Kamati ya Maadili ya TFF yamsimamisha Haji Manara wa Simba kwa mwaka 1 na faini ya Milioni 9

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,266
8ac6da13b637ba3168f3025e78028eb8.jpg

Kamati ya Maadili ya TFF imemsimamisha Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Haji Manara kujihusisha na soka ndani na nje ya nchi kwa muda wa miezi 12 na faini shilingi milioni 9 vyote kwa pamoja

Mapema wiki hii TFF ilimfungulia mashtaka Manara kwenye Kamati hiyo inayoongozwa na Wakili Jorome Msemwa kutokana na kauli alizotoa wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari makao makuu ya klabu ya Simba SC.
 
Ni kutokana na makosa mbalimbali hukumu yake ni kifungo cha mwaka 1 kutojihusisha na mpira wa miguu na faini shilingi milioni 9.
 
Wamafurikoni fc mnachekelea nini sasa?
Issue ya Kagera mmeikalia kidete kama ya kwenu mnawaweza tu Africa Lione sio sisi na Alger walio waunganishia 4G.
 
8ac6da13b637ba3168f3025e78028eb8.jpg
Kamati ya Maadili ya TFF imemsimamisha Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Haji Manara kujihusisha na soka ndani na nje kwa muda wa miezi 12 na faini shilingi milioni 9 vyote kwa pamoja

Mapema wiki hii TFF ilimfungulia mashtaka Manara kwenye Kamati hiyo inayoongozwa na Wakili Jorome Msemwa kutokana na kauli alizotoa wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari makao makuu ya klabu ya Simba SC
Kosa na adhabu sina uhakika sana kama vinafanana. Ngoja nisubiri wajuvi wa mambo waje kudadavua.
 
8ac6da13b637ba3168f3025e78028eb8.jpg
Kamati ya Maadili ya TFF imemsimamisha Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Haji Manara kujihusisha na soka ndani na nje kwa muda wa miezi 12 na faini shilingi milioni 9 vyote kwa pamoja

Mapema wiki hii TFF ilimfungulia mashtaka Manara kwenye Kamati hiyo inayoongozwa na Wakili Jorome Msemwa kutokana na kauli alizotoa wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari makao makuu ya klabu ya Simba SC
Mbona heading na Content ni tofauti?
Pili kama ni kweli faini ni 9m/-, sidhan kama ana sababu ya kulipa hela za mtaji wa biashara! Ni bora akaachana na mambo ya mpira kuliko faini kubwa hivyo,ambayo sidhan kama ataimudu kwa usawa huu!
 
Tunamsubilia kwenye uchaguzi kisa kuambiwa ni nshomile ndio kumpa ban na mihela rundo kwani ni uongo kuwa rais na katibu wake ni nshomile.
 
Tatizo tunaowapa usemaji wa timu ni watu ambao hawana weredi na kazi hyo matokeo yake wanaropoka tu hovyohvyo,timu zetu ziangalie watu wa kuwapa nafasi hiyo. Haina tofauti na ulimi unavyoweza kuuponza kichwa
 
Back
Top Bottom