Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria yaukataa muswada mpya, Waziri mwenye dhamana atimuliwa

kama ana hoja iliyomfanya abadili huo muswaada si ailezee na wanakamati muijibu kwa hoja,, kwanza yeye ndo mwenye dhamana ana mamlaka ya kufanya hvy,, Tatizo liko wapi au kwa kuwa Ni waziri kwenye Serikari inayoongozwa na CCM? ,, mlitaka afanyeje?,, kila ki2 imekuwa kulinda kulinda,, kama ni Misimamo hy hata KATIBA itoke Mbinguni bd hapatakuwa na Suluhu,, au hamuelewi Refa anayesimamia mchezo wa Maisha kati ya Wananchi NA mihimili mikuu ya nchi? ungewasilishwa na Upinzani ndo mngeukubali hata kama hawana mamlaka?, Cyo Tanzania tuitakayo jamani.
 
Hii siyo katiba mpya tunayoitaka bali ni mpya kwa upande wa CCM, ya kwetu tutaendelea kuidai ya kwetu....PIPOOOOOOOOOZ! mambo ya voda faster ccm wanayaingiza kwenye katiba, anyway akina Celina Kombani kwa uchache tu ni moja wa aina ya viongozi lukuki tulionao ambao ama uwezo wao ni mdogo au hawana uwezo kabisa.......watutolee mambo ya voda fasta hapa
 
Inaelekea kwamba bunge kama bunge lilitoa maelekezo yake na baadaye bi-kiroboto akatoa maelekezo yake ya kimagamba, ndiyo maana kombani anasema aulizwe bi-kiroboto

Nakubalian na wewe, yawezekana kabisa bi kiroboto aliingilia kati maana huyu bibi nae!
 
Naunga mkono hoja. Hakuna sababu ya kuwa na katiba ambayo haikidhi haja. Tena wakisumbua tutaikataa hata bungeni na refendum
 
Katika vipengele vyote kibaya zaidi ni kile kinachompa rais nguvu za kuteua bunge la katiba. Ananafasi ya kuteua wabunge mia na sita
 
nashanga sana katiba ya watanzania itakayo waongoza watu wa tabaka mbalimbali inaandaliwa na mtu mmoja tena mwenye akili za kubabaisha.nimuonavyo kombani hana sifa za kua waziri inakuaje anapewa kazi kama hiyo.
Kazi hiyo ni rahisi sana kama utasimamamia haki lakini kama utasimamamia masilai ya aliye kuweka madalakani utaonekana hufai na kazi utaiona ngumu
ninacho kishuutukia hapo ni kwamba huenda wamepanga kujivutavuta ili mchakato wa watanzania kupata katiba yao mpya usifanyikiwe kwa haraka na kama ni haraka basi iwe mbovu kuliko ya awali
eee mwenyezi mungu tusaidie Tanzania.
 
ole wenu ccm mnaodhani hii nchi ni yenu pekeyenu, mna muda mdogo sana wa kujirudi, inawezekana mmechelewa, enewei jaribuni kama mtawahi, hii dunia iko kama chungwa nyie mwangangania iko kama meza, msijesema sikuwaonya kabla!!!
Jamani eenhe, naomba tena naomba. Kama itatokea vurugu yoyote hapa nchi kutokana na upupu wa hawa magamba, nawaomba tena, huyu Kombani mniachie mie. Maana tusije kujikuta tunagombea kitoweo kimoja bure ndugu kwa ndugu.
 
Jamani eenhe, naomba tena naomba. Kama itatokea vurugu yoyote hapa nchi kutokana na upupu wa hawa magamba, nawaomba tena, huyu Kombani mniachie mie. Maana tusije kujikuta tunagombea kitoweo kimoja bure ndugu kwa ndugu.
Katika mazingira haya katiba mpya ni kiinimacho cha kuhakikisha katiba mpya haiji katika kipindi cha ******.
 
Back
Top Bottom