Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria yaukataa muswada mpya, Waziri mwenye dhamana atimuliwa

EasyFit

JF-Expert Member
Jul 4, 2011
1,269
1,082
  • Waziri Kombani atimuliwa
  • Atuhumiwa kubadili muswada wa Katiba mpya

WAZIRI wa Sheria na Katiba, Celina Kombani, juzi jioni alitimuliwa ndani ya kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria kwa madai ya kukiuka maagizo ya Bunge kuhusiana na muswada wa upatikanaji wa Katiba mpya ya nchi.

Akizungumza na Tanzania Daima Mbunge wa Muhambwe ambaye pia ni mjumbe wa kamati hiyo, Felix Mkosamali (NCCR-Mageuzi), alisema walifikia hatua ya kumtimua waziri huyo baada ya kubaini kuwa aliwasilisha muswada wa Katiba, badala ya kufanyia marekebisho vipengele kadhaa kama ilivyoamriwa na Bunge katika kikao cha Aprili, mwaka huu.

"Kwa mujibu wa kanuni za Bunge kifungu cha 84 na 85, muswada ukishawasilishwa bungeni ni mali ya Bunge, lakini kilichofanywa na waziri huyo ni kuandaa muswada mpya kinyume cha taratibu," alisisitiza Mkosamali.

Alisema kama waziri angetaka kuandaa muswada mpya alipaswa kuishirikisha kamati ya Bunge katika mchakato mzima kuliko alivyofanya kinyume na maagizo aliyopewa na Bunge ya kubadili baadhi ya vifungu na kuiweka katika lugha ya Kiswahili.

Mbunge huyo alisema mara baada ya kuwasilisha muswada bungeni ambao ulizua manung'uniko kutoka kwa wananchi wa pande zote mbili za nchi-bara na visiwani-hasa baada ya kugundua kuwa Rais amepewa madaraka ya uundaji wa Katiba mpya.

"Rais wa Tanzania analalamikiwa kuwa na madaraka makubwa mno na sasa katika uandikaji wa Katiba ya Watanzania wote bado anapewa kusimamia kila kazi inayohusiana na Katiba hii, hili hapana," alisema Mkosamali.

Akithibitisha kukataliwa kwa muswada huo Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Pindi Chana, alisema leo atatoa ufafanuzi kuhusu sakata hilo.
"Siwezi kusema sana juu ya hilo na hivi sasa ninaingia katika kikao cha IDEA ndugu yangu," alisema Pindi.

Muswada huo unaonyesha kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na ile ya Zanzibar (ZEC) bado zinapewa mamlaka ya kusimamia masuala ya kura ya maoni ya wananchi wakati wa kupitisha Katiba.

Katika muswada huo mpya mkuu wa wilaya na watendaji wa kata, vijiji na mitaa wamepewa kazi ya kusimamia taratibu za ukusanyaji wa maoni ngazi ya chini hali ambayo haikubaliki.

Akizungumza na Tanzania Daima kwa njia ya simu jana, Waziri Kombani alikiri kutimuliwa na kuongeza kwamba yeye hana hatia kwa vile amefanya kilichotakiwa na kuwataka wabunge wanaoupinga wamuulize Spika.

"Nimefanya lililo ndani ya uwezo wangu lakini hilo la kusema kama muswada mpya au la aulizwe Spika yeye ndiye msemaji wa mwisho kwenye hilo," alisema Waziri Kombani.
 
ole wenu ccm mnaodhani hii nchi ni yenu pekeyenu, mna muda mdogo sana wa kujirudi, inawezekana mmechelewa, enewei jaribuni kama mtawahi, hii dunia iko kama chungwa nyie mwangangania iko kama meza, msijesema sikuwaonya kabla!!!
 
aisee huyu asituletee upuuzi wake hapa hii nchi si ya watu wababaishaji. tunatunga katiba na sikutungiwa katibabna ccm
 
Kwa mtu ambaye amewahi msikia Martha Karua zamani waziri wa sheria na katiba Kenya na sasa Mutula Kilonzo utaelewa ni kwanini wenzetu wameweza na sasa wanasonga mbele! Najisikia aibu eti Celina Kombani ni waziri wetu wa Sheria na Katiba. Aibu inaongezeka zaidi pale AG wetu ambaye ni mwanasheria na jaji anapoinajisi taaluma yake ya sheria na kujikita katika ukada wa chama chake cha CCM.
 
Waache haraka kuchezea nguvu ya umma,tunataka katiba ya watanzania si ya Kikwete na marafiki zake kabla hatujaanzisha Tahrir square bongo,wakome kuchezea akili zetu
 
Waache haraka kuchezea nguvu ya umma,tunataka katiba ya watanzania si ya Kikwete na marafiki zake kabla hatujaanzisha Tahrir square bongo,wakome kuchezea akili zetu

Hivi Tahrir Square yetu ipo wapi? Au Arusha coz wale nina wahaminia 100%
 
Lakini ajabu ni kuwa jana kamati hiyo hiyo imetangaza kuukubali muswada huo. Kimetokea nini?
 
Huyu mama anaposema huu mswada kama ni mpya au la aulizwe spika mbona simwelewi? Kamati ya bunge imeugomea, huyu mama sijui anaweza nini kwenye hii wizara.
 
Waache haraka kuchezea nguvu ya umma,tunataka katiba ya watanzania si ya Kikwete na marafiki zake kabla hatujaanzisha Tahrir square bongo,wakome kuchezea akili zetu

Tahrir square ya bongo ianzie Mwanza na tunawahakikishieni itafanikiwa kwa sana tu, mtujuze kama muko tayari tufanye maandaliza, twaweza anzia viunga vya kirumba ambako nepi alionjeshwa tamu ya shubiri, rufiji au pale sahara nyamagana kwa kamanda wenje.Dar ni waoga .
 
Ni bora tuchukue hata miaka 20 ijayo kupata katiba mpya ya Watanzania sio kama hii ambayo
CCM wanataka kutuletea ya RAIS kuwa yeye ndiye ALPHA na OMEGA. I'm sick with JK and his
government au anataka na yeye apigwe na NATO akajifiche kwenye bomba la maji machafu
hapo ferry ndiyo ajue watanzania tumechoka kuchakachuliwa?
 
CCM NA TANZANIA TUNAYOITAKA, sina hakika kama huwa kina kombani wanafikiria yanayoweza kutokea baada ya hapo
 
Tahrir square ya bongo ianzie Mwanza na tunawahakikishieni itafanikiwa kwa sana tu, mtujuze kama muko tayari tufanye maandaliza, twaweza anzia viunga vya kirumba ambako nepi alionjeshwa tamu ya shubiri, rufiji au pale sahara nyamagana kwa kamanda wenje.Dar ni waoga .

Tuachieni wana arusha sisi ndo mwisho wa yote hawawezi kutupeleka puta hawa makuzi
 
haya sasa ccm mnapambana na nguvu ya uma
Inaelekea kwamba bunge kama bunge lilitoa maelekezo yake na baadaye bi-kiroboto akatoa maelekezo yake ya kimagamba, ndiyo maana kombani anasema aulizwe bi-kiroboto
 
  • Waziri Kombani atimuliwa
  • Atuhumiwa kubadili muswada wa Katiba mpya

WAZIRI wa Sheria na Katiba, Celina Kombani, juzi jioni alitimuliwa ndani ya kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria kwa madai ya kukiuka maagizo ya Bunge kuhusiana na muswada wa upatikanaji wa Katiba mpya ya nchi.

Akizungumza na Tanzania Daima Mbunge wa Muhambwe ambaye pia ni mjumbe wa kamati hiyo, Felix Mkosamali (NCCR-Mageuzi), alisema walifikia hatua ya kumtimua waziri huyo baada ya kubaini kuwa aliwasilisha muswada wa Katiba, badala ya kufanyia marekebisho vipengele kadhaa kama ilivyoamriwa na Bunge katika kikao cha Aprili, mwaka huu.

“Kwa mujibu wa kanuni za Bunge kifungu cha 84 na 85, muswada ukishawasilishwa bungeni ni mali ya Bunge, lakini kilichofanywa na waziri huyo ni kuandaa muswada mpya kinyume cha taratibu,” alisisitiza Mkosamali.

Alisema kama waziri angetaka kuandaa muswada mpya alipaswa kuishirikisha kamati ya Bunge katika mchakato mzima kuliko alivyofanya kinyume na maagizo aliyopewa na Bunge ya kubadili baadhi ya vifungu na kuiweka katika lugha ya Kiswahili.

Mbunge huyo alisema mara baada ya kuwasilisha muswada bungeni ambao ulizua manung’uniko kutoka kwa wananchi wa pande zote mbili za nchi-bara na visiwani-hasa baada ya kugundua kuwa Rais amepewa madaraka ya uundaji wa Katiba mpya.

“Rais wa Tanzania analalamikiwa kuwa na madaraka makubwa mno na sasa katika uandikaji wa Katiba ya Watanzania wote bado anapewa kusimamia kila kazi inayohusiana na Katiba hii, hili hapana,” alisema Mkosamali.

Akithibitisha kukataliwa kwa muswada huo Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Pindi Chana, alisema leo atatoa ufafanuzi kuhusu sakata hilo.
“Siwezi kusema sana juu ya hilo na hivi sasa ninaingia katika kikao cha IDEA ndugu yangu,” alisema Pindi.

Muswada huo unaonyesha kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na ile ya Zanzibar (ZEC) bado zinapewa mamlaka ya kusimamia masuala ya kura ya maoni ya wananchi wakati wa kupitisha Katiba.

Katika muswada huo mpya mkuu wa wilaya na watendaji wa kata, vijiji na mitaa wamepewa kazi ya kusimamia taratibu za ukusanyaji wa maoni ngazi ya chini hali ambayo haikubaliki.

Akizungumza na Tanzania Daima kwa njia ya simu jana, Waziri Kombani alikiri kutimuliwa na kuongeza kwamba yeye hana hatia kwa vile amefanya kilichotakiwa na kuwataka wabunge wanaoupinga wamuulize Spika.

“Nimefanya lililo ndani ya uwezo wangu lakini hilo la kusema kama muswada mpya au la aulizwe Spika yeye ndiye msemaji wa mwisho kwenye hilo,” alisema Waziri Kombani.
Huyu ndo yule wazziri ambaye Kichwa chake ilikuwa nazi/dafu? Maana alipinga katiba wazi wazi na leo anandika mswada wa kuianzisha ovyo ovyo. Kwani Kiwete haoni kuwa huyu mama hana capacity? Ataendelea kutwanga maji kwenye kinu mpaka lini?
 
Tahrir square ya bongo ianzie Mwanza na tunawahakikishieni itafanikiwa kwa sana tu, mtujuze kama muko tayari tufanye maandaliza, twaweza anzia viunga vya kirumba ambako nepi alionjeshwa tamu ya shubiri, rufiji au pale sahara nyamagana kwa kamanda wenje.Dar ni waoga .

kila wilaya wawe na tahrir Square yao maana nchi hii ni kubwa. Sisi wa Bongo kufika huko itakuwa kazi kubwa!!
 
Hawa wanatufanya sisi kama watoto wadogo. Waache kufanya masikhara katika mambo yanayohitaji umakini, la sivyo watu wataingia mtaani kwa kukosa uvumilivu!
 
Katiba ni mali ya wananchi kwahiyo ni lazima itokane na wananchi hili la kutaka itokane na Kikwete ahh sorry itokane na rais halitakubaliwa na watanzania wote
 
Back
Top Bottom