Kamati ya Fedha ya Bunge PAC yatoa tamko: ATCL iko mahututi, itakufa hivi karibuni

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
11,129
18,741
Katika kuthibitisha kile ambacho wanasiasa wa upinzani na wananchi kwa ujumla wamekuwa wakikipigia kelele siku zote na serikali kujifanya kiziwi haitaki kusikia, makamu mwenyekiti wa Kamati ya Fedha ya Bunge, Japhet Hasunga, ametoa tamko rasmi kwamba shirika la ndege la Tanzania ATCL liko mahututi na litakufa hivi karibuni.

Itakumbukwa kwamba suala la mkurupuko katika kulifufua shirika la ndege la Tanzania, ATCL, ni jambo lililosemwa sana na watu wa upinzani na Watanzania kwa ujumla, lakini CCM na serikali iliyopo madarakani siku zote hawakutaka kusikiliza na kukebehi ushauri na mapungufu yaliyokuwa yakitolewa na wadau hao.

Kwa kauli hii ya kamati ye fedha, inadhihirisha mtazamo kwamba sio kila ushauri unaotolewa na upande wa upinzani ni mbaya na unapaswa kubezwa kwamba ni harakati za upinzani kupinga kila kitu.

Nukuu ya maneno ya Makamu mwenyekiti wa kamati ya fedha PAC juu ya kuwa mahututi na kifo cha ATCL hivi karibuni iko hapa chini.

1630310363141.png

Tafsiri; "ukichukua madeni yote ya ATCL, yanayofikia 472.8bln/-, na mtaji wa mali za shirika ambazo ni 256.2bln, na ukatoa thamani ya madeni toka mtaji, wanabaki na mtaji ambao ni deni wa 216.6bln, alifafanua (Hasunga), akisisitiza kwamba hii ni dalili kwamba ATCL iko mahututi na itakufa hivi karibuni"

Jambo moja ambalo kamati ya fedha imeliongelea kwa namna ya kukosoa sana na kuonyesha kuwa ni mojawapo ya chanzo cha matatizo ya ATCL ni suala la kwamba ndege za ATCL sio zao ni za serikali kwa hiyo kwa namna fulani ATCL wanakuwa hawana mamlaka kamili kusimamia ATCL, bali mamlaka hayo yako Wizara ya Usafirishaji. Hii ni pamoja na matengenezo na matumizi ya ndege za ATCL. PAC imeeleza kuwa hawawezi kutoa maagizo moja kwa moja bali lazima wapitie kwa Katibu Mkuu Wizara ya Usafirishaji.

Angalia:

Kwanini Rais Samia anatumia ndege za ATCL kwa safari zake hata fupi badala ya ndege ya Rais?


Kwa habari kamili fuatilia

 
Prof Assad (The Genius) aliyaona haya kuanzia kipindi cha JK, na akashauri shirika lisifufuliwe na ni heri lianzishwe shirika jipya ndio ndege zinunuliwe hilo shirika la ATCL liachwe life na madeni yake. Alishauri ndege zisinunuliwe kwa hela taslimu kwasababu ni long-term project itakayolipa taratibu na kwa miaka mingi.

JK alimuelewa Prof Assad na ndio maana akaachana na ATCL, ila alivokuja yule kichwa maji akaona sifa sana kununua mi-ndege kibao kwa hela taslimu kwa kukamua wananchi na wafanya biashara. Akaona haitoshi amfanyie figisu na kile kijeba cha bungeni ili Prof Assad aondoke kama CAG.

Hakika Prof Assad aliwazidi akili na maono kina Kichwa Maji na jopo lake lote la washauri, watendaji, bunge na mawaziri.

Sasa hivi ni mwezi wa tatu ATCL hakuna timetable sahihi ya safari zao, unaweza ukakata ticket ya leo na ndege ikaondoka kesho kutwa, ukiuliza unaambiwa kulikua na matengenezo ya ndege. Unaweza ukakata ticket ya kwenda KIA ukapelekwa mwanza.

Yule "Mtakatifu Kichwa Maji Wa IIX" alikuja kushtuka kwamba amefanya upuuzi kiwango cha lami baada ya kuliingiza taifa kwenye hasara ya kununua ndege hizo 12 za ATCL, alishajua kafanya utopolo, ndio akaanza kujisemea nikiondoka mimi hizi ndege zote watakaokuja wataziuza. Kumbe alishajua kafanya upumbavu utakaokuja kuli gharimu taifa, watu wakamuita Nabii.

Hizi lawama sio za Bi Kidude, yeye ametwaa fuko la mavi tu kutoka kwa Kichwa Maji na alikua hana budi zaidi ya kulibeba kichwani. Sasa linampasukia kichwani.

Matokeo yake;

1) Kodi zimepanda maradufu.

2) Tozo zimepanda maradufu.

3) Kilimo zimewekwa kodi maradufu.

4) Ajira hakuna.

5) Nyongeza za mishahara hakuna kwa miaka 6 sasa.

6) Malimbikizo Ya Wastaafu na waliofukuzwa kazi hakuna kwa miaka sasa.

7) Serikali haina vyanzo vya mapato, zaidi ya kubuni njia za kukamua raia kila kukicha.
 
Sirro yupo atamrudisha madarakani
Sirro huwa anasoma upepo wa wananchi waliowengi. Mara nyingi kazi zinazokuwa zimefanyika na ahadi za kazi mpya huwa zinatosha kuwapoza machungu raia waliowengi. Subiri hao raia waliovumialia waambiwe na ATCL imekufa, elimu bure kwa heri, huko zahanati habari za madawa wananchi wanajua yanayoendelea, kitaumana!
 
ahaaaa kumbe ndiyo maana wananchi tunatwishwa maharaka haraka matozo ya ajabu ajabu na hii serikali ya CCM, kumbe wana agenda yao juu ATCL!!!!
 
Kwisha habari.
Mataga Pori mtaambia nini watu?
Watatuambia nini tuwaelewe kimburutuku wale wasiosikia ushauri?

Walishauriwa na Prof Assad ila yule Mtakatifu Kichwa Maji Wa 11X akajiona yeye ndio ana akili kuliko raia millioni 60.

Mi sina muda mrefu ntapigwa Ban humu JF kama kuna mdudu atajitokeza kutetea upuuzi uliofanyika wa kununua mi-ndege kibao kwa hela cash na kufufua shirika marehemu kama hilo ATCL, kwa hela ambazo zilipaswa kufanya mambo mengine ya msingi kama kuongeza mishahara walimu na kulipa mafao ya wastaafu sambamba na walioachishwa kazi (NSSF na PSSSF).
 
Kwahiyo wewe ndondocha unawaza uchaguzi tu maishani mwako?
Tuchote mabilioni kuendelea kuwekeza kwenye biashara inayoleta hasara kwa miaka mitano yote huku watoto wa shule ya msingi wakikaa mpaka 200 katika darasa moja?
Rais Samia usikubali ATCL ikufe mikononi mwako, itatupa kazi ngumu kuwashawishi wananchi for relection 2025
 
Back
Top Bottom