Kamati ya Maadili ya CCM ina wajumbe wangapi?

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
39,707
71,017
Ile kamati ya maadili iliyokaa siku mbili Dodoma ikiwasubiri Makamba na Kinana (pengine kwa kukosa usafiri) huku aliyetoka Mtama Lindi akiwahi, tumeambiwa iliamua kuonana na hao wazee Dar.

Lakini la ajabu, hakuna mjumbe yeyote aliyetambuliwa kuongea na hao wazee zaidi ya Mangula na Katibu Mkuu, Bashiru.

Je, haya yalikuwa mahojiano na kamati kama wanavyo aminishwa watu au yalikuwa mazungumzo ya agenda nyingine tofauti?

CCM ya sasa ikikutangazia kuwa kuna mvua kubwa inanyesha basi toka nje uhakikishe kweli kuna mvua kabla ya kuamini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiyo ndio kamati yenyewe?
IMG_20200211_053710.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakurekebisha usiyoyajua. Kamati ndogo ya usalama na maadili inaongozwa na makamu mwenyekiti wa CCM Ina wajumbe wanne lakini kamati ya usalama na maadili Ina wajumbe 12 na inaongozwa na mwenyekiti wa CCM.
 
Kamati ina wajumbe 11. Hapo naona wametumia busara baada ya wazee kudinda kuwa hawawezi kuhojiwa na vijana wadogo wadogo eti wakina Keisha, sijui Leila.

So hapo wajumbe wa kamati halali ni Mangula na Mzee kombo. Hata Bashiru sio mjumbe halali wa kamati ya maadili.
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom