Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,410
Madawati hayo yalikabidhiwa kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Jordan Lugimbana chini ya Mwenyekiti wa Kamati ya harusi Philbert Rwakilomba ambaye alisema kuwa madawati hayo yalikuwa na thamani ya Sh1.6 milioni.
Dodoma. Shule ya Msingi Chang’ombe B katika Manispaa ya Dodoma imepokea madawati 21 yaliyochangiwa na Kamati ya harusi kwa lengo la kuunga mkono juhudi za Serikali.
Madawati hayo yalikabidhiwa kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Jordan Lugimbana chini ya Mwenyekiti wa Kamati ya harusi Philbert Rwakilomba ambaye alisema kuwa madawati hayo yalikuwa na thamani ya Sh1.6 milioni.
Richard Masesa ni mfanyakazi wa Ofisi ya Rais Tamisemi ambaye alifunga ndoa na Miriam Emmanuel Mei 29, 2016 na sherehe kufanyika katika ukumbi wa kilimani mjini Dodoma.
Akipokea mchango huo, Lugimbana alisema kitendo kilichofanywa na kamati hiyo ni cha mfano wa kuigwa na watu wengine kwa ajlili ya kujiwekea kumbukumbu za kudumu katika matukio yao.
“Niwapongeze sana kwa uamuzi huu ambao naweza kusema ni wa kimuujiza, pamoja na sherehe ya harusi mkaona kwamba sehemu ya pesa mhifadhi kwa ajili ya mchango kwa jamii, hongereni sana,” alisema Lugimbana.
Chanzo: Mwananchi
My take: Shime na wengine kamati zenu zichangie hata vitabu