Kamati ya kudumu ya bunge iliitaja Acacia kuwa ni wakorofi kwenye kulipa kodi

jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
30,918
2,000
Naona Rais Magufuli anafanyia kazi ushauri wa kamati ya kudumu ya bunge ya nishati na madini.

Katika bunge mwaka 2015/16 Ripoti ya kamati hii inaitaja acacia na a.k.a zake zote kuwa ni kampuni ya madini iliyokataa kulipia kodi zilizowekwa kisheria na kimkataba...hii ni pamoja na kufuatiliwa na kutakiwa kufanya hivyo.

Hii ina maana ni kiburi chao wenyewe kilichopelekea kuliamshi Dubwana Magufuli.

Lakini pia ina maana ni kampuni isiyo na uadilifu linapokuja suala la ulipaji kodi hivyo ni sahihi kabisa mtu akisema kuwa wanatumia mbinu chafu kutuibia.

Madini ya Dhahabu
Mheshimiwa Spika,
uchambuzi wa Kamati umebaini kuwa migodi mikubwa ya dhahabu nchini hailipi kodi ya mapato (Corporate tax) kwa kisingizio cha kupata hasara endelevu katika uzalishaji. Hata hivyo kamati haikubaliani na sababu hiyo kwani taarifa zinaonesha kwamba makapuni yanayomiliki migodi hiyo yamekuwa yakipata faida kwenye masoko ya hisa ambako kampuni hizi zimesajiliwa.
Aidha, Ripoti ya TMAA ya mwaka 2015 inaonesha kwamba makapuni ya madini ya dhahabu hayakulipa jumla ya shilingi bilioni 10.27 kwaajili ya ushuru wa Huduma (Service Levy), na Mrabaha (Royalty) kwenye Halmashauri husika. Kamati inaitaka Serikali ifuatilie malipo ya tozo hizo.
Mheshimiwa Spika
, Kamati inasikitishwa na ulipaji mbovu wa kodi kwa mgodi wa ACACIA (zamani Baarick gold na African Barrick Gold) kwa kutolipa kodi ya zuio (Withholding Tax) na kodi ya mapato(Corporate Tax) kwa miaka minne hata baada ya kuamriwa na mahakama ya usuluhishi kulipa kodi hiyo inayofikia jumla ya shilingi bilioni 89.
Kamati inaitaka Serikali kuchukua hatua madhubutu juu ya mwenendo huo. Ili iweze kudhibiti ukosefu wa mapato kama ilivyotokea kwenye migodi ya Resoultena Tulawaka ambayo ilifunga shughuli za uchimbaji bila kulipa kodi stahiki[QUOTE/]

TAARIFA YA KAMATI YA BUNGE YA NISHATI NA MADINI 20 May, 2016 - Bukombe sasa
 
ZILLAHENDER MPEMA

JF-Expert Member
Apr 4, 2015
2,057
2,000
Naona Rais Magufuli anafanyia kazi ushauri wa kamati ya kudumu ya bunge ya nishati na madini.

Katika bunge mwaka 2015/16 Ripoti ya kamati hii inaitaja acacia na a.k.a zake zote kuwa ni kampuni ya madini iliyokataa kulipia kodi zilizowekwa kisheria na kimkataba...hii ni pamoja na kufuatiliwa na kutakiwa kufanya hivyo.

Hii ina maana ni kiburi chao wenyewe kilichopelekea kuliamshi Dubwana Magufuli.

Lakini pia ina maana ni kampuni isiyo na uadilifu linapokuja suala la ulipaji kodi hivyo ni sahihi kabisa mtu akisema kuwa wanatumia mbinu chafu kutuibia.Mgodi wa Buzwagi(ACACIA)kuna mstaafu mmoja ambaye kwa sasa hatajiki kwa kuwa kageuzwa "weapon of mass destructions" na amehifadhiwa kambini ana hisa za kutisha katika mgodi huo,kipindi cha uchaguzi mkuu alisafiri kimya kimya na kuja kujichimbia kahama kuhakikisha mh.Lembeli haendi bungeni kwa sababu aliamini maslahi yake yanaweza kuyumba ikiwa kahama ingeangukia mikononi mwa UKAWA.

"Kombora hilo la maangamizi ya umma"lilimwaga fedha nyingi kuhakikisha migodi yote inaendelea kuwa chini ya uwakilishi wa ccm bungeni,kutuambia kuwa hawalipi kodi ni hadaa tu,hata mukulu alisema tunawadai zaidi ya trilioni 200 ambazo zitatuwezesha watanzania wote kumiliki Noah lakini mwisho wa siku tumeshuhudia akikutana na mshirika wa serikali katika Wizi wa Rasilimali zetu na wameahidiana kulipana,Sasa unapokuja na hadaa za ukwepaji kodi wakati wenyewe walishamalizana,unaonekana kama mtu usiyejitambua na huiamini serikali ya chama chako.
 
jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
30,918
2,000
Mgodi wa Buzwagi(ACACIA)kuna mstaafu mmoja ambaye kwa sasa hatajiki kwa kuwa kageuzwa "weapon of mass destructions" na amehifadhiwa kambini ana hisa za kutisha katika mgodi huo,kipindi cha uchaguzi mkuu alisafiri kimya kimya na kuja kujichimbia kahama kuhakikisha mh.Lembeli haendi bungeni kwa sababu aliamini maslahi yake yanaweza kuyumba ikiwa kahama ingeangukia mikononi mwa UKAWA.

"Kombora hilo la maangamizi ya umma"lilimwaga fedha nyingi kuhakikisha migodi yote inaendelea kuwa chini ya uwakilishi wa ccm bungeni,kutuambia kuwa hawalipi kodi ni hadaa tu,hata mukulu alisema tunawadai zaidi ya trilioni 200 ambazo zitatuwezesha watanzania wote kumiliki Noah lakini mwisho wa siku tumeshuhudia akikutana na mshirika wa serikali katika Wizi wa Rasilimali zetu na wameahidiana kulipana,Sasa unapokuja na hadaa za ukwepaji kodi wakati wenyewe walishamalizana,unaonekana kama mtu usiyejitambua na huiamini serikali ya chama chako.
Nimekuwekea ripoti ya kamati ya bunge wewe unaongelea habari za vijiweni.
Hebu tulia wanaojua mambo watakuja kwa uchambuzi zaidi....
 
jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
30,918
2,000
Inashangaza hata wabunge wanaochangia mihadala ya makanikia wanashindwa kurejea mapendekezo ya kamati.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom