Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge imependekeza Jerry Silaa kuondolewa kwenye Bunge la Afrika (PAP) na kutohudhuria vikao 2 vya Bunge

Ss Jr

JF-Expert Member
Jan 15, 2018
577
450
Jerry Silaa

KAMATI ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, imemkuta na hatia Mbunge wa Ukonga (CCM), Jerry Silaa, katika tuhuma za kudharau mhimili huo na kupendekeza asimamishwe kuhudhuria mikutano miwili mfululizo, pamoja na kuondolewa uwakilishi wa Bunge katika Bunge la Afrika (PAP).

Mapendekezo hayo yametolewa leo Jumanne, tarehe 31 Agosti 2021, bungeni jijini Dodoma na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Emmanuel Mwakasaka, akiwasilisha taarifa ya uchunguzi dhidi ya tuhuma zilizokuwa zinamkabili Silaa, za kudharau mhimili huo pamoja na kuuchonganisha kwa wananchi.

Akisoma taarifa hiyo, Mwakasaka amedai kwamba Silaa wakati anahojiwa hakuomba radhi wala hakujutia makosa aliyoyafanya kitendo kilichotafsiriwa kwamba ana mwenendo usiofaa na unaodhalilisha hadhi ya nafasi ya mbunge kwa kusema uongo na kuwachonganisba wananchi na Bunge.

“Kwa kuwa Silaa mbele ya kamati hakukiri wala kujutia makosa yake, alionesha dharau na kudhaliliisha hadhi ya bunge, kuchonganisha Bunge na wananchi. Hivyo kamati imemtia hatiani,” amesema Mwakasaka na kuongeza:

“Na kwa kuwa kanuni za kudumu za Bunge toleo 2020 inaipa Bunge mamlaka ya kupokea na kujadili mapendekezo ya kamati, linaadhimia kuwa Jerry Silaa asimamishwe kuhudhuria mikutano miwili ya Bunge mfululizo na aondolewe kwenye nafasi ya uwakiliwa wa Bunge PAP.”
 
wauane tu si wako wenyewe kwani kuna shida gani hata wakiaua kuonyeshana maujuzi kama yale ya mama J wa Yanga waendelee tu , p[osho zao nchi yao makalio pia yao kwani kuna ishu unadhani? waendelee tu huku miwanananchi ikiendelea kupiga makofi tu
 
“Kwa kuwa Silaa mbele ya kamati hakukiri wala kujutia makosa yake, alionesha dharau na kudhaliliisha hadhi ya bunge, kuchonganisha Bunge na wananchi. Hivyo kamati imemtia hatiani,” amesema Mwakasaka na kuongeza:
Ni "makosa" yapi aliyotenda Jerry?
 
Naona hao wahalifu wa CCM watalipwa nusu mshahara, kwani wale wa upinzani walikuwa wanalipwa nusu mshahara wakiadhibiwa na Ndugai?
 
Na hili walishangilia sana lilipo tajwa, wamvue basi wampe kibajaji lakini wasisahau naye alishasema ataongea anachokiamini wakitaka wamchague kwenye kamati kuu CCM ama wamnyie kura ni hiari yao lakini alishasema alichokuwa akikiamini.
 
Back
Top Bottom