bajeti hiyo itajadiliwa na kuhitimishwa Agosti 20, mwaka huu.

Miongoni mwa mambo ambayo yamepata upinzani kutoka ndani ya Kamati ya Nishati na Madini pamoja na wabunge wengine wa CCM ni mapendekezo ya wizara hiyo kutaka kujenga makao yake makuu jijini Dar es Salaam kinyume cha ilani ya CCM ambayo inaweka wazi kwamba hakutakuwa na ujenzi wa makao makuu ya wizara jijini humo katika kipindi cha miaka mitano ijayo.
 
Kiongozi ambaye anajari
kazi yake anapokua akisikia taarifa zinazoihusu ofisi yake ama sekita ambayo anaiongoza anapaswa kufuatilia ili kujua undani wake na kuchukua hatua ama anasubiri aletewe kama Mh.Pinda anavyo dai ndipo achukue hatua? Au ilikuwa janja yakutaka kulimaliza kimtindo?
 
Kiongozi&nbsp; ambaye anajari<br> kazi yake anapokua akisikia taarifa zinazoihusu ofisi yake ama sekita ambayo anaiongoza anapaswa kufuatilia ili kujua undani wake na kuchukua hatua ama anasubiri aletewe kama Mh.Pinda anavyo dai ndipo achukue hatua? Au ilikuwa janja yakutaka kulimaliza kimtindo?
 
habari za kusadikika zimetoka bungeni, huku waziri mkuu Mizengo Pinda akithibitisha kuwa Wizara ya Nishati na Madini inayoongozwa na mjukuu wa wa Mapcha wa magamba Ndugu Ngeleja, ikiwa imewahaonga wajumbe wa kamati ya Nishati na Madini ya bunge la JMT. Kamati hii inasadikika kula mlungula ili kuwadhulumu watanzania haki yao ya msingi ya kuibana serikali ili umeme uwake.

Maswali.
Kwanini wizara itoe rushwa kwa wabunge inaficha nini?
Je kwanini tuwe na wabunge kama wao kazi yao ni kula rushwa na kuacha kufanya kazi ya kuiwajibisha serikali.
Je takukuru walikuwa wapi?
Usalama wa taifa/CCM walikuwa wapi?
Kwanini hawa wabunge bado wapo bungeni?
Kwanini Ngeleja bado ni waziri?


Ninafikiri inabidi nguvu ya umma iingilie kati kumwajibisha ngeleja na kurugenzi yote ya wizara ya Nishati na madini. Vilele kama wajumbe wa hiyo kamati hawatajitakasa, nao wakimbizwe wote kwani ni wezi na wasioitendea nchi mema. Ni wahujumu wakubwa wa uchumi.
attachment.php

270102_249371588412260_100000182626581_1157660_5263231_n.jpg
 
Like father like son, baba yake alikuwa mtetezi mkubwa wa mafisadi na kudai kuwa CCM hakuna mafisadi sasa haya magamba yametoka wapi? Huyu dogo wala hakuchaguliwa na wana Bumbuli, alipata ubunge kwa kufadhiliwa na mafisadi papa yaliyowahonga wagombea wa vyama vingine wajitoe ili apite bila kupingwa. Lakini ungefanyika uchaguzi asinge pita kabisa.Huyu ni zao la mafisadi hawezi akawa na moyo wa uzalendo hata siku moja. Huyu hana tofauti na JK kwani aliingizwa ikulu na mafisadi na leo ndiye mlinzi mkubwa wa mafisadi.
 
January Makamba ni fisadi mkubwa, yeye na kamati yake wamewekwa sawa na TANESCO, istoshe hachoki kupiga simu TANESCO kuomba miradi ili aifadhili kupitia hela zake 'India'

January amemwomba MD wa TANESCO wammalize Ngeleja ili wizara ile apewe yeye, kifupi anamiradi kadhaa itaendeshwa thru 'ufadhili' wake

Ninasubiri siku ya kusomwa bajeti hii nimwage ushahidi jamvini ....kwasasa inatosha kusema JM si msafi! Hivyo asinyooshee kidole wengine!
 
MAOFISA WA JUU WATUHUMIWA KUIHONGA KAMATI YA MAKAMBA


WIZARA ya Nishati na Madini imeingia katika kashfa nzito ambapo baadhi ya maofisa wa wizara hiyo wanatuhumiwa kuwahonga baadhi ya wabunge katika Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini kwa kile kinachodaiwa kutaka bajeti ya wizara hiyo kupita kwa urahisi, Mwananchi limebaini.
Habari zilizopatikana kutoka Dodoma na Dar es Salaam zimedokeza kuwa taarifa za uovu huo tayari zimefikishwa mezani kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ambaye amesema atalishughulikia baada ya kuwa amewasiliana na Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja.
Kwa mujibu wa habari hizo suala hilo pia tayari limefikishwa kwa Spika wa Bunge, Anne Makinda na kwamba kamati ya uongozi ya bunge anayoiongoza pia imearifiwa kuhusu suala hilo.
Kashfa hiyo imeikumba wizara hiyo katika kipindi kigumu ambacho nchi iko gizani huku wizara hiyo ikilaumiwa kutokana na uhaba wa nishati ya umeme kiasi cha Waziri Ngeleja kutangaza mgawo wa saa 10 wakati wa mchana na saa sita wakati wa usiku "ni janga la kitaifa".
Habari zaidi zinasema miongoni mwa mambo muhimu ambayo kamati hiyo ilikuwa ikitaka maelezo ni mapendekezo ya wizara hiyo kutaka kujenga jeno la makao yake makuu jijini Dar es Salaam kinyume cha ilani ya CCM ambayo inaweka wazi kwamba hakutakuwa na ujenzi wa makao makuu ya wizara jijini humo katika kipindi cha miaka mitano ijayo.
Habari zilizolifikia Mwananchi zilidai kwamba, Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini ya Bunge, January Makamba ndiye aliyewasilisha malalamiko kwa Pinda na Makinda baada ya kubaini 'ulegevu' miongoni mwa wajumbe wa kamati yake wakati wa mchakato wa kujadili mapendekezo ya bajeti ya Wizara hiyo na kwamba mapema alikuwa ameishapokea taarifa kuhusu baadhi ya wajumbe wake kuhongwa.
"Mwenyekiti (January) alipewa taarifa za wajumbe wawili wa kamati yake ambao walikataa hongo hiyo, na baada ya kufanya uchunguzi alibaini kwamba kuna kila dalili kwamba baadhi ya wabunge katika kamati yake walikuwa wamebadili msimamo katika baadhi ya mambo," kilieleza chanzo chetu mjini Dodoma.
Habari zaidi zilidai kuwa kufuatia hali hiyo, January aliitisha kikao cha wabunge ambao ni wajumbe wa kamati yake na kugeuka mbogo, huku akiweka bayana kuchukizwa kwake na taarifa za wajumbe wake kuhongwa na kwamba alikwenda mbali zaidi akitishia kujiuzulu nafasi ya uenyekiti ili kutoa nafasi kwa wabunge hao kuchagua mwenyekiti mwingine ambaye atakuwa tayari kuvumilia uovu huo.
"Yule kijana (January) alikasirika sana, alichukizwa kweli kweli na hali hiyo kwa sababu ni kama wajumbe waliopokea hizo bahasha walikuwa wakimzunguka kwani tayari walikuwa wanajua nini wanachopaswa kufanya ili kuziokoa sekta za nishati na madini,"kilieleza chanzo hicho.
Kadhalika suala hilo la hongo lilijadiliwa katika kikao cha pamoja baina ya wajumbe wa kamati hiyo na viongozi wa Wizara ya Nishati na Madini, ambapo Waziri Ngeleja na Naibu wake, Adam Malima waliomba radhi kutokana na tukio hilo, hivyo kamati hiyo kuagiza maofisa wa wizara waliohusika wachukuliwe hatua.
"Ni kama Ngeleja na Malima walimalizana na kamati, si unajua maana ni kama January alikuwa peke yake, kama kulikuwa na wanaomsapoti (wanaomuunga mkono) walikuwa ni wachache, hivyo kama waziri na naibu wake waliomba radhi hakukuwa jinsi zaidi ya kumalizana nao," zilidai taarifa hizo na kuongeza:
"Hata hivyo Mwenyekiti na baadhi ya wajumbe walimwagiza Ngeleja na Malima kuwachukulia hatua maofisa waliohusika na ugawaji wa fedha hizo kwa baadhi ya wabunge".
Kauli za viongozi
Mwananchi liliwasiliana na January ili kufahamu undani wa suala hilo, lakini mbunge huyo wa Bumbuli hakukanusha wala kukubali kuhusu baadhi ya wajumbe wake kupokea rushwa.
"Nani kakwambia bwana, mimi siwezi kuzungumza lolote, mambo ya kamati jamani si yote tunayoweza kuweka wazi, lakini siku hizi hatufanyi vikao bila kuwaruhusu waandishi wa habari, kama hayo yangetokea si yangeonekana wakati huo?,"alihoji January.
Waziri Ngeleja kama ilivyo kwa January naye hakukubali wala kukanusha kuwepo kwa tuhuma hizo na badala yake alisisitiza kwamba anayeweza kuzizungumzia ni mwenyekiti wa kamati akimaanisha January.
"Unasikia, kama jambo limetokea kwenye kamati mimi sina mamlaka ya kulizungumzia hata kidogo maana nitakuwa navunja kanuni, kama wengine nilivyowaambia maana naona leo wengi wananitafuta kwa habari hii, mpigieni mwenyekiti wa kamati yeye ana mamlaka, mimi kwangu no comment (siwezi kusema chochote),"alisema Ngeleja kwa simu.
Spika wa Bunge, Makinda kwa upande wake pia alikanusha kupokea taarifa hizo. "Mimi ndiyo nazisikia kutoka kwako, pengine kama zimeletwa kwa barua sijaiona, lakini sifahamu kitu kama hicho," alisema Makinda alipozungumza kwa simu na Mwananchi.
Kwa upande wake Naibu Spika Job Ndugai alisema kuwa hana taarifa hizo kwa kuwa yeye alikuwa nje ya nchi kikazi. "Ndugu yangu, pengine ukimpata Spika anaweza kukusaidia, mimi nimerudi jioni hii (jana jioni) ndio naingia hapa Dodoma najiandaa kwa ajili ya kesho,"alisema Ndugai.

Source: Kashfa nzito Wizara ya Ngeleja


 
Back
Top Bottom