Kamati ya Jaji Bomani yatua Buzwagi

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,007
Kamati ya Jaji Bomani yatua Buzwagi

na Irene Mark
Tanzania Daima

KAMATI ya kupitia sheria na mikataba ya madini, iliyo chini ya uenyekiti wa Jaji Mark Bomani, kesho itazuru mgodi wa Buzwagi, mkoani Shinyanga.
Mbali na kuzuru kwenye mgodi huo, wajumbe wa kamati hiyo iliyoundwa na Rais Jakaya Kikwete, watafanya mkutano wa hadhara na kuzungumza na wananchi, ili kupata maoni yao.

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyopatikana Dar es Salaam jana, ilieleza kwamba awamu ya pili ya ziara za kamati hiyo ilianza rasmi Januari 3, mwaka huu.

Taarifa hiyo iliyosainiwa na Jaji Bomani, inataja mikoa itakayotembelewa na kamati kuwa ni Shinyanga, Mwanza, Mara, Arusha, Iringa na Mbeya.

“Napenda kuwaarifu wananchi wa mikoa hiyo na wengine watakaoweza kufikisha maoni yao kwenye kamati hiyo kuwa wazi ili kusaidia kazi za kamati,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.

Pamoja na Buzwagi, maeneo mengine yatakyotembelewa na wajumbe wa kamati hiyo ni Kishapu, Nzega, Maganzo, Kahama, Kakola, Geita, Nyakabale, Rwamgasha na Mwanza.

Sehemu nyingine ni Tarime, North Mara, Musoma, Nyamongo, Arusha, Merelani, Tukuyu, Mgodi wa Kiwira na Liganga.

Kamati hiyo yenye wajumbe 12 iliteuliwa Novemba 13 mwaka jana, ikiwa ni ahadi ya Rais Kikwete ya kufanyia marekebisho sekta ya madini kwa lengo la kuiboresha.

Mbali ya Bomani wajumbe wengine wa kamati hiyo ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto (CHADEMA), Mbunge wa Bariadi Mashariki, John Cheyo (UDP) na Mbunge wa Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe (CCM).

Wengine ni Mbunge wa Msalala, Ezekiel Maige (CCM), mwanasiasa mkongwe Iddi Simba, Peter Machunde anayetoka Soko la Hisa, Dar es Salaam na David Tarimo, Kutoka Kampuni ya Price Water Coopers.

Yumo pia Maria Kejo, ambaye ni Mkurugenzi wa Madai na Sheria za Kimataifa kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, Mwanasheria wa Wizara ya Nishati na Madini, Salome Makange, Kamishna wa Sera Wizara ya Fedha, Mugisha Kamugisha, na Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Makazi, Wizara ya Ardhi, Edward Kihundwa.

Hadidu za rejea za kamati hiyo ni kupitia mikataba ya madini na nyaraka nyingine zinazohusu migodi mikubwa na kuchambua mfumo wa kodi unaotumika katika sekta ya madini.

Aidha, itapitia mfumo wa usimamizi wa shughuli za uchimbaji mkubwa unaofanywa na serikali, itachambua na kuainisha haki na wajibu wa mwekezaji na mwenye rasilimali (serikali), na pia itakutana na Chamber of Minerals na wadau wengine.




 
Chama chenye wabunge wengi badala ya CCM ni Chama gani,hivi hapakuwa na umuhimu wa kumuweka japo mmoja toka kwenye Chama hiki,inaonyesha wazi hawa walikuwa na ule mpango uliosemwa wa kumpagawisha Zito na uroda wa fedha za matumizi mpaka alewe nazo na hapo ndipo watakapotimiza lengo na madhumuni ambayo yatazima kelele za walala hoi.Huwezi kujua !!!
 
Back
Top Bottom