Kamati ya kuchunguza matokeo ya Shule ya Sheria inapokea maoni na ushauri kwa maandishi ili kuboresha mfumo wa elimu ya Sheria

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,586
217,977
Taarifa Hii imetolewa leo 18/10/2022 na Waziri wa wizara hiyo Mh Damas Ndumbaro

====

Kufuatia taarifa ya matokeo ya wanafunzi wa Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo ya hivi karibuni, na baada ya kuibuka kwa taharuki miongoni mwa wanajamii wakiwemo wanazuoni na wadau mbalimbali wa sekta ya sheria kuhusu ufaulu mdogo wa wanafunzi katika tasnia ya Sheria, tarehe 12 Oktoba, 2022 Mheshimiwa Dkt. Damas D. Ndumbaro (Mb.), Waziri wa Katiba na Sheria aliunda Kamati Maalum ya kufanya tathmini ya mfumo wa elimu ya Sheria nchini na changamoto zinazoukabili mfumo huo ikiwa ni pamoja na namna mafunzo ya uanasheria kwa vitendo yanavyotolewa.

Pamoja na mambo mengine, Kamati hiyo imepewa jukumu la kushauri namna ya kuboresha mfumo huo ili kukidhi mahitaji ya taaluma ya Sheria kwa lengo la kuwa na ushindani wa kitaifa na kimataifa. Kamati katika utekelezaji wa majukumu yake kwa mujibu wa Hadidu za Rejea ilizopewa, itapokea maoni kwa maandishi pia kuwasikiliza wadau mbalimbali ana kwa ana.

Kwa kuwa siyo wananchi wote watapata fursa ya kufika mbele ya Kamati kutoa maoni, Mhe. Dkt. Harrison G. Mwakyembe, Mwenyekiti wa Kamati anawaalika wananchi na wadau wenye mapenzi mema na uboreshaji wa mfumo wa elimu ya sheria nchini na elimu ya uanasheria kwa vitendo, kuwasilisha maoni kwa maandishi ili kuiwezesha Kamati kupata maoni mengi kadri inavyowezekana na hatimaye kushauri ipasavyo.

Mwisho wa kupokea maoni ya maandishi ni tarehe 24 Oktoba, 2022 saa 10:00 jioni.

Maoni hayo yawasilishwe kupitia barua pepe ya km@sheria.go.tz, mitandao ya kijamii ya twitter: @Sheria_Katiba; Instagram @katibanasheria_ au WhatsApp kwa namba 0742910529.

C0449B09-C006-4332-9332-E5B1168A76F5.jpeg
 
Tumechoka na matumizi mabaya ya pesa za walipa kodi wa nchi hii.

Kila siku tunapewa taarifa ya kuundwa kamati za uchunguzi.....

......Lakini hatusikii kila wakati,pale tunapopaswa kupewa taarifa ya kamati iliyomaliza uchunguzi na hatimae kuleta ripoti yake,ili umma ujuwe kilichotokea kwa uwazi na Ukweli.

Na pia tutangaziwe bajeti kamili iliyotumika kwenye zoezi zima la hiyo kazi.

Na kisha tutangaziwe kuvunjwa rasmi kwa tume toka kwa aliyekuwa ameiteua na kuituma kutekelrza kazi husika.

Kwa hiyo ....hakuna tija kuunda tume na kutumia gharama kubwa na kisha taarifa zake kuishia kuwa siri sirini.

Ni aina ingine ya ubadhilifu wa pesa za walipa kodi wa Tanzania.
 
Yani hizi ni siasa tupu wanalazimisha vilaza wawe wengi mtaani hili iwe rahisi kuwatawala kama mbuzi... mawakili wote siku hizi wanacho waza ni kugombea ujumbe CCM!
sijakuelewa.... vilaza (ingawa sipendi neno hili) kuwa wengi vipi?
 
Tumechoka na matumizi mabaya ya pesa za walipa kodi wa nchi hii.

Kila siku tunapewa taarifa ya kuundwa kamati za uchunguzi.....

......Lakini hatusikii kila wakati,pale tunapopaswa kupewa taarifa ya kamati iliyomaliza uchunguzi na hatimae kuleta ripoti yake,ili umma ujuwe kilichotokea kwa uwazi na Ukweli.

Na pia tutangaziwe bajeti kamili iliyotumika kwenye zoezi zima la hiyo kazi.

Na kisha tutangaziwe kuvunjwa rasmi kwa tume toka kwa aliyekuwa ameiteua na kuituma kutekelrza kazi husika.

Kwa hiyo ....hakuna tija kuunda tume na kutumia gharama kubwa na kisha taarifa zake kuishia kuwa siri sirini.

Ni aina ingine ya ubadhilifu wa pesa za walipa kodi wa Tanzania.
Tuliwaonya sana kwamba shetani hana rafiki lakini hamkuelewa
 
Ukiwa na kesi ya mchongo bora kumalizana na polisi ushahidi ukapotea kuliko kuwa na wakili kilaza ukaambulia mvua.

Wakili msomi abakie lisu, kibatala na rutashobolwa.
 
Pitia hapa Erythrocyte
Kama vile yanajibika..... but it is difficult to make any meaningful conclusion due to the sample size being small...
 

Attachments

  • LAW_SCHOOL_OF_TANZANIA_ORAL_EXAMS_BRIEF.pdf
    297.5 KB · Views: 3
How to Study Effectively For Law School Exams
  1. Create a finals study schedule. ...
  2. Complete your outlines and then work on memorizing them. ...
  3. Take practice exams. ...
  4. Focus on all the tiny details from cases. ...
  5. Work non-stop during finals weeks. ...
  6. Procrastinate!
 
Sekta nyingi wangekuwa wanaomba ushauri na kufanyia kazi tungekuwa mbali
Natumia neno kali, ni ukosefu wa maadili, haiwezekani mambo ya kitaalamu eti yaamuliwe ili kuwafurahisha wanasiasa. Mkitaka kujua elimu yetu ilivyo mbovu chekini tu jinsi wahitimu wa vyuo walivyo vilaza na wana mabonge ya ufaulu.
 
Back
Top Bottom